Uber itaanza kuweka matangazo kwenye App yake

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
web 2 copy 2.jpg


Uber itaanza kuweka matangazo katika app zake mbili, app ya Uber ambayo inatumika kuita usafiri (gari, bajaji, pikipiki n.k) na katika app ya Uber Eats. Watumiaji wa app hizi wataona matangazo wakati wa kutafuta usafiri, kusubiri usafiri kufika na wakati wa safari.

Matangazo (Ads) yatakuwa ni sehemu kubwa ya kibiashara katika Uber. Tayari matangazo yalianza kwenye app ya Uber Eats mwaka jana kama sehemu ya majaribio na idadi ya kampuni ambazo zimefanya matangazo zilizidi 345,000.

Uber imesema biashara ya matangazo itasaidia kuongeza faida, kwa wastani watu wanasubiri usafiri kwa dakika 15; na watu wanatumia dakika 2 mpaka 4 kutazama app ya Uber kuona dereva atafika muda gani na hii itakuwa ni nafasi kubwa kwa Uber kuweka matangazo kwa urahisi.

Pia Uber ina faida kubwa ya kuweka matangazo kuendana na maeneo ambayo unaenda na maeneo ambayo umewahi kutumia usafiri wa Uber. Hivyo itakuwa ni platform ambayo itapata faida kubwa hasa katika matangazo ya Hoteli, Migahawa, Maduka na maeneo ya kutembea.

Kwenye mfumo wa majaribio, Uber inajaribu pia kuweka matangazo kwenye app ya dereva na tablets za magari ambazo zinatumia app ya Uber. Matangazo yatakwepo kwenye simu na tablets.

Bado haifahamiki mabadiliko haya yatawanufaisha vipi madereva ambao wanatumia app hii kupata kipato. Haifahamiki kama Uber itagawana nao faida au itakuwa inachukua faida ya matangazo bila kugawana na madereva.
 
Back
Top Bottom