Hi Wakuu
Ninasikitika sana,jamii hii ya JF,kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nafasi zao kubishabisha,na kukashfu hoja za msingi na mifano halisi ya ubaguzi wachache tuliyobahatika kuushudia ktk jamii yetu ya kitz.
Kipande nilichowapa ni ukweli niliushuhudia mimi mwenyewe,na si hadithi ya kuleta uchonganishi hapa JF.
Ni vigumu sana,kwetu sisi watz kutoa ushahidi wa kukamilisha hoja ya kibaguzi,nimejitahidi kuwaaelezeni ukweli hasa,wa ubaguzi niliouona kwa macho yangu,lakini kuna watu fulani,kwa kulinda maslahi ya wahusika,wanatuita wachonganishi,si jambo jema.Ni hatari sana kwa jamii kama yetu,kukosa haja ya kuhoji ukweli kwa hoja na kuibishia tuuu,ilihali hata ukibisha hakuna atakayekuhoji.
Hapa twapaswa kupiga vita wanaobagua wenzao,na si kupinga waleta mada.
Members,hoja na vipande vyote nilivyoleta hapa ni vya kweli,labda nilulize mnataka nithibitishe vp?waliyafanya haya nawajua kwa majina na sura zao,na bado wapo hai,na wana nafsi zao,sasa nifanye nini?au nanyi hamnitakii mema?Niwawezeshe vp sasa?