Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya usifumbie macho udhalilishaji huu dhidi ya viongozi waandamizi wa nchi yetu.

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Kitendo cha kusema Rais wa nchi amelala na mwanamke nje ya ndoa yake pasipo kuwa na "concrete evidence" hayo ni matusi mazito sana kwa yeye mwenyewe, familia yake pamoja na taifa kubwa la Tanzania. Hii ni nini kama sio "Cyberbullying"?

Nimesikitishwa sana na kitendo cha magazeti mengi maarufu nchini Kenya kuokota habari ya isiyo na udhibitisho inayomuhusu mkuu wa nchi yetu (Hata kama ni Hayati kwa sasa) kutoka katika mitandao ya kijamii kisha kuichapisha kwenye "main stream media".

aswedfcvgtr.jpg


Just imagine leo kuwe na tetesi kuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Msanii wa Bongo Movie kisha gazeti lenye ushawishi hapa Tanzania kama vile Mwananchi au The Guardian wakaichapisha habari hiyo, hivi italeta picha gani katika familia yake hata jamii ya Wakenya kwa ujumla?

Rais ni raia number moja katika taifa lolote hapa duniani na anapaswa kupewa heshima yake "to the fullest" na sio wa kuandikwa andikwa kwa habari chafu za tetesi kwenye media pasipo kuwa na taarifa kamili.
==========
fgtfgbhgt.jpg

==========
John Magufuli alikuwa ni Rais, baba pamoja na mume aliye mtiifu kwa wanawe, mkewe pamoja na Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, na kamwe asingweza kufanya kitendo kama hiki cha kuidhalilisha ndoa yake pamoja na taifa letu.

Mimi ninashauri ubalozi wa Tanzania nchini Kenya ufikishe masikitiko yake katika mamlaka husika (probably ni foreign service Department) ili mambo kama haya yasije kujirudia tena siku za mbeleni kwa Rais wa sasa Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan.

Tunachotaka sisi ni kuwa nchi jirani na marafiki zijue tuna msimamo mkali sana linapokuja suala la kulinda taswira njema ya taifa pamoja na viongozi wetu waandamizi. Leo kadhalilishwa hayati Magufuli, kesho wataanza na Rais mama Samia.

Kama ni kweli tunahitaji kuwa na umoja wa Afrika ya Mashariki ambao ni imara na wenye tija kwa pande zote, ni lazima Kenya ituhakikishie kuwa itapambana na wahalifu watakaokuwa wanafanya cyberbullying dhidi ya viongozi waandamizi wa Tanzania.

Nilazima Wakenya wajue Tanzania ni taifa kubwa kwa Afrika Mashariki na Kati. Sisi tuliwakomboa Waganda jambo ambalo wao Wakenya liliwashinda. Tunataka urafiki wenye tija and not the otherway round.

==========

Friday, March 19, 2021 – Hours after the sudden death of Tanzanian President John Pombe Magufuli, reports emerged on social media that a female Kenyan lawyer had an affair with Magufuli and that the two had a child together.

However, the lawyer has since denounced the viral social media post bearing her image, suggesting that she was in bed with Magufuli.

In a statement yesterday, the female Kenyan lawyer, who identified herself as Angela Gitahi, noted that her image had been used with malicious intent.

The post alleged that she had a child with the late president, and was looking for assistance to access Tanzania’s Embassy.

Gitahi, who is a KANU National Executive Committee Member, dismissed the claims as baseless.

“Today, I have been made aware of a social media post circulating with my image and captioned in what I would call an ‘outrageous’ misrepresentation of my person.”

“It is truly unfortunate, unnecessary, and outrageous slander by a careless propaganda outlet.”

“I find it necessary, therefore, for both my sake and those that look up to me, to share my side of the story,” she stated.

She noted that she was unbowed by the inaccurate reports.

“When someone is cruel or acts like a bully, you don’t stoop to their level.”

“No, our motto is, ‘When they go low, we go high,” she stated.
=======
Sources;
=======
(1) Did the late Tanzania President JOHN POMBE MAGUFULI ‘sleep’ with this Kikuyu lady and sired a child with her? Alleged baby mama speaks

(2) Kenyan Lawyer Reported as Magufuli's Baby Mama Issues Statement | Nairobi Times

(3) Kenyan Lawyer Alleged to be Magufuli's 'Secret Wife' Speaks | Frontliner

(4) DRAMA AS MAGUFULI’S BABY MAMA SPEAKS OUT AFTER HIS DEATH. - Challyh News

(5) Kenyan Lawyer Reported as Magufuli's Baby Mama Issues Statement

(6) Kenyan lady speaks about a report on her relationship with the late President Magufuli

(7) See Photos Of Magufuli's Alleged Kenyan Baby Mama - Kenyan Music

(8) See Photos Of Magufuli's Alleged Kenyan Baby Mama - Kenyan Lyrics
==========
aqasde.jpg

==========
T.C.R.A fungieni hii website ya kipuuzi inayochafua taswira njema ya viongozi wetu. Ni wangapi miongoni mwenu mnakumbuka lile sakata la "Ze Utamu" wakati wa uongozi wa Mzee Kikwete?
Ze Utamu>>> Search results for query: ze utamu

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mauzo ya ilo gazeti yameshuka mno kutokana na janga Covid-19,sasa kwa sababu Magufuli ni maarufu wanatumia jina lake kupata mauzo kwa habari za uongo na uzushi,kama wazushi wengine wa hapa Bongo walivyozusha kuchotwa mabilioni BOT ya kumtibu mwendazake.
 
1. Mambo ya kidiplomasia hususan kwa nchi rafiki huwa hayafanywi kwenye vyombo vya habari, inawezekana ubalozi umeshafikisha malalamiko kwenye sehemu husika na wameshayazungumza.

2. Kumbuka Kenya wana moja ya katiba bora duniani ina mapungufu yake lakini ni katiba nzuri sana. Kenya vyombo vya habari vinalindwa na katiba na vina uhuru sana, waziri wa habari hawezi akaamka tu asubuhi akafungia chombo cha habari. Kuna tume ya vyombo vya habari ambayo haihusiani na serikali ambayo yenyewe ndio ina shughulikia mambo ya kinidhamu kwenye media.

So usifikiri ubalozi unaweza ukalalamika kwenye serikali ya kenya na serikali ikakifungia chombo cha habari.
 
hii kawaida bana, acha stress
haujawahi kusingiziwa ushatembea na msichana fulani mtaani? kazini? kanisani? n.k

utapata stress

Ki afrika kama ni kweli...basi sifa kwa Marehemu, alikuwa na nguvu huku anaumwa moyo??
 
2. Kumbuka kenya wana moja ya katiba bora duniani..ina mapungufu yake lakini ni katiba nzuri sana. Kenya vyombo vya habari vinalindwa na katiba na vina uhuru sana..waziri wa habari hawezi akaamka tu asubuhi akafungia chombo cha habari.
Mkuu, masuala ya sheria za Kenya na udhalilishaji wa viongozi wetu hauna uhusiano kabisa. Ni lazima tuwe wakali linapokuwa suala zima la kulinda heshima yetu kama taifa. This is nonsense.
 
inawezekana ubalozi umeshafikisha malalamiko kwenye sehemu husika na wameshayazungumza.
Kwanini unaongelea uwezekano? Ina maana hauna uhakika? Kuna proof gani kama ubalozi umefanya hivyo? This is against our common EAC values. Rais sio msanii wa bongo movie wa kufanyiwa dhihaka.
 
Back
Top Bottom