Kuna demu nilimuonaga siku moja cafeteria akanivutia kinoma, kajaaliwa kunako maeneo, maji ya kunde flani hv, mzuri kwel kwel. Basi bahati nzuri jamaa yangu mmoja pale alikua anajua ni nani. Nikafanya harakati za mtu mweusi nikapataga namba yake, lakini hakunipa yeye.
Basi kumuendea hewani nilipigwa hyo interview, we nani? wa wapi? unashida gani? n.k mimi nilienda direct to the point. Sasa kumbe sijui siku hyo alichanganya mafile, maana nilijitambulisha na nini lakini akawa anahisi mimi ni dogo gani cjui alimsumbua sumbua mchana. Basi nikaishia kujibiwa tu "katafute 1st year wenzako". Nikasema sio kesi stress za UE hizi.
Baadae sana miezi na miezi nimeshamaliza chuo nikaja kumchek tena, this time mambo yakawaga fresh, hata alivyokuwa anajibu ilikua tofauti. Akajaga kuniambia kuna siku alikua anapitia pitia text zake za kwenye archive. Alivyosoma ile convo akawa anaona mbona huyu alikua direct haleti longo longo sana, sema ndo hvo wanawake asijifeel cheap hawezi kukutafuta.
Tulidate kama miez miwili tu kila mtu akaendelea na ishu zake.