SoC01 Uandaaji wa mazingira tamanishi na uboreshaji wa Sekta ya Elimu kwa tija ya maendeleo ya taifa katika sekta zote

Stories of Change - 2021 Competition

Elimu story

New Member
Sep 9, 2021
2
2
Habari wanaJF na wasomaji wote wa andiko hili.
Hongereni na pilikapilika za ujenzi wa taifa.

Utangulizi.

Kumekuwa na misemo mingi sana ambayo imekuwa ikielezea maana na umuhimu wa elimu kwa mtu mmoja mmoja, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Misemo kama: elimu ni ufunguo wa maisha, elimu ni bahari, elimu ni mwangaza na elimu ni chanzo cha hekima. Huku vitabu vitakatifu vikitukumbusha pia madhara ya kukosa elimu, tukirejea ule usemi maarufu usemao 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'. Hii yote ni kuonyesha kuwa elimu ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu ili kupata maendeleo yake binafsi na taifa lake.

Hivyo ni wazi kuwa msingi bora wa maendeleo unategemea kuwa na elimu bora inayotolewa katika nchi ili kuwajenga Wananchi wake katika maarifa na weledi wa ufanyaji kazi wenye tija kwa maendeleo. Jambo ambalo limekuwa wazi hata zaidi kuona umuhimu wa elimu bora ni tunapolinganisha na kutofautisha nchi za dunia ya kwanza (nchi zilizoendelea) na nchi za dunia ya tatu (nchi zinazoendelea) ambapo tunaona kuwa nchi zilizoendelea zina misingi bora ya elimu ambayo inazalisha wasomi wengi wenye ujuzi na ubunifu wakubuni na kuunda vitu vipya.

Na hii inathibitishwa na orodha ya vyuo bora mwaka huu ambapo vyuo hamsini bora duniani zinatoka katika nchini ambazo zimeendea. kiunganishi (link) hii World University Rankings 2021-22 | Global 2000 List | CWUR inaonyesha orodha ya vyuo 2000 bora duniani huku Tanzania ni chuo kimoja tu kipo kwenye orodha hiyo ambacho kimeshika nafasi ya 1872 ambacho ni Muhimbili University of Health and Allied Sciences ndo chuo namba moja kwa ubora Tanzania. (chanzo cha habari ni Center for World University Rankings)

Ninamaanisha nini kupitia utangilizi nilioandika hapo juu? Acha nilejee kichwa cha habari cha Andiko hili 'UANDAAJI WA MAZINGIRA TAMANISHI NA UBORESHAJI WA SEKTA YA ELIMU KWA TIJA YA MAENDELEO YA TAIFA KATIKA SEKTA ZOTE' . Namaanisha yakuwa ukuaji wa sekta zote za maendeleo zinategemea ubora wa elimu itolewayo katika nchi. Sekta kama ya kilimo, uvuvi, ufugaji, michezo, biashara, utalii, ujenzi, madini, afya na uwekezaji ilizisonge mbele kwa tija ya maendeleo tunahitaji kuwa na wananchi wenye elimu bora katika kila sekta ilikupata uzalishaji bora wenye tija kwa taifa.

Iko wazi kuwa tunapotembelea wakulima, wafugaji, wavuvi, na wachimba madini wadogowadogo, kwa kweli tutakubaliana kuwa wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea na wachache tu ndo wanafanya kwa weledi kama ambavyo elimu waliopata katika nyanja yao inavyowataka kufanya na hata uzalishaji wao ni mkubwa. Hatuwezi kumfananisha mkulima, mfugaji na mchimba madini mdogomdogo wa nchi hii na nchi zilizoendelea na sababu kuu ya utofauti huu ni elimu.

Wenzetu wanafanya kazi kwa maarifa na ujuzi wa hali ya juu waliyosomea wakati huo huku nchini wakulima walio wengi ambao ndo wako kijiji kwa kweli wengi wao wameishia darasa la saba japo sasa idadi kubwa inaongezeka pia yawalio maliza kidato cha nne lakini bado elimu hii ipatikanayo shule za msingi, sekondari na vyuoni bado haziwaandaai wananchi kuwa bora katika nyanja wafanyiazo kazi.

Mapendekezo/Maoni yangu juu ya 'UANDAAJI WA MAZINGIRA TAMANISHI NA UBORESHAJI WA SEKTA YA ELIMU KWA TIJA YA MAENDELEO YA TAIFA KATIKA SEKTA ZOTE'

1. Kufanyike ufuatiliaje na tathmini ya kina juu ya Sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 (Education Policy 2014) na uboreshaji wa mitaala ya elimu itakayoweza kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi na maarifa yakutosha. Sera ya elimu mwaka 2014 ambayo ndo tunayotumia kwa sasa ambayo inalenga katika kuzalisha wasomi wenye elimu ya kulifanya taifa kuwa lakujitegea badala kuwa tegemezi inapaswa kufanyiwa tathmini itakayoonyeshe wazi sehemu zilizofanikiwa na ambazo kama taifa bado hazijafanikiwa katika kutoa elimu kwa wananchi kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wangu naona wazi elimu itolewayo bado ni duni katika kufanya mwanafunzi kuwa mbunifu na mjuzi katika uzalishaji wake. Nakili kuwa kumekuwa na maboresho ya mara kwa mara kwenye mitaala. nakumbuka kabla ya mtaala tunaotumia sasa yaani unaokazia umahiri (competency based) kulikuwa na mtaalama uliokazia ujuzi (knowledge based) mtaala huu hadi ulipobadilishwa kwa kuwa ilionekana unafanya wanafunzi kukariri tu masomo wafundishwayo darasani ili wafanye mitihani na kufaulu tu, lakini wanapomaliza masomo na kurudi mtaani wanakuwa hawana ujuzi wakutosha kukabiliana na maisha.

Hivyo serikali iliamua kuja mtaala huu tutumiao sasa yaani unakazia umahiri (competency based). Lengo la mtaala huu nikuwafanya wanafunzi kuwa mahiri katika nyanja wanazofundishwa huku ujifunzaji wa vitendo ukitiliwa maana ili wahitimu wanapomaliza masomo waweze kuyaaishi kwa vitendo mambo waliyojifunza. lakini kusudi la mtaala huu bado halifanyika kwa vitendo

3. Uhamasishaji wa viongozi wa kiserikali katika ubora wa elimu usikazie ufaulu tu wa kitaaluma badala yake uangalie sekta zote. Mfano kama shule ina miradi ya ufugaji, shamba, michezo ya aina mbalimbali. Sisi sote tumekuwa tunajiona pale inapokuja suala la kutaja shule bora nchini, imekuwa ikitaja shule ambazo zimefaulisha vizuri wahitimu kwa mwaka husika. Mfano ukitaka kujua shule 10 Tanzania kwa kidato cha sita zinatangazwa tu ambazo zinaongoza kitaifa katika matokeo ya kadato cha sita, kama jedwali hapa chini linavyoonesha kulingana na NECTA na pia OR-TAMISEMI walivyotangaza shule bora kwa kidato cha sita 2021.

View attachment 1930790

4. Kuandaa mazingira tamanishi ya kupata walimu pamoja na mazingira tamanishi ya kuwaandaa walimu wawapo vyuoni. Sote tunakubaliana kuwa huwezi kujenga kitu bora ikiwa mjenzi si bora. Huwezi kupata kilicho bora ikiwa anayeandaa au kukitengeneza si bora. Namaanisha nini? Naamanisha kuwa elimu yetu inaonekana kutokuwa bora hii ikichangakiwa na mazingira duni yanayotumiwa kuwachagua wanafunzi wa kwenda chuo kusoma ualimu na pia mazingira duni wanavyoandaliwa huko vyuoni.

Iko wazi inapokuja suala la kuchagua ufaulu wa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda kusoma ualimu vyuoni mara nyingi wanachaguliwa wenye ufaulu wa chini, huku waliofaulu vizuri wanakwenda kusoma kozi kama udaktari, urubani na uhandisi. Madhara yake ni kwamba; tunapata walimu ambao hawana maarifa yakutosha zaidi. Hebu fikiria kuwa ilifikia hatua ukiwa na ufaulu wa daraja wa IV pointi 28 ( division IV 28) unachaguliwa kusoma ualimu shule ya msingi! hivyo wazi inakuwa vigumu kuzalisha wanafunzi bora kwa kwa walimu wamechaguliwa kwa mfumo usio bora hivyo elimu itakayotolewa lazima iwe ya chini tu. Walimu ndo inapaswa kuwa fani ya kwanza ya kupata wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ambapo itasaidia katika kupata walimu bora ambao watatoa elimu bora na kuzalisha watoto bora.

5. Kujenga mazingira tamanishi kwa waalimu waliopo kazini. Leo hii unapowauliza wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu hivi 'ukimaliza shule ungependa kuwa nani?' majibu ya wanafunzi wengi huwa ni kwamba ningependa kuwa daktari, mwanajeshi, rubani au mhandisi. Kwa nini wanajibu hivyo? ni kwa sababu wazazi, walezi na hata walimu wanaambia watoto wasije kuwa walimu kwa kuwa masirahi yaani mshahara ni kidogo, makazi duni, mazingira ya sehemu ya kazi yenyewe ni duni yaani ofisi za walimu, madarasa na hata vyoo.

Wakati huo wanajua madaktari, wanajeshi na hata marubani wanamaisha mazuri kwa kuwa masirahi yao ni mazuri. Hii inachangia kushusha msukumo wa walimu kuwafundisha wanafunzi kwa weledi wanafunzi. Fikiria msemo usemao "waalimu ni wito" kwamba mwalimu anapaswa kuvumilia kwa hali na mali kwa kujitoa kuwafundisha watoto kwa nguvu zote lakini ni kweli kwamba mazingira tamanishi yaani uboreshaji wa mishahara, makazi na sehemu za kazi utawafanya walimu kufundisha kwa msukumo mkubwa.

6. Kukazia masomo kufundishwa kwa vitendo zaidi kuliko nadharia na kujenga shule za ufundi nyingi zaidi kama za Mtwara Tech, Moshi Tech, Ifund Tech, Tanga Tech nk. shule za muundo huu ndo zinafaa kwa mtaala tunaotumia sasa wa kujenga umahiri. Ufundishaji wa vitendo zaidi ndo unafanya nchi nyingi duniani zinazotoa elimu bora kufanikiwa.

Ufundishaji huu ndo mzizi wakutengeneza na kuibua wanafunzi wabunifu na vipaji. Mfano leo nchi ya Cuba ndo inaongoza kwa kuwa na uwiano na mdogo zaidi wa wataalamu wa afya kutibu watu wachache. hii ni kutokana na repoti World Health Organization's Global Health Workforce Statistics, OECD, supplemented by country data. katika link hii Countries ranked by Physicians (per 1,000 people).

Cuba imetuma sehemu mbalimbali zenye uhaba wa madaktari duniani kusaidia nchi zenye uhaba na mojawapo wa nchi hizo ni kenya. Je, ndo kusema kwamba Cuba wana akili sana? Tukiangalia mfumo wetu wa Tanzania wakupata madaktari tungesema ndio Cuba wana akili sana kwa kuwa hapa Tanzania ili uwe daktari lazima uwe na ufaulu mkubwa sana. Lakini la hasha sivyo kwa Cuba. Kwao elimu ya vitendo ndo inakaziwa zaidi kuliko nadharia, na ukweli ni kuwa udaktari unahitaji mazoezi ya vitendo. hivyo elimu ikazie vitendo zaidi


Hitimisho.
Naomba nihitimishe kwa kwa tafakuri hii usemi wa kwamba "ukololoni mambo leo upo na moja njia ambayo inatumia ni kuchukua wasomi wetu na kuwapeleka nchi za kwao. pia wametuachia mifumo ya elimu ambayo itazalisha wasomi wasiweza kuwa wabunifu na wagunduzi ili tuendelee kuwa tegemezi tu"

Swali ni kuwa ikiwa tunajua hivyo na wanafunzi wetu wanafundishwa hivyo kwenye darasa la sita somo la Maarifa ya jamii na hata kidato cha nne somo la Civics kuhusu somo la ukoloni mamboleo (Neo colonialism) hivyo ni wazi jamii inajua mbinu zitumiwazo juu ya ukoloni mamboleo.

Kwa nini hatuchukua hatua? Hatua nilizoanisha hapo juu bila shaka utakubaliana nami mojawapo ya njia za kutumia kuwa wasomi na elimu bora nchini. Ni kweli wasomi wetu hawatakubali kwenda nje ikiwa wanapatiwa mazingira bora hapa nchini. Pia tutazalisha wasomi wabunifu na wagunduzi ikiwa mitaala na sera zikifuatiliwa kikamili kuhakikisha ufundishaji ni vitendo na si nadharia zaidi ambayo wanakaririshwa ili kufaulu mitihani.

Ahsanteni sana kwa kutenga nafasi ya kusoma andiko langu.
Ni mimi, Elimu Story.

1631201027648.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom