Kampuni ya Uber Kuanza Kutoa Huduma Tanzania

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
155
112
IMG-20230118-WA0024.jpg


Meneja wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Imran Manji akizungumza wakati wa kutambulisho ujio mpya wa Kampuni ya Uber kuanza tena kutoa huduma zake nchini Tanzania.
---
Kampuni ya Uber imetangaza ramsi kuanza tena kutoa huduma zake nchini Tanzania, hii ni baada ya kusitisha huduma zake mapema Aprili mwaka uliopita.

Meneja wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Imran Manji, anasema “Tuna furaha kubwa sana kurudi na kuanza kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania, na tunaipongeza serikali kwa juhudi zake katika kukuza sekta ya usafiri wa kutumia teksi za mitandao.

Kipaumbele chetu ni kuwa na mfumo ambao utawasaidia madereva kutengeneza kipato cha kujikimu sambamba na kutoa usafiri wa uhakika wa kutegemewa kwa Watanzania.”

Kampuni ya Uber imerudisha huduma za UberX na Uber XL ambazo wasafiri wanaweza kutumia katika Jiji la Dar es Salaam. UberX, ni huduma ya bei nafuu ambayo inawawezesha watu wengi kufurahia huduma za usafiri wa uhakika kwenye mfumo wa Uber.

Huduma za UberXL ni kwa ajili ya wasaifiri sita na magari yanayotoa huduma hii yana nafasi inayotoa usafiri wa starehe na huduma hii inafaa kwa safari za familia au marafiki au msafiri anaposafiri akiwa na mizigo mingi.

IMG-20230118-WA0027.jpg


Balozi wa Kampuni ya Uber Idriss Sultan akiteta jambo


Uongozi wa Kampuni ya Uber ukiongea na wanahabari

Sekta ya usafiri wa teksi za mitandao imeleta mageuzi makubwa katika namna watu wanavyosafiri katika miji yetu, na tangu mwaka 2016 Uber ilipoanza kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam, kampuni ya Uber imekuwa mshirika muhimu katika jiji hili kwa kutoa usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa, kuchangia katika fursa za kiuchumi, kuwapa madereva uhuru wa kufanya kazi kwa muda wanaotaka sambamba na ulipaji kodi.

Uber imeweka msukumo mkubwa kwenye usalama, na kadri watu wanvyoendelea kutumia teksi za mtandaoni, ndivyo Uber itaendeleakuwekeza kwenye usalama. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, abiria wengi hawana uelewa wa vipengele vya usalama ambavyo wanaweza kutumia wanapokuwa safarini.

Hivyo basi, Uber imeanzisha kampeni ya kuhamasisha kuhusu usalama, maarufu kama Safety Check-up nchini Tanzania ambayo inalenga kuhimiza wasafiri nchini Tanzania kukamilisha wasifu wao wa usalama kwa kuwasha na kutumia vipengele vya usalama vinavyopatikana kwenye mfumo wetu kama vile Watu Unaowaamini, Uthibitishaji wa PIN na kukagua taarifa za gari na dereva yaani RideCheck.

Imran amehitimisha kwa kusema, “Bila shaka tuna matarajio makubwa kuhusu kesho ya soko la Tanzania. Tuko tayari kushirikiana na watunga sera, kuimarisha usalama, kusaidia madereva kukuza biashara yao, sambamba na kuboresha huduma za usafiri kwa abiria wanaotumia mfumo wetu.”
 
Back
Top Bottom