Ubishi kati ya Scania, Vs Benz Vs Daf Vs Iveco stralis Vs Howo

Ubishi kati ya Scania, Vs Benz Vs Daf Vs Iveco stralis Vs Howo

Ibang

Senior Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
121
Reaction score
25
salaam

kwa mazingira yetu hapa Tanzania Malori hayo Matano yapi yako imara, na yenye matumizi mazuri ya mafuta pia yenye upatikanaji wa spea kwa urahisi bila kusahau bei zake

Kundi moja la watu linasema
1) Scania

kundi la pili linasema mjerumani ni mjerumani tu
2) Benz

Kund la tatu wao wanakwambia
3) Iveco Stralis

kundi la nne wao wanawa admire wachina wanakwambia
4)Howo

kundi la tano wanakwambia mholanzi ndio kila kitu so wana recommend
5)Daf
na ni series gani kati ya magari hayo mtu una recommend mtu anunue?

natanguliza shukrani

umemsahau kitu cha mswideni, volvo au internatonal
 
kaka naomba nichangie mada yako nipo nchini Ujerumani kwa sasa mwaka wa3 nasoma magari,tafadhari Benz mwisho tena akigiza kutoka kiwandani hapa ujerumani..ni mwisho wa mkkono yote hiyo uliyoitaja..ila sio mtumba.
maana huku mpaka uitwe mtumba ni 25 miaka..jaribu utasema ndio..
 
Kwa upande wa nguvu, Volvo ndio the world's record kwa sasa ikiwa na 750 power, ikifuatiwa na scania v8 730 power! All in all msisahau American trucks kama INTERNATIONAL na MAN!
 
salaam

kwa mazingira yetu hapa Tanzania Malori hayo Matano yapi yako imara, na yenye matumizi mazuri ya mafuta pia yenye upatikanaji wa spea kwa urahisi bila kusahau bei zake

Kundi moja la watu linasema
1) Scania

kundi la pili linasema mjerumani ni mjerumani tu
2) Benz

Kund la tatu wao wanakwambia
3) Iveco Stralis

kundi la nne wao wanawa admire wachina wanakwambia
4)Howo

kundi la tano wanakwambia mholanzi ndio kila kitu so wana recommend
5)Daf
na ni series gani kati ya magari hayo mtu una recommend mtu anunue?

natanguliza shukrani

HOWO ndio mpango mzima.
Kuna jamaa mmoja anamiliki kampuni ya LAKE GROUP yenye kampuni tanzu kama 5 hivi pale Mikocheni, opposite na chuo cha kodi.
Hizi HOWO anazo kama 200 hivi. Ngoja nitafute namba yake anipe ushuhuda
 
Kwa upande wa nguvu, Volvo ndio the world's record kwa sasa ikiwa na 750 power, ikifuatiwa na scania v8 730 power! All in all msisahau American trucks kama INTERNATIONAL na MAN!

Mkuu nasikia Volvo ni vimeo zinaharibika sana ni kweli? au ni mafundi wetu bongo hawazijui?
 
Benzi ndo mpango mzima,unakutana na zile actros kama za TBL gari imebeba tani 32 lakini inakimbia kama coaster !!
 
Unapozungumzia Tanzania na malori, hakuna kitu kinaikaribia Scania. Kuna sababu kadhaa. Kwanza, Scania ni miongoni mwa malori bora zaidi kutengenezwa duniani katika vigezo vya uimara, nguvu na matumizi mazuri ya mafuta. Lakini kikubwa zaidi ni urahisi wa upatikanaji wa spea na mafundi wanaomudu kuzifanyia matengenezo Scania. Hii ni sababu kubwa kwanini ni nadra sana kuona lori la Scania likiwa juu ya mawe Tanzania kwa ukosefu wa spea. Hata leo hii kuna malori ya Scania modeli 111 na 81 ambayo bado ni mazima na yanafanya kazi zaidi ya miaka 30 tangu yalipotengenezwa.
 
Back
Top Bottom