Tanzania imewasaliti Waislamu !

Status
Not open for further replies.

The Fixer

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
1,365
583
Ndugu zangu wana JF
Ndugu zang Watanzania woote !

Assalaama aleykum....!

Nayaandika maneno haya nikiwa na majonzi makubwa sana katika nafsi yangu na hata kwa jamaa zangu Waislamu wa Tanzania majonzi haya nayaona kila siku tunapokutana na kuzungumza mambo mbalimbali katika hali ya ana kwa ana na hata kwenye mitandao ya kijamii kama huu..

Leo naandika kwa kichwa cha habari " Tanzania imewasaliti Waislamu ". Serikali ya Tanzania leo yenye kila aina ya neema ambayo waliipigania kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya kupigania Uhuru, walitoa fursa zao zoote na michango yao ya hali na mali kwa ajili ya neema ya Tanzania hii , imewasaliti !

Mwaka 1954, Mwl Nyerere akifundisha Pugu sekondari alitembelewa na Bw Joseph Kasela Bantu baada ya kushauriana na Wazee wa Dar es salaam kuwa hapa yupo Mwanachama wa TAA kutoka Tabora ambaye inawezekana hajui kama hata huku harakati zimepamba moto ili amfahamishe kuwa Wazee wa Dar es Salaam nao wameamka kifikra na walikuwa wameanzisha chama chao cha harakati za kupigania uhuru kilichoitwa TANU pale makao makuu " New Street " Lumumba, Mwl Nyerere alipotaka Tabora kule aliacha chama cha TAA wakati huo akifundisha Saint Marry - Tabora na chama hicho kikiongozwa na akina MZEE MAULID KIVURUGA, HAMIS NYANYAA na MZEE CHAMANG'ANDA USINGIZI

Bw Joseph kasela Bantu alimuomba Mwl Nyerere aungane nao katika harakati na ndipo alipofika huko Lumumba aliwakuta akina MZEE MSHUME KIATE, JUMBE TAMBAZA, AIDARI MWINYIMVUA na SULEIMAN TAKADIRI. Mkristo Mkatoliki kutoka Butiama akaalikwa na kupewa ushirikiano na fikra chanya na Wazee wale, Akiwa na kaptura yake ! Kwa Wazee wale kuwa na kaptura mbele yao na mbele ya jamii ni sawa na uko uchi ! Mzee Aidari Mwinyimvua akampima Suruali na Mzee Mshume Kiate akalipia Suruali zile tatu ( 3 ) Kijana kutoka Butiama akaungana rasmi na wazee wale katika harakati zile za kupigania Uhuru na Bw Mshume Kiate akampatia Mwl Nyerere nyumba na akaanza kumlipa mshahara !

Akiwa Tabora katika harakati za Uhuru, Mwl Nyerere alitumia nyumba ya AMINA BINTI CHANDE, BW RAMADHANI SINGO - Bodyguard, JAFFARI IDDI - Mpishi, JAFFARI KASONGO - shushushuu wake akitangulia kuandaa mzaingira, Gari aliyotumia ilikuwa ya BILAL REHANI WAIKERA kila mahali ambako atafanya harakati zao na hao woote waliapishwa msikitini kuwa kwa HAKI YA MUNGU hawatamdhuru kabisa Mwl Nyerere, hao nnao kutajia woote walikuwa ni Waislamu isipokuwa wachache sanaaaaa JOHN RUPIA na VEDASTOS KYARUZI. Akiwa Dar es salaam katika kitovu cha harakati za kudai Uhuru Mwl Nyerere alitumia Gari ya Marehemu DOSSA AZIZI

• Tanzania imewasaliti Waislamu •
Mwl Nyerere akiwa Lindi katika harakati za TANU na kudai kwao uhuru kwa kuwaamsha Watanzania. Alikwenda pia na kufungua tawi jipya la TANU na hamadiii....ikafika jumapili na Wazee wanafahamu kuwa Mwanaharakati wao sio Muislamu ikabidi wamuandalie mazingira ya kumsindikiza na kumrudisha alipofikia ofisi ya TANU baada ya sala yake hiyo siku moja ya jumapili. Wakatafutwa vijana YUSUFU CHEMBELE na RASHID SALUM MPUNGA kama ma- bodyguard, wale vijana ikabidi wamuulize sheikh wao kwamba Mzee tukifika na kanisani tubaki nje ama tuingie naye kanisani ? Mzee wao akawaagiza waingie naye ndani kanisani na watoke naye baada ya misa na kumrudisha walikomtoa. Askofu / Padri wa siku ile alishangaa kumuona kijana anaingia na walinzi wa Kiislamu nyuma yake ndani ya kanzu na bakrashea zao hawacheki na mtu. Dhamana yao ilikuwa ni kumlinda hadi kanisa kwa wenzake Wakristo wale waliokuwa very concerned na Usalamaa wake na walikuwa ni Waislamu, Baada ya Uhuru mwaka 1964 Bw Yusuf Chembele na Rashid Salum Mpunga , Mwl Nyerere aliwatia KIZUIZINI mwaka mmoja na miezi 9

•Tanzania imewasaliti Waislamu •
Leo hii miaka 39 iliyopita baada ya kuanzishwa kwa NECTA na kufanya kazi zake kulingana na kanuni na sheria zake , lakini Wakristo waliamua kwa maksudi kupitia Baraza la maaskofu kulihujumu Baraza na kuwafanya Waislamu kuwa ni watu tu wa kusoma Madrasaa na hawana akili za elimu hii ya upande mwingine.... Marehemu PROF KIGOMA ALI MALIMA aliliona hilo na kuanzisha mfumo wa namba katika kutahiniwa / mitihani na kusahihisha mitihani lakini linapokuja swala la nani apate daraja gani na apelekwe shule gani kwa masomo ya juu basi kuna KAMATI YA KUTUNUKU ambayo hukaa na kuamua nani aende mbele na nani abaki nyuma na kukosa elimu kabisa, Waislamu kuwa asilimia chache katika taasisi za elimu ya juu sio bahati mbaya ni " mipango " ya Serikali ya Tanzania wakishirikiana na Kanisa kuwahujumu Waislamu !

Waislamu wa Tanzania wanalipa kodi na kuna Waislamu ( wafanyabiashara ) wakubwa wa 5 ni walipaji kodi wakubwa sanaa na kati ya hao wa 5 ni 4 tu ambao hufanya biashara ya chakula. Baada ya kulipa kodi serikali huchukua fedha hizo na kuwapa Wakristo kupitia mkataba wao wa MEMORANDUM OF UNDERSTANDING ( MOU ) ulioandikwa na Prof MAHALU akiwa UDSM, Waislamu huo mkataba wameuona na wanao. Kwanini Waislamu walipe kodi zao kwa serikali na Serikali ichukue hela hizo na kwenda kutunisha shughuli za kibiashara za Makanisa ie ( hospitali, shule ? )Huduma hizo hata baada ya kupunguziwa / kuondolewa kodi katika taasisi hizo bado huduma hizo sio za BEI NAFUU kabisa . Ugomvi hapa wa JK na Makanisa ulianzia hapo katika kuondoa Mabilioni hayo katika MFUMO KRISTO, Bunge lilipewa mswada huo na kulazimishwa kuondolewa baada ya Kanisa kuchachamaa na kuonekana Amani itatoweka so soon, Waislamu hawana ugomvi na Wakristo ila kuna watu wachache sana wanaotumia vichwa vyao kufugia nywele tu ili kuwachonganisha ndani ya jamii hii ! Kwanini serikali ya Tanzania inawafanyia hivi Waislamu ?

• Tanzania imewasaliti Waislamu•
Mwl Nyerere anasimulia miaka ile baada ya kustaafu kuwa Mzee Dossa Azizi alikuja nyumbani kwangu, nyumba anayosema ni ya Mshume Kiate kuwa Wazee wanamuita na alipelekwa kwa Mzee Jumbe Tambaza, Mwl Nyerere aliwakuta wazee wa Kiislamu na kwa kauli yake mwenyewe walimsomea Duah , Yeye Mwl alisema kuwa walikuwa wanasoma Quran . Mzee Dossa Azizi alikuja nyumbani kwangu usiku - anasimulia Mwl Nyerere na akamwambia MZEE RAMIA anakuita Bagamoyo, Akampitia na gari asubuhi na kumpeleka Bagamoyo baada ya kufungishwa Swaumu kwa siku kadhaa walichimba shimo kubwa na kumchinjia Mbuzi humo na Mwl Nyerere akaambiwa kuruka damu hiyo ! Mzee akasema Mwingireza amekwishaaa....

• Tanzania imewasaliti Waislamu.
Leo Tanzania Waislamu hata muda wa kufanya ibada zao ama ile siku ya Ijumaa hawapewi ruhusa kufanya ibada na wala sio siku ya mapumziko kama ilivyokuwa kwa wenzao Wakristo wao wanatakiwa kufanya kazi tu !

Sensa ya mwaka huu iliangukia siku ya sikukuu ya Idd na zipo taarifa kuwa Waislam walikuwa kwenye Semina ya usimamizi walizuiliwa kufanya ibada siku ya Idd kwakuwa tu ratiba ya Sensa imewekwa na ifuatwee hii si haki hata kidogo yaani pamoja na mchango wao woote bado thamani yao ni ndogo sana na wala hawaheshimiwi na kupewa fursa yao ya kufanya ibadaa zao, Mzee Dossa Azizi alikufa mlandege akiwa miguu peke hana hata kandambili ( Dossa alikufa maskini wa kutupwa ) baada ya mali na fursa zake zoote kuwekeza katika kuikomboa Tanzania lakini Tanzania ikamsaliti na wala hakuna shaka kama wajukuu zake leo wamekosa hata fursa ya kusoma Sekondari kwasababu ya kubaguliwa na MFUMO KRISTO !

Quran inachomwa Mwanza na mchomaji anaonekana hana hatia na wale Waislamu waliosimama kutetea kitabu chao kisichomwe waliambulia mabomu ya machozi na vipigo, kesho yake Mchomaji anasindikizwa kama shujaa kurudi kwa mkewe ! Maisha ya Waislamu leo Tanzania ni ya ajabu sanaa kwa kielelezo kuwa wao wanaishia / wanatumia muda wao woote kwenda madrassa na sio shule !

Waislamu wa Tanzani wanataka haki yao kama walivyo binadamu wengine na pia Serikali ikome mara moja kuwapatia Wakristo kodi za Waislamu kufanyia biashara zao, hakuna mahala popoote duniani ambako Kanisa linastawi sambamba na jamii husika.. Hii ni zaidi ya THEOLOJIA YA UKOMBOZI !

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndo walivo hawa jamaa,ukiwakuta kwenye vijiwe vya kahawa sasa,kama hawaongelei simba na yanga,basi wanawaponda wakristo..
Baada ya kuona maisha magumu na elimu hawana,wameanza kutoa cd kuhusu freemason,bas ukiziangalia utacheka pumba wanazoongea..
Kimsingi mwalimu ka-pay tribute kubwa sana kwa waislam,Mfano likitokea jambo lolOte kitaifa basi Rais anawaita wazee wa Daressalaam(ambao wote ni waislam) na kuongea nao,mbna kwa hilo sisi hatupig kelele.!

"Upumbavu n kipaji,kuna watu wanazaliwa nacho"..Mwl:Nyerere...
 
Ndugu zangu wana JF
Ndugu zang Watanzania woote !

Assalaama aleykum....!

Nayaandika maneno haya nikiwa na majonzi makubwa sana katika nafsi yangu na hata kwa jamaa zangu Waislamu wa Tanzania majonzi haya nayaona kila siku tunapokutana na kuzungumza mambo mbalimbali katika hali ya ana kwa ana na hata kwenye mitandao ya kijamii kama huu..

1. Kwanza huelewi unachokisema
2. Pili, labda unieleweshe hapa maana ya Qur'an ni nini: ni kitabu (karatasi na maandishi) au ni ujumbe (neno liloandikwa kwenye kitabu, linaweza kufundishwa bila kuandikwa au linaweza kurekodiwa kwa namna tofauti na kuandikwa).
3. Hoja zako zote zina harufi ya udini tunaopambana nao kwa sasa.
4. Tatizo ni wewe mwenyewe na si mwingine.
5. Jifunze vizuri dini yako na uishi vizuri na Watanzania wenzako na saidia kupiga vita udini usiuendekeze.
 
Ngano za Mohamed Said hizi zinawamaliza vijana wa kiislamu..

Kwa kukusaidia ww The Fixer nenda kule kwenye thread ya "uchochezi wa mohamed said" Yericko Nyerere utakuta nondo nzito zilizochambuliwa na kina Nguruvi3 Jasusi n:k hakika watakutoa ktk wingu zito lililotanda kichwani mwako

Mungu akubariki
 
Last edited by a moderator:
Kazi ipo!!! jamani fanyeni kazi muache kulia lia kama watoto wadogo. Ongezeni bidii kwenye Elimu bila kujali dini mtatoka kwenye dibwi la ufukara wa akili
 
You want to rewrite the History of this country. Sad to inform you that you are not the first and certainly not the last. Just be curious to know what has been the fate of your friends' unproven theses!
 
Mtoa mada umeniudhi sana. Huu sio wakati wa kuongelea habari za dini, tunaongelea utaifa wetu na masuala ya msingi ya maendeleo yetu!Tupa kule udini bwana!!!!!
 
Mi ni Mwislaam. Lakini waislaam wenzangu tunakolekea naona tunakosea sana. Kila mahubiri tunaongelea san habari za wakristo hatupati hata muda wa kukumbuka hata hadithi za Mtume SAW na maswahiba wake. Hatuhubiri tena quraan na baadala yake tunawajaza waumini wetu chuki na maneno ya kuuwa, Itqafu na mahubiri yasiyo kuwa na ilimu akhera. Tujirudi wakuu. Huu io waqti wake..,
 
Nimesoma kwa uangalifu sijaona mambo yafuatayo anayodai mlalamikaji:
1. Huo mSWADA wa kufuta RUZUKU kwa kanisa uliletwa na nani na lini bungeni, . Huo mswada unaitwaje?
2. Usaliti uko eneo gani haswa kwani kama ni vyeo vya kitaifa, kimikoa na Wilaya dini zote zipo. Usaliti upo wapi?
3. Hospitali na za kikristo zimejengwa na wamissionari kwa kushirikiana na wakristo wa kwanza mlitaka mgawiwe vitu visivyo wahusu?

Hivi ninyi wale waarabu walioeneza Uislamu kwanini hawakujenga Mashule na Mahospitali na badala yake kujenga misikiti na ngome za kuhifadhia watumwa?

Baada ya kugundua hamkuwa na elimu ya kupambana na mkoloni mkamwomba nyerere mlitaka mgawiwe vyeo kama pipi hata kama mtu hajui kusoma?

Kama mlikuwa na shida mbona hamkumweleza Mwinyi alipokuwa rais ili awapatie haki mnayohitaji. Si alikuwa Mwislamu au hakuona madai yenu. JK naye si mwislamu, Makamu wa rais naye si mwislamu, Jaji Mkuu na kiongozi nao si waislamu, IGP naye si Mwislamu? mlitaka nini?

Acha upumbavu na uchochezi hapa si mahali pa kutoa hoja zisizo na mashiko au ulitaka Kardinali Pengo naye awe mwislamu, na Askofu Malasusa naye awe mwislamu?
 
Mkuu rushanju umenifilisi hoja.Ijumaa iliyopita nilikuwa mitaa ya Bondeni napata chakula cha mchana wakati naendelea na zoezi la kupambana na njaa namsikia Sheickh kupitia vipaza sauti ana bwabwaja.

Kaanza Ndugu zangu Waislam tumeonewa sana,tumepuuzwa sana,tunanyanyaswa katika nchi yetu tuliyoipigania uhuru.Hawa jamaa zetu wanachota fedha za kodi kupita MoU,Wamejazana katika maofisi ya serekali kote huko ni wao hakuna waislam,NECTA inafelisha watoto wa kiislamu sasa wametuingilia wanataka wachinje wao.......

Serekali hii dhalimu sana najisogeza niusikie huo udhalimu Sheickh anarejea tena NECTA inafelisha watoto wa Kiislam.Bunge linawanyanyasa waislamu Mtu mzima anasema bila aibu Rais wetu ni mdini kwakuwa ni muislam.....blah blah.....


Najiuliza ikiwa serekali ni dhalimu mbona kiongozi wake akisemwa unaumia ?....Muda wote wa mawaidha sheickh kajikita kuwalaumu wakristo na serekali hakuna mawaidha hakuna hadithi za mtume SAW hakuna.

Namaliza chakula nabaki nikiiwaza Tanzania ya kesho itakuwaje.


Mi ni Mwislaam. Lakini waislaam wenzangu tunakolekea naona tunakosea sana. Kila mahubiri tunaongelea san habari za wakristo hatupati hata muda wa kukumbuka hata hadithi za Mtume SAW na maswahiba wake. Hatuhubiri tena quraan na baadala yake tunawajaza waumini wetu chuki na maneno ya kuuwa, Itqafu na mahubiri yasiyo kuwa na ilimu akhera. Tujirudi wakuu. Huu io waqti wake..,
 
acha kulilia kama demu wewe, taasisi za umma milango haifungwi vyuo na mashule hayana milango muda wowote waweza ingia nakupata huduma. kama ulichelewa kama inavyoonyesha, peleka wanao, wajukuu na wa himiza hilimu dunia misikitini badala ya chuki

kuna kitu umeandika kimenishangaza, matambiko aliyofanyiwa Mwalimu yana uhusiano gani na uislam???, matambiko kama hayo ni nguvu za kishetani, dunia inaongozwa na sayansi katika kila nyanja, waambie waislamu wenzio waachane na imani na ibaada za kishetani kwani haziwezi kushinda (Sayansi)+(Shule)=(Ukristo)

mwisho waambie waislamu waache uvivu kama wa kwako kusubiri serikalii iwapelekee maendeleo kwenye jiwe vya ghahawa, jishughulishe mbona wapemba(waislamu) wanajishughulisha huku mitaani na wanafanikiwa bana???
 
Tanzania imewasaliti Waislamu.
Leo Tanzania Waislamu hata muda wa kufanya ibada zao ama ile siku ya Ijumaa hawapewi ruhusa kufanya ibada na wala sio siku ya mapumziko kama ilivyokuwa kwa wenzao Wakristo wao wanatakiwa kufanya kazi tu !

Sensa ya mwaka huu iliangukia siku ya sikukuu ya Idd na zipo taarifa kuwa Waislam walikuwa kwenye Semina ya usimamizi walizuiliwa kufanya ibada siku ya Idd kwakuwa tu ratiba ya Sensa imewekwa na ifuatwee hii si haki hata kidogo yaani pamoja na mchango wao woote bado thamani yao ni ndogo sana na wala hawaheshimiwi na kupewa fursa yao ya kufanya ibadaa zao, Mzee Dossa Azizi alikufa mlandege akiwa miguu peke hana hata kandambili ( Dossa alikufa maskini wa kutupwa ) baada ya mali na fursa zake zoote kuwekeza katika kuikomboa Tanzania lakini Tanzania ikamsaliti na wala hakuna shaka kama wajukuu zake leo wamekosa hata fursa ya kusoma Sekondari kwasababu ya kubaguliwa na MFUMO KRISTO !

Quran inachomwa Mwanza na mchomaji anaonekana hana hatia na wale Waislamu waliosimama kutetea kitabu chao kisichomwe waliambulia mabomu ya machozi na vipigo, kesho yake Mchomaji anasindikizwa kama shujaa kurudi kwa mkewe ! Maisha ya Waislamu leo Tanzania ni ya ajabu sanaa kwa kielelezo kuwa wao wanaishia / wanatumia muda wao woote kwenda madrassa na sio shule !

Waislamu wa Tanzani wanataka haki yao kama walivyo binadamu wengine na pia Serikali ikome mara moja kuwapatia Wakristo kodi za Waislamu kufanyia biashara zao, hakuna mahala popoote duniani ambako Kanisa linastawi sambamba na jamii husika.. Hii ni zaidi ya THEOLOJIA YA UKOMBOZI !

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ulichokisema, nakoment kama ifuatavyo...
1. Kwa mtazamo wako, Tanzania iliyowasaliti waislamu, wanaishi watu gani?
2. Waislamu si sehemu ya Tanzania? Kama ndiyo, nao wamejisaliti wenyewe?

NB
You can't strengthen the weak by weakening the stronger!!! Hii ina maana ya kwamba

You cannot help small men by tearing down big men.
You cannot help the poor by destroying the rich.
You cannot lift the wage earner by pulling down the wage payer.
You cannot help men permanently by doing for them what they could and should do for themselves.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom