Ubora hafifu wa vichuma vya kufungua na kufunga gesi kwenye mitungi midogo

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,722
2,073
Sijui ni mimi tu ndio naona hili au kuna wapo wengine mmeona hivi vichuma vya kufungua na kufunga gesi kabla ya kuwasha kwenye mitungi midogo.

Sivijui jina lake kwa kingereza au kiswahili wee elewa ivo tu nilivoandika.

Ubora wa hivi vichuma nina mashaka nao kama uko sahihi na sijui pia kama hapa nchini pia vipo vinatengenezwa

Labda mimi nanunua vya bei ndogo lakini kama vipo vya bei kubwa ambavyo ni vizuri zaidi wadau kama mpo tujuzeni.

Lakini kwa majiko hatari kama ya gesi suala kutengeneza vitu feki ni hatari sana kwamba eti utachagua cha bei ndogo ili usave bajeti.

Mi naomba serikali ijaribu kuangalia haya majiko na ubora wake.Shirika la viwango tanzania Tbs lijaribu kufuatilia haya majiko hasahasa hivi vichuma.

Mitungi iko imara sana hofu yangu ni hivi vichuma jamani tusicheze na majiko ya gesi tusilete masihara kabisa. Juzi kuna mtu kaleta uzi hapa kuna familia ya watu 4 imepoteza maisha kwa haya majiko.

Kuna vitu vya kununua feki vya bei rahisi au vizuri vya bei kubwa lkn sio kwa haya majiko.Ni sawasawa na kuziba pancha tairi la ndege.

Au unaenda dukani kununua tairi feki la gari unasema nasave bajeti.

 
ubora ni pesa yako tu. vipo vya tshs. 5,000/- havimalizi miezi sita vinakuwa vishaharibika na kuanza kuvujisha gesi na vipo vya elfu 15 ndo mwisho wa matatizo. wewe ulinunua cha tshs ngapi?
 
Kweli aisee juzi kati kuna binti wa kazi akati anazima gesi kikakatika afu moto ukajiongeza, ikabidi akimbie nje kuita watu, tukatoa jiko nje, tukalifunika na sufuria ndipo likazima, ikabidi kichuma kibadilishwe, vibovu sana hivi vichuma
 
Back
Top Bottom