Ubaguzi regency hospital nimeona sijasimuliwa-ukiwa na bima hapafai

MKITO

Member
Oct 8, 2010
52
7
Ukiwa na bima hapa ni shida nimeitwa kuingia kwa daktari akaja mgonjwa nyuma yangu na fail mhudumu kamruhusu mie kaniacha pale aliponiita awali
 
Na wewe uliachaje mtu kakukuta afu anaingia tu?....

piga ngumi, kichwa na kitu chochote chenye ncha kali! Nchi tabu hii.
 
Mimi pamoja na familia yangu hupata huduma ya tiba hospitali hiyo hiyo na sijawahi kushuhudia aina yoyote ile ya ubaguzi.
Mke wangu alipata stroke na tukapewa namba na daktari wa kumuona . Tulikuta wangonjwa wengine wakingojea zamu zao kuingia lakini alipokuja daktari alitaka kwanza kumuona mgonjwa wangu. Kutokana na experience hiyo basi inawezekana kulikuwa na wagonjwa ambao aidha walikuwa wako more serious au pengine undugunasation ambao wengi huutumia kupata huduma hasa zile ambazo kuna rafiki ndugu iwe benki na hata polisi.
 
Kuna issue za appointment pia, isije ikawa yeye aliweka appointment kabla hajafika. Mimi nimewahi kutibiwa hapo sio chini ya mara tatu, na sikuwahi kukumbwa na adha hiyo.

Ila waswahili wanasema uoga wako ndio umaskini wako, siku nyingine mkuu uliza kwa utaratibu tu....au hata waweza muambia nesi kuwa nimetangulia kabla, si ingekuwa nafasi yangu kumuona daktari? Labda ungepewa majibu ambayo yangepelekea wewe kuondoka bila duku duku moyoni.
 
Mimi pamoja na familia yangu hupata huduma ya tiba hospitali hiyo hiyo na sijawahi kushuhudia aina yoyote ile ya ubaguzi.
Mke wangu alipata stroke na tukapewa namba na daktari wa kumuona . Tulikuta wangonjwa wengine wakingojea zamu zao kuingia lakini alipokuja daktari alitaka kwanza kumuona mgonjwa wangu. Kutokana na experience hiyo basi inawezekana kulikuwa na wagonjwa ambao aidha walikuwa wako more serious au pengine undugunasation ambao wengi huutumia kupata huduma hasa zile ambazo kuna rafiki ndugu iwe benki na hata polisi.

asante mkuu kwa maelezo mazuri ila yule nes na mgonjwa aliyekuja nyuma yangu kwa mazungumzo tu wanafahamiana ..maana daktari alisema anaona mgonjwa wa mwisho kabla ya kuenda raundi arejee badae lakini mhhh !! doctor akamwambia nes naona mmmoja wa mwisho nesi akamwambia bado mmoja ndio mimi sasa huyo baada ya yule mwenza wa nes kuingizwa kinyemela..doktari akajibu mie natoka muone we mwenyewe...
 
Tumekuelewa ila nauliza wewe ma mgonjwa wako mnatumia bima ya NHIF?
NHIF ni shida kila hospital ukienda unaangaliwa kama kinyaa vile hawakupi huduma hata.
Mie nimeshaenda karibu zoteee hospital kweli ni tatizo bima za NHIF wakati mwingine yanipasa kutumia cash ndo wanahangaika sasa.Ukienda Hindu Mandal ndo utalia na kibima chako.
 
Mkuu ni kadi yangu tukufu ya NHIF
 
Huwa natibiwa regency hosp sijaona kabisa ubaguzi,
ni wewe tu kadri ulivyowahi na foleni yako ikoje,

Penye ukweli usemwe ukweli na kwenye bahati mbaya
kama ya kwako ijulikane tu ni bahati mbaya.

Pole sana.
 
Mimi nimetibiwa ktk hospitali nyingi hapa DSM, lakini ubaguzi ulioko Regency ni wakutisha na sio dhidi ya wenye kadi za NHIF bali ubaguzi wa watu wenye asili ya Asia dhidi ya waswahili.Walinifanyia ubaguzi hadi wao wenyewe wakaona aibu na ikabidi DKT. mmoja kijana mwenye asili ya Asia aniombe samahani kwa kitendo hicho.
 
Kusema kweli natibiwa hapo regency inapokuja swali unamuona dr nani jibu la kwanza huwa nawaambia nataka daktari mswahili.
 
Pole sana baba koku
kwa hiyo naweza kusema nina bahati,
kwa kweli sijawahi kuona shida kwenye hosp yeyote hata tz
toka najifungua watoto wangu wote wanne tena kwenye hosp
za kawaida kuanzia mawenzi hosp, kcmc, na meta hosp huko mbeya,
sijawahi hata siku moja kuona dalili ya kukosewa; i thank God for that.

Poleni sana wote mliokwisha kuumizwa na hosp zetu.

Mimi nimetibiwa ktk hospitali nyingi hapa DSM, lakini ubaguzi ulioko Regency ni wakutisha na sio dhidi ya wenye kadi za NHIF bali ubaguzi wa watu wenye asili ya Asia dhidi ya waswahili.Walinifanyia ubaguzi hadi wao wenyewe wakaona aibu na ikabidi DKT. mmoja kijana mwenye asili ya Asia aniombe samahani kwa kitendo hicho.
 
Last edited by a moderator:
Mimi pamoja na familia yangu hupata huduma ya tiba hospitali hiyo hiyo na sijawahi kushuhudia aina yoyote ile ya ubaguzi.
Mke wangu alipata stroke na tukapewa namba na daktari wa kumuona . Tulikuta wangonjwa wengine wakingojea zamu zao kuingia lakini alipokuja daktari alitaka kwanza kumuona mgonjwa wangu. Kutokana na experience hiyo basi inawezekana kulikuwa na wagonjwa ambao aidha walikuwa wako more serious au pengine undugunasation ambao wengi huutumia kupata huduma hasa zile ambazo kuna rafiki ndugu iwe benki na hata polisi.

Ulikuwa na bima au ulikuwa na cash mwenzio alikuwa na bima ndo kabaguliwa
 
Mimi nimetibiwa ktk hospitali nyingi hapa DSM, lakini ubaguzi ulioko Regency ni wakutisha na sio dhidi ya wenye kadi za NHIF bali ubaguzi wa watu wenye asili ya Asia dhidi ya waswahili.Walinifanyia ubaguzi hadi wao wenyewe wakaona aibu na ikabidi DKT. mmoja kijana mwenye asili ya Asia aniombe samahani kwa kitendo hicho.
Ubaguzi ya rangi ni kikwazo kikubwa sana kwa maendelo na ustawi wa waafrika, Ulaya wanbaguliwa, Asia hivyohivyo, basi hata kwetu Afrika pia!!!
 
Ulikuwa na bima au ulikuwa na cash mwenzio alikuwa na bima ndo kabaguliwa
NINA BIMA YA NHIF
Tena kwa taarifa yako pale pale hospitali pana jamaa wenyewe wa NHIF hivyo kama unamatatizo next time waulizie tuu ndugu yangu.
 
Mimi nimetibiwa ktk hospitali nyingi hapa DSM, lakini ubaguzi ulioko Regency ni wakutisha na sio dhidi ya wenye kadi za NHIF bali ubaguzi wa watu wenye asili ya Asia dhidi ya waswahili.Walinifanyia ubaguzi hadi wao wenyewe wakaona aibu na ikabidi DKT. mmoja kijana mwenye asili ya Asia aniombe samahani kwa kitendo hicho.

wewe nakubaliana nawe hata kama una kadi ya matibabu ya aina gani haijalishi ukiwa mswahili , akija muhindi tu unaona anakaa kidogo anaingizwa na nesi ni mara chache sana kukuta muhindi anasubiri katika foleni. hili hata mie nimeshuhudia.
 
Kusema kweli natibiwa hapo regency inapokuja swali unamuona dr nani jibu la kwanza huwa nawaambia nataka daktari mswahili .

...bilashaka hii mbinu inafaa! Dawa ya ubaguzi ni ubaguzi...
Wote mtakao kwenda kutibiwa hapo Regency Hospital tumia njia hiyo... "NATAKA DKT MSWAHILI"
 
...bilashaka hii mbinu inafaa! Dawa ya ubaguzi ni ubaguzi...
Wote mtakao kwenda kutibiwa hapo regency hospital tumia njia hiyo... "nataka dkt mswahili"

mie nimekaa nikaona bora hospitali kubwa zishinikizwe kutumia mfumo kama wa crdb ya makumbusho....ukifika unachukua namba ya digiti na kuingia kwa daktari iwe ni mashine ya umeme isome namba YAKO, hapo tutakomesha ubaguzi
 
Back
Top Bottom