Uandishi ni talanta ninayoihusudu sana

Melon Micky

Member
Sep 13, 2020
25
73
Uandishi ni talanta ninayoihusudu sana. Kwa maana hiyo napenda pia kusoma.
Kila siku huwa naamini ya kuwa kwa kusoma sana makala, ngano na riwaya zinazoandikwa na baadhi ya waandishi nguli labda naweza kupanua fikra zangu ili nami niweze japo kuandika! Lakini wapi bwana...
Hili suala ni gumu kwangu!

Waandishi hupata maudhui kila siku na hata kwa vyanzo vidogo tu ambavyo kwa jicho la kawaida huwezi ona lkn wao huvumbua maudhui na kuandika kitu ambacho kinaweza kukusisimua.
Wanabuni na kutunga visa ambavyo ukivisoma vinakujengea uhalisia wa kitu halisi.
Lakini mimi naishi katika jamii hizo hizo ila sioni cha kuandika. Hata visa vyepesi vya kufikirika kwangu hiviji. Na hapa ndipo thamani yao kwangu inapozidi kuwa kubwa!
Kongole waandishi....
 
Na Kweli huwezi kabisa

Hujui vina vinakaa wapi, mshangao hutambui kbs,, sasa hata paragraph ndo balaaaa yaani kusoma nimepata ukakasi.

Nkuulize tu secondary ulikuwa combination gani?
 
Na Kweli huwezi kabisa

Hujui vina vinakaa wapi, mshangao hutambui kbs,, sasa hata paragraph ndo balaaaa yaani kusoma nimepata ukakasi.

Nkuulize tu secondary ulikuwa combination gani?
Wewe sio mwalimu mzuri hivyo hata nikijibu swali lako haitanisaidia.

Hata hivyo nikushukuru kwa uwezo wako mkubwa wa kushauri ambao unatokana na miaka uliyokaa darasani.
Tofauti ya kusoma na kuelimika iko wazi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom