Hivi kikawaida sijui hapa tuchukue hatua gani dhidi ya huyu mchungaji...

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,889
15,934
Ni mchungaji ndio. Wa haya makanisa ya kilokole haya ya akina Tayana-wog . Kiukwel nimesikitishwa na kushikwa na hasira kwa wakati mmoja.

Ni mama yangu mkubwa kabisaa yamemtokea.
Ni kwel sikatai hakulazimishwa kwenda huko kusali lakini ndio hivyo tena mambo ya imani (magumu sana).
Jana wakiwa katika vipindi cha maombi , mchungaji anapita anapiga maombi huku waumini nao wanagonga prayers ki individual kukemea shetani.

Mchungaji akawa anaweka mikono kwa watu tofauti tofaut randomly.
Akafika kwa aunt anamuwekea mikono huku anakemea pepo (tulivyoambiwa na wahusika) sasa ile kuona muumini yuko stable haanguki ,inaonekana akatumia nguvu kama kumpushi (hii hata mimi naijua, nilishawahi kukutana nayo, pastor akiona huanguki anakupush backward, hata sijui logic yake huwa nini?).

Sasa kwakua aunt ni mtu mzima (sana) akakoshindwa kustahimili msukumo akaona kama anataka kuanguka. Sasa haraka haraka akawa anatafuta pozi ili akae kwenye kiti (cha plastic) kilicho nyuma yake, akakosea timing..TATIZO LIKATOKEA.

Akaanguka kwa kutulia makalio ila ndio habar ikaishia hapo , akawa hawez kuamka. Kumbe inaonekana alifikia kiupande akakalia/akaangukia nyonga. MAUMIVU SI YA KITOTO.

Aunt alishapata shida kama hii miaka mi 3 nyuma akiwa nyumba akijikwaa akavunjika nyonga barabarani. Na ni mimi ndiye nilimchukua nikiwa na mwanaye wa kike (mdogo angu) tukamkimbiza Regency Medical Centre. Pale kwakua kuna watu najuana nao, nikashauriwa baada ya vipimo kwamba mgonjwa wetu apelekwe Muhimbili kwakua pale ghatama zitakua nafuu maana kwa Regency ,operation ile ingetugharimu milion 20 kwakua ni private. Ma hata kama ana bima, ingeweza ku cover not more than 9 millions.

Na kwel, tukapewa rufaa Muhimbili, shukrani sana sana sana kwa mtaalamu wa mifupa pale Moi, dokta *****. Japo tulilazimika pia kumuhonga ila kupata huduma ila tunashukuru Mungu pale Muhimbili ilitugharimu million 10.

Hiz pesa tulikamuana wana ndugu ili kufanikisha hili zoezi kwakua aunt ana watoto wadogo bado hawana uwezo kiuchumi.
HAYA SASA MCHUNGAJI KALIZUA TENA.
Na maza amasema kabisaa anahis hali kama ile ya miaka ileee ila sasa ni mguu mwingine. Ameanza vipimo vya awali leo na kama wana ndugu tumekaa mkao wa kula matumbo joto kujua donei kias gani itahitajika na JANUARY yoote hii.

Kwakwel binafsi makosa majibu, huyu mchungaji tumfanye kitu gani?? Maana kikawaida hatuna namna ya kumtia hatian kwa mujibu wa sheria.

am sorry kwa uzi mrefu.

Nimemaliza
 
ingekua mimi ningemfata huyo mchungaji atajua yeye kama atamponya atamubea au atampeleka hospital vinginevyo mchungaji a jiandae kutrend
Shida ndio hapo sasa mnajikita huwez kumuacha mgonjwa aendelee kupata shida kisa tu kumuandama huyu mchunga kondoo
 
SI Wewe TU mwenye maumivu,,,,yupo mwingine humu jf, yeye anauza maembe mjini anamtumia Hela Maza kijijini,nae anzipeleka Kwa mchungaji.
20231111_000713.jpg
 
😂😂😂😂😂😂😂 mkuu nimecheka kama mazuri hizi imani bhn kuna mwengine aliikuwa anachukua akiba pesa yeye na mumewe anapeleka kwa mwamposa sasa hivi anatafuta mchawi wa ndoa yake
Very very insane mindsets. Sina maana ya kukashifu dini maana hata mimi nasala haya makanisa ila nina mipaka na ukomo kwenye mambo mbali mbali.
Kuna hayuabsiwez vuka wala siwez ruhusu mchungaji avuke
 
Pole sana Mkuu.
Mimi ni mkristo ila mambo ya kuombewaombewa hasa kuwekewa mikono kizembezembe na watu wasioeleweka sipendi kabisa.

Watu wenyewe hawaeleweki asipokuangusha ukaumia, anawezakukuachia maroho ya ajabu ajabu.

Mambo ni Bluetooth, untouch kabisa. No hands over my head.
 
Back
Top Bottom