Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,024
Nzi
unapoteza muda wako
article ndeefu kisa unataka kum dis mtu?
unafahamu journals ngapi dunia hii?
unafikiri waalimu wa UDSM ni vilaza? ulizia mkuu
suppose sio au hana elimu au hana ubobezi, unachotaka kusema nini hasa
Ni naibu spika, wewe haujawa, ni PhD holder wewe hauna,ni notable figure wewe ni NZI TU
Mkuu kwa nilivyoona mimi binafsi sikudhani kama msingi wa hoja yako ya KUBOBEA umejikita kwenye "machapisho" sababu kwanza kitendo tu chakuwa na PHd kina maana lazima utakua na machapisho, swala la kuyaweka mtandaoni au la hakufanyi mtu kuwa mbobezi
Lakini pili swala la machapisho kuwa cited bado inategemea na chanzo cha habari yako ambacho kililalia zaidi oline, kwa mazingira yetu ya kibongo
Pengine nikubaliane na wewe kwamba kupitia online Dr Tulia hajafanya vizuri sana, nakushauri jaribu kwenda mbali zaidi kwenye utafiti wako mkuu kutafuta data zingine zaidi ya online naamini utapata kitu na utakua katika kipimo kizuri cha kujua ubobezi wake
Natamani sana JF tungekuwa tunapata threads kama hizi so often.
Sawa leteni sasa na Machapisho ya Tundu Lisu halafu tulinganishe!
Lakini mkuu Kama mpaka karne ya leo utafiti wako hauwezi kuwa online si kuna tatizo hapo? Most of the consultancy for example zinaanzia online, sasa kama hayupo online atakuwa active kweli?
Sasa hii kazi ya Tundu Lissu tumekuchagua wewe ukafanye utafiti ulete hapa tuutazame kiroho safi.
In short burden of proof kuwa Tundu lisu sio mbobezi kwenye sheria iko mikononi mwako.
Ni muhimu watu wakajua kwamba ubobezi mwanataaluma na mtemdaji au practioner unatofautiana. Sina hakika Kama Lisu ni mwanataaluma.
Hivi kuna kesi yoyote aliisha wahi kushinda.??
Muungano wa taaluma na siasa ni recipe ya hatari sana kwa nchi yetu.
Sikushangaa kusikia kuwa Dr Kigwangala anamalizia PhD
hivi kuna kesi yoyote aliisha wahi kushinda.??
Uko sahihi mkuu. Journal zote muhimu ziko online na paper zao zote unasema kuzipata ama bure au kwa kununua cash/annual subscription ya mtu binafsi au taasis. Ila journal nyingi za nchi zetu hazipo online na hazina impact factor. Kwa mtaalamu makini utapeleka huko chapisho lako kama limekataliwa na journal makini au kama linafaa kwa matukizi ya ndani.
Ni muhimu watu wakajua kwamba ubobezi mwanataaluma na mtemdaji au practioner unatofautiana. Sina hakika Kama Lisu ni mwanataaluma.
Mkuu nzi kwa wenye akili wamekuelewa vizuri sana! Huo ubobezi wa kanuni za bunge alifanyia bunge gani au lile la siki 90? Mbona alikua benchi? Kazi ya ubobezi wa kutafsiri sheria za nchi hua ni kwa mawakili waliohangaika na kesi za mashtaka miaka mingi kama kina Lissu na Change! Sasa huyu binti uwakili wake practical ilikua ya kesi ngapi?Mazee, asante kwa hii video. Napenda sana alichokisema kuanzia dakika ya 2.20 hadi 2.44. Amesema:
"...ninajiamini, nina uwezo na kazi ya naibu spika na spika ni kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na pia katiba. Na mimi haya ndiyo maeneo ambayo nimebobea kikazi"
Amebobea kikazi kwenye kutafsiri kanuni za Bunge, sheria za nchi na katiba?!? Haya wanamwona huyu ni mbobezi katika maeneo hayo walete ushahidi. Maana kwenye utafiti huo usio rasmi, sijaona kubobea kwake.
Huyu bidada hajielewi kumbe! Hakika hii ni mbeleko. Angebaki kufundisha tu sheria au kuwa naibu mwanasheria mkuu...maana hapo Bunge kuaibika kwake is bound to happen. Na yeye ni mfano wa 'wabobezi' na 'wasomi' wajanja waliojaa Tanzania chini ya CCM.
Wataalamu wa lugha wangetuambia kuwa neno "kubobea" lina maana gani? Baada ya hapo tusome bango la mkuu Nzi.
Kubobea kwa kiingereza lina maana ya "specialization". Dr. Tulia Akson amebobea "specialized" katika maswala ya sheria. Sioni kuna kosa. "Daktari amebobea kwenye magonjwa ya wanawake", n.k . Labda kama mnataka kuleta siasa, lakini Dr. Tulia amebobea kwenye maswala ya sheria.
Hivi tukimchukua Dr.Tulia tukamlinganisha na Mh.Ndugai na mama Makinda mathalani, hivi hawa kwenye ubobezi wa sheria wapo sawa? Hivi hili neno kubobea nd'o linalotoa mtu roho kujaribu kufanya mjadala usioisha? Basi tufanye DrTulia ni msomi mzamivu wa sheria hajabobea kama ambavyo inaonekana Nzi,Nyani Ngabu and Co hilo linawatesa sana. Manake hata tujadili vipi habari haibadiliki nd'o naibu spika sasa yupo anakula bata sasa. Na si mbobezi.