Ubaguzi uliotia fora.

huko marekani watu wanataka wasikilizwe, lakini hakuna pahala walipodai kwanini hawajapewa uwaziri!

ingelikuwa watu wanataka kuripua makanisa huko zanzibar, wangelianza na yale makanisa makuu yaliyopo.

kuna habari kuwa kanisa la minara miwili (catholic) zanzibar, wakiristo waliolifungua (wazungu) walipewa mkataba wa land wa miaka 99, miaka hiyo imeisha na hakuna hata sehemu moja serikali ya zanzibar iliposema kuwa italipokonya kanisa hili na kurudisha ardhi hiyo kwa watu wake. (ambao wanao waraka wa ardhi yao)

kwa hiyo kabla ya kukaa watu wakasema serikali ya zanzibar inaupendeleo kwa waislam, watafute facts kwanza........na wasikurupuke tu
 
Heshima mbele, Mkuu! Kaa kwanza na wakristo wa huko halafu uje utuambie kuwa hakuna malalamiko.

Huko marekani, unadhani kwa nini wanamshangilia Obama? Kukubalika kwa mtu mweusi katika jamii kutahitamishwa hapo atakapochaguliwa rais kutoka jamii hiyo. Kama vile ilivyokuwa kwa wakatoliki na Kennedy. Kama vile kwetu alipochaguliwa Al Haj Mwinyi palivyoonyesha kuwa sis wote tuna haki sawa na hakuna sehemu iliyotengwa kwa ajili ya dini moja!

Vitisho vya kulipua makanisa yalishawahi kufanywa na si la kubishia. sasa kama walikuwa wanatingisha kiberiti hilo ndilo jamii ya huko inatakiwa kuliangalia. Kama nakumbuka vizuri, serikali ilitoa tamko la kulani na kusisitiza kuwa yeyote atakayethubutu atachukuliwa hatua kali! Ndivyo inavyotakiwa.

Tatizo si kwenye makanisa yaliyopo. Serikali ya Zanziba hata siku moja haijajitangaza kuwa ni serikali ya kiislamu kwa hiyo kutokupokonya makanisa hayo si fadhila bali ni wajibu wao!

Kama nilivyosema mwanzo, hatuangalii idadi ya watu bali kila aliye raia wa nchi hiyo ana haki sawa na mwenzake za kusikilizwa na mahitaji yake kutimizwa pale yanapowezekana na si kumtolea nje kama mnavyotaka kumfanyia huyu mwenzenu. Kutimiziwa matakwa yake si fadhila ni wajibu wa serikali yeyote makini.
 
Watz woote,sifurahishwi na hali hii hata kidogo,natoa wito kwenu wakristo woote,munaomwogopa MUNGU na mlio tayari kumtetea MUNGU wenu,hali hii ikiendelea na ikitokea hakua representatives wa wakristo ktk serikali ijayo zenj,nasi tuanze kuwabagua waislamu woote huku bara,ktk nyanja zooote,na hakuna kumpigia kura mgombea yeyote muislamu.Kwa ufupi tutampa kura zetu mgombea yeyote yule mkristo tuu,hata urais tutampa mkristo tuuuuu,hadi kileweke,Mtikila hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Ni lazima niseme kuwa hii sikubaliani nayo hata kidogo! Mawazo kama haya ndiyo bila shaka ambayo yamewafanya wengine kumuita Mukombosi bigot! Kwenye hili walikuwa na haki kabisa.

Lakini bado ninaamini kuwa hizi ni symptoms tu za ugonjwa wenyewe. Tunachotakiwa kufanya ni kuachana na upuuzi huu na kuangalia kiini cha kilio chake!
 
Kuhani Mkuu na wenzako mnatia aibu
Fungeni midomo yenu kwanza kwa kurishabikia ri element la kibaguzi.
Wangelikuwa waislamu wachache wako zenj hawapewi nafasi wangeandama hadi UN(mfano mzuri ni wapemba wamechoshwa na kutopewa nafasi),wakristo wakihoji,oooohhh wanaleta ubaguzi.
Ninyi ni wabaguzi tena wa kutupwa,nawaambieni wakristo wooote hapa JF wanawacheki mnavyojikanyaga kuukwepa ukweli.
Mungu atujahalie uzima,Chama Cha Kutetea Maslahi ya Wakristo kitasimamisha mgombea wake wa uraisi na wabunge then mtauona moto.Na ahakika tutashinda,hakutakuwa na mafisadi huko wala matatizo tena,waislamu itakuwa zamu yenu kuongozwa hadi mwisho wa dunia.
Acheni ubaguzi wa kishenzi la sivyo nyamazeni kimya.

Kutokana na maandishi yako nadhani wewe ndio Mbaguzi Mkubwa na mbaye hufai kabisa katika jamii ya Kitanzania. Maneno yako ni sumu ya hali ya juu na sidhani watu kama wewe wanafaa kuchangia chochote kwenye jamii kwani ulichoandika ni pumba tupu zilizochanganywa na hisia za kibaguzi kama za Ku Klux Klan, what a waste.
 
Ceeque
Nasikitika kwa kutojua mukombosi ni mtu gani.
Usitie hofu,ni waziri wako ajaye.
Atakubagueni vilivyo.
Hahahahahhaahahhaahahahahahh
 
Sio Wakristo wote wana religious bigotry kama unayo ionyesha hapo. Na nani amekwambia kwamba huko Bara kuna clear Christian majority, (or Islamic, for that matter)?

And you better be faking that foreign twang, because if you really are an alien then I question your motives. Watu wanajaribu kujenga madaraja na kuziba nyufa zinazo weza kuligawa Taifa, wewe una introduce uninformed demagoguery hapa.

Big bigot, shut your face!

Usimbeze ana HAKI ya kusema na kutoa maoni ila tu havunji sheria...mwache anene kwani katiba inamruhusu atoe maoni yake..lakini na wewe unapaswa kujibu kwa hoja na si kumbeza.
 
Usimbeze ana HAKI ya kusema na kutoa maoni ila tu havunji sheria...mwache anene kwani katiba inamruhusu atoe maoni yake..lakini na wewe unapaswa kujibu kwa hoja na si kumbeza.

Yeye ni bigot na inabidi aungue hell kwa kuleta chuki za kidini hapa. Do you have problems with that?
 
kwanza asilimia ya wakiristo zanzibar ni ngapi? haifiki hata 5! na naming a few kwa kumbukumbu zangu za siasa za tanzania nawakumbuka wakristo hawa waliowahi kushika nyazifa za juu visiwani.

Isack Sepetu
bregedia jenerali Mwakanjuki

isitoshe, kusikia jina mtu anaitwa Mrisho, au Amani, kusikutishe ukafikiria hao watu wanahusiana vyovyote na uislam, pengine wamekuwa waislam kimazingira tu, lakini hawafati wala hawanufaiki na dini hiyo au nyengine

Mkuu sasa hapo unakosea...sasa unamaana kama wapo wachache hawana haki ya kushika nyadhifa na kuwaongoza waislam huku Zenj???hapo watu wanadai usawa kama wanavyo dai hapo Pemba wanadai usawa kama Unguja...
 
Kuhani Mkuu na wenzako mnatia aibu
Fungeni midomo yenu kwanza kwa kurishabikia ri element la kibaguzi.
Wangelikuwa waislamu wachache wako zenj hawapewi nafasi wangeandama hadi UN(mfano mzuri ni wapemba wamechoshwa na kutopewa nafasi),wakristo wakihoji,oooohhh wanaleta ubaguzi.
Ninyi ni wabaguzi tena wa kutupwa,nawaambieni wakristo wooote hapa JF wanawacheki mnavyojikanyaga kuukwepa ukweli.
Mungu atujahalie uzima,Chama Cha Kutetea Maslahi ya Wakristo kitasimamisha mgombea wake wa uraisi na wabunge then mtauona moto.Na ahakika tutashinda,hakutakuwa na mafisadi huko wala matatizo tena,waislamu itakuwa zamu yenu kuongozwa hadi mwisho wa dunia.
Acheni ubaguzi wa kishenzi la sivyo nyamazeni kimya.

Mukombosi,

Hizi attitude za wapi muzee? Umetokea Rwanda-Urundi au wapi?

Kwanza kabisa, unaposema

Wangelikuwa waislamu wachache wako zenj hawapewi nafasi wangeandama hadi UN

Kwanza una assume, halafu pili unakuwa huelewi principle ya "two wrongs do not make a right" halafu zaidi ya hapo unashindwa kung'amua kuwa kusema watu wasipewe kazi kwa misingi ya walikotoka hakusigishani na kusema kuwa watu wa eneo moja wasiwabague watu wa eneo lingine katika kupata kazi kwa misingi ya geographical origin.

Kwa maneno mengine, ni vibaya kwa Wapemba kukoseshwa kazi serikalini Zanzibar kwa sababu wao ni Wapemba kama ilivyo vibaya kwa Wapemba kutaka kupata kazi serikalini kwa sababu tu wao ni Wapemba.

Tunachotaka kuona ni kuwa watu wapate kazi kwa mujibu wa elimu na uzoefu bila kujali dini wala kabila.

Tuonyeshe Mkristo aliyekoseshwa kazi kwa sababu ya dini yake then tutakuwa na issue ya kuongelea, otherwise itakuwa ubishi usio kichwa wala mguu.

Unajua Zanzibar kuna Wakristo asilimia ngapi? Kisha katika hao walio na sifa na nia za kufanya kazi serikalini ni asilimia ngapi?

Halafu unamshambulia Kuhani Mkuu na wenzake kama wote ni waislamu wanaokupinga kwa sababu unatetea wakristo, kwa kweli hili linaonyesha kukosa kina kwa mawazo yako, unajuaje kwamba Kuhani Mkuu si Mkristo?
 
Kitu alichokosea Mheshimiwa Mukombosi ni gia aliyotumia kuingiza hoja yake! Aliingia katika mtego kwa kufanya kile anachowatuhumu wenzake kumfanyia. Ninavyoelewa ni kuwa kweli jumuia ya kikristu Zanziba wanajisikia kuwa second class citizens katika nchi ambayo in everything but name inajitambua kuwa ya kiislamu. Kwa vile wao kama raia wa nchi hiyo wana haki ya kusikilizwa na wale walio wengi. Uchache wao ndiyo unaleta uzito zaidi kwenye suala hili. Nchini Marekani kupitia gerrymandering, (kabla haijawa abused;tazama-http://en.wikipedia.org/wiki/Gerrymandering) mipaka ya majimbo ilikuwa inarekebishwa ili kuhakikisha kuwa wale ambao ni minorities wanapata uwakili katika bunge la jimbo. Badala ya kuteua token figures inabidi serikali ifanye jitihada kuwa hao walio wachache wanapata nafasi ya kupata watakaowakilisha matakwa yao. Na hii si kwa wakristu peke yao bali wengine kama wangazija, wahindi n.k. Kwa bahati mbaya hatuna hulka ya kumthamini yule tunayemuona ni mnyonge katika jamii yetu. Waunguja hawaoni sababu ya kukaa meza moja na wapemba. Na sisi wakristu wa bara kwa muda mrefu tulifumbia macho malalamiko ya wenzetu waislamu. Tu wepesi wakutoa majibu ya mkato badala ya kuangalia kwa undani namna gani tunaweza kurekebisha hali. Ndio maana pamoja na kuwa napinga kwa nguvu zangu zote maneno aliyoyatumia Mukombosi maana yanachangia katika kuongeza chuki naelewa anakotokea. Ni kama vile wazungu wamarekani walivyostushwa na kauli za Rev. Wright na kumuona ni mbaguzi wakati weusi walielewa machungu yake yanatokea wapi!
 
Fundi,

Hili swala linazidishwa utata na elements nyingi kama vile

1.Zanzibar si nchi as such (kwa maana ya nchi yenye raia na kutoa passport zake) bali ni a state within a state. Kwa hiyo swali linakuja hawa watu wanaobaguliwa ni Wazanzibari Wakristo,watu wa bara wanaokaa Zanzibar au wakristo wote tu?

2.Pili tunaongelea kazi gani? Kazi katika hoteli za kitalii , kazi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au kazi zote tu? Kama ni kazi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar naomba nielimishwe Watu wa Bara wanaweza kufanya (nakumbuka Brigedia Adam Mwakanjuki alikuwepo SMZ kama sijakosea,hapa napo walikuwa wabaguzi? Kwani Mwakanjuki ni Mkristo na mtu wa bara)

Kama hatujapata statistics za Zanzibar kuna wakristo wangapi, wangapi wako eligible na wangapi wamefanyiwa mizengwe (au kitu concrete cha kutupa muelekeo huo) tutakuwa tunacheza Makida
 
1. Naam, Pundit!Inaelewaka kuwa Zanziba si nchi kamili in the sense of sovereinghty, lakini ina serikali yake na rais wake na kwa hiyo katika nyanja fulani inatamblika kama nchi. Wakristu wanaozungumziwa wanatoka katika vikundi vyote ulivyovitaja. Tatizo ninaloona mimi ni kwa kuzingatia majority (zaidi ya asilimia 90) Zanziba imekuwa ni de facto taifa la kiislamu. Kwa hili tu, inamfanya yule asiye muislamu kujiona hana nafasi katika jamii. Ni rahisi sana kwa mahitaji yake kutiliwa maanani.

2.Kwenye kazi nadhani wanazungumzia representation katika corridors of power. Naamini kabisa kuna glass ceiling Zanziba kwa minorities kama ilivyo katika nchi nyingi duniani. Kazi sehemu nyingi zinatokana na networks popote pale. Mkiwa wachache ni vigumu kujipenyeza katika hizo networks. Yamewakumba wanawake, watu weusi ulaya n.k. Na ndiyo maana wenzetu kwa kutambua hili wakaweka namna ya kuwawezesha wale wanaotoka katika minorities kuweza kupenya. Watu kama wakina Mwakanjuki ni kama vile sisi tulivyowaweka wakina Dr. Stirling, Jamal, Shamim Khan na yule mwingine niliyemsahau. Kuweko kwao hakujaondoa distust ya wengi wetu ambao tunadhani nchi ile ni ya wenye rangi kama yetu.

3. Si rahisi kupata takwimu katika mazingira ya kwetu. Ni vizuri kusikiliza anecdotal evidence kutoka kwa hao wanaoishi huko. Badala ya kuwatolea nje, wale walio wengi inabidi wafanye juhudi za ziada ku'reach out' kwa walio wachache na kuwahakikishia kuwa wana haki sawa kama wengine. Si lazima wapewe uwaziri ili mradi wajue kuwa wanasikilizwa na kuthaminiwa!
 
Wanangu!!

Amani iwe nanyi!!!!!

Naombeni sana msicheze ngoma ya maadui. Ipo gharama gani kama tukikosoana na kunyooshana kimitizamo na uadilifu katika utawala. Sioni kama ni busara kuwatangazia waisilamu kutengwa bara kama njia ya kutatua tatizo la wakristo kutengwa Visiwani.

Nainukuu Biblia pale isomekapo: Mpende Adui yako. Waombeeni wanaowaudhi, Watendeeni watu kama jinsi ninyi wenyewe mgependa mfanyiwe. Msilipe ovu kwa ovu. Haya maneno yalisemwa na Yesu Kristo Mwokozi wetu, kwa nyakati tofauti. Na huu ndiyo ukristo.

Lakini najua jinsi ajisikiavyo mtu anayehisi kutengwa, kunyanyapaliwa na kubaguliwa. Poleni sana. Ila sidhani kama hii ni njia sahihi hata kidogo
Moyoni mwangu ninajiridhisha kuwa yapo mambo hayawezi kuondolewa kwa hatua yoyote ya majukwaani, mahakamani, mitaani, kwanye media nk. bali ni MAOMBI tu!!! Hili jambo naona mahali pake haswa ni kwenye POWER HOUSE.
Likishapita kwenye power house linakuwa jepeeeesi kama bua la mpunga vile.

and more........
 
Mbona mnamaka kiasi hicho? Mukombosi amewastua kuwa kuna malalamiko katika jamii ya kikristo Zanziba. Anawastua kuwa kuna wengi Zanziba zaidi ya wapemba na waunguja (wakristo, wangazija n.k) na wote wana haki ya kutambuliwa. Ni kama vile sisi wa bara tunavyodhani kuwa Tanzania ni ya watu weusi tukisahau wahindi, wazungu na wengineo.

Bigots ni sisi tunaokataa kuwaona walio wachache katika jamii yetu! Ni haya ambayo yanawafanya waunguja na wapemba wasiweze kukaa na kumaliza tofauti baina yao. Tusiwe kama mbuni na kujifanya hatuoni matatizo yalio mbele yetu.

..fundi,

..iyo issue kaileta kiubaguzi!
 
..fundi,

..iyo issue kaileta kiubaguzi!

Mkuu DAR si LAMU!
Nilirudi kumsoma vizuri na ikabidi na mimi nijiunge na wale wengine waliomshupalia! Gia aliyoingia nayo ni ya hatari na ina sumu mbaya ya ubaguzi! Hii haikubaliki hata kidogo.Kwa hali hiyo sina budi kuwaomba radhi wale wote walioona, kwa haki kabisa, kuwa nimewashambulia bila sababu. Samahanini sana.

Lakini bado naamini suala la msingi alilolileta linastahili kujadiliwa kwa makini.
 
Hahahahahahahahhhh
Mwafrika wa kike,na nnaoniombea niende hell,nawaomebeeni muzidi kuomba mufanikiwe,ok?

Database wape kile kipande kilichobaki,kutoka dodoma.
 
Beat_Dead_Horse-1.jpg
 
Wana JF naona mnamshambulia mukombosi kama mpira wa kona.
Siamini kama kuna kiumbe amabacho bado hakiamini kuwa wazenj + baadhi ya waislamu ni wabaguzi.
Kuleni basi kijipande cha muhogo dume hapo chini:

"Tukiwa ndani ya chaguzi moja maarufu hapa tanganyika(dodoma),kati ya wagombea wote,wagombea wawili tuu(mmoja muislamu na mwingine mkristo) walikuwa tishio(kupata ushindi) pale ukumbini,wakati kampeni za mwisho mwisho zinawadia pale ukumbini,mgombea mmoja kati ya wale wawili(muislamu) aliona ngoma inakuwa nzito ikabidi aanze kucheza rafu,mtu mzima huyu bila aibu aliwaaendea wale wapiga kura toka zenj na kuwanong'oneza na kusema ..............MUSIMUPE HUYU MPINZANI WANGU KURA NI KAFIR .............."
Yule mugombea mukristo alipewa hizi habari ndani ya sekunde zilezile,lakini,alijikaza kiume.

Kufumba na kufumbua kura zikapigwa,matokeo yakatoka,MUBAGUZI wa kidini akashinda kwa kishindo cha ubaguzi.

Naomba mufahamu kuwa habari hizi ni za kweli,hakuna unafiki hapa,
Kwa wanaobisha juu ya ubaguzi huu,wamugeukie MUNGU wao,la hasha waendeleee,ikiwa MUNGU wao anaruhusu elements za kibaguzi.
Timu yetu haitachoka kupigania haki za wakristo,kupigana zidi ya wabaguzi hawa,Eee MWENYEZI MUNGU utujahalie,amen.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom