SoC04 Mambo ya kuboresha ili kukuza elimu bora na yenye tija

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
26
11
Serikali katika suala la elimu ihakikishe
  • Inatatua changamoto ya uhaba wa walimu kwa baadhi ya shule
  • Ukosefu wa vifaa vizuri vya kufundishia na kujifunzia
  • Kuongeza mashule hususani katika maeneo yenye uhaba wa shule
  • Kuandaa mitaala itakayowafanya wanafunzi kujifunza uhalisia wa changamoto zilizopo katika jamii na namna ya kuzitatua(elimu ujuzi)
  • Kuboresha mazingira na miundombinu (kama maji, umeme, madarasa, maktaba za vitabu na madawati) ya shule mbalimbali iwe yenye kuvutia kwa kujifunzia
  • Kuhakikisha adhabu zote zenye kuleta mtizamo hasi juu ya elimu kwa wanafunzi zinaondolewa, na
  • Kuhakikisha walimu wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
 
Kuhakikisha adhabu zote zenye kuleta mtizamo hasi juu ya elimu kwa wanafunzi zinaondolewa,
Kuondoa adhabu moja kwa moja la. Sema tu adhabu iendane na kosa.

Ni lazima mwanafunzi afundishwe kuwajibika kwa matendo yake iwe kwa zawadi ama kwa adhabu stahiki.

Napendekeza tu pia kuongezwe fungu la kuwapatia zawadi watoto shuleni. Hiki kipengele kinaachwa mno. Baadhi ya shule zawadi za wanafunzi zinatoka mifuko binafsi ya walimu hii sio afya.

Lakini pia wale wadau wa kutoa misaada 'charity' sio mbaya kama mkienda shule za serikali na kuwapa watoto zawadi za ufaulu au kitu chochote kuwapatia morali. Watoto wanafurahia sana zawadi.
 
Back
Top Bottom