Kuna ubinafsi mkubwa ambao unashangaza wengi sana kwenye nchi zetu za Afrika na zinazoendelea. Mfano kwenye magari ya Serikali mimi naishi state ya Texas magari mengi ya Serikali ya hili jimbo ni Ford, Toyota, Nissan, Jeep .
Cha ajabu ukienda kuulizia Toyota wenyewe wanakwambia Gari za hapa USA zina viwango vya juu zaidi ya zile VX zinazotumwa Afrika! hata finishing za gari za huku ni mzuri na wa viwango vya juu sana. Bei kwa haya magari mapya ni kati ya $40,000-$50,000 kwa gari jipya toleo la 2021.
Cha ajabu serikali inanunua magari kati ya Tsh 220,000,000 mpaka 400,000,000 ambayo ni $98,000 mpaka $178,000. Hakuna sababu ya msingi kuona mpaka vyama vinanunua magari kwa pesa hii wakati sio yao ni pesa za wananchi.
Hivyo hapa naongelea matumizi ya Serikali sio binafsi. Kibaya zaidi magari mengi hayatumiki vilivyo hayaendi hata mbali!. Mshahara wa mfanyakazi wa Africa kwa wastani ni $200 kama tsh 500,0000 tu hivyo gari moja tu ina uwezo wa kulipa watu 40 laki tano kila mwezi kwa mwaka mzima! hebu jiulize.
Wakati huku unakuta mtu anatengeza $100,000 kwa mwaka na ananunua gari ya $25,000 tena kwa mkopo wa miaka 5. Sasa tutapigana madongo lakini nchi zetu bado zina matumizi mengi sana mabaya na viongozi wengi hawana uchungu na pesa za wananchi kama wanavyodai