Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Kutokuoa sio solution ila kupata mwenye mapenz ya kweli na ambaye ni mwaminifu ndio solution la cheating zinazoendela kila mara katika mapenzi.

Hao wanapatikana wapi tena siku hizi kaka?
Hujasikia Diamond alisema, "...wazuri ni wengi lakini kumpata mwenye mapenzi ya kweli ndo balaa..."

#iamaSINGLEboy
 
ha haaa, umenichekesha sana Nyamayao, hayo yapo kabisaaa.
kuna siku mtu aliandika hapa yupo kwa kitanda na mkewe, mke yupo busy na simu, basi mara ajigeuze kushoto mara kulia mume anadhani anajilaza vizuri kumbe jamaa anafwata maelekezo kwa njemba huko nje, nilicheka sana.

hahahah haki vile Kristu arudi tu, hahaha hii kali
 
si ulikapa no mwenywe, wewe utakuwa mtaalamu, unakula unafuta mdomo, hahaha,jokes aside, haya mambo yanakera sana, kuna mkaka tupo nae ofisini,ana mobile anaiachaga ofisini ni special kwa uzinifu tu, anakwambia simpi mpango wa nje no yangu halisi hata siku moja, anavyowabadili sasa, na mkewe anavyojisifia kuhusu mume wake, yaani namwangaliaga kimoyoni nasema laiti we mwanamke ungelijua usingekaa ujidai mbele za watu mume wangu hivi wala vile, mie ndio mana nikiingiaga ofisini kwa msukuma sitaki kuchekewa mara mbili, kusanifiana tu, sijui kwanini sikwendaga u sister, lol

Hapo kwenye Red, je hauoni uchungu kumuona mwanamke mwenzako anaingizwa kwenye shimo lisilo stahili aingie.
 
Hapana mdogo wangu Nyamayao, ilikuwa utani tu, na kwa hiyo nikawa na wasi wasi kwamba kangeweza kupiga simu wakati niko na Bibi kakalikoroga.....Baadaye nilimsimulia Bibi akanicheka hata akatoa sauti ya kule chini....lol!!

Usista tena wewe??

Ningesema mengi ila ngoja tumalize kwaresma......

Unadhani mapadre wanakula wapi?....Halafu kuna baadhi ya walei ambao wanajisevia...lol!!

Kuna mmoja alikaribia kunibaka wakati nimemaliza kidato cha 4!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye Red, je hauoni uchungu kumuona mwanamke mwenzako anaingizwa kwenye shimo lisilo stahili aingie.

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ungemwambia kwamba mume wakao analizungusha mtaani kama dala dala??

Babu DC!!
 
he he heee, hukawii kupata ugonjwa wa moyo.....
sasa babu ulikuwa umekumbatioa simu kwa sababu hutaki ku-miss call yake au sababu mida hiyo sasa upo na bibi unaogopa ikiwa mbali bibi anaweza aione kabla yako? maana hapo kuna utata, lol!
all in all hayo ni mateso jamani asikwambie mtu

Kumiss call tena na wewe?

Yaani hapo natamani usiku uingie mapema nizime simu...(huwa nazima simu usiku)....kwa sababu nilihisi kanaweza kupiga simu halafu kakaleta utani....Na jinsi Bibi alivyo namba mbaya....duhhhhhhhhhhhhhhh...sikuwa na hamu na dunia kabisa!!

Ndiyo maana kila siku nawasahauri wadogo zangu, kama huna ubavu wa ku-control magari basi achana na kazi ya udereva!! Babu niliamua kustaafia mie!

Babu DC!!
 
Mkuu pamoja na mambo mengine mengi, lakini pia utandawazi umechangia sana kuondoa uaminifu katika ndoa,zamani watu wanapopatwa na vishawishi inakosekana miundo mbinu ya kutimiza hizo nia ovu,kwa mfano hapakuwa na simu,facebook,jamii forum,whatsup,nimbuzz na mingine mingi ambapo kupitia ukuaji huu wa teknolojia watu wanawasiliana kirahisi sana na pengine kupelekea kufanya vitu ambavyo mara nyingine si vyema machoni pa jamii.

Hapo kale watu wachache walimiliki magari tofauti na sasa kila mtu anamiliki gari ambalo linaweza kuiba mke/mme wa mtu kirahisi,linaweza kubeba mwanafunzi etc zamani ilikuwa ni daladala tu sasa sidhani kama ni rahisi kuanzisha mada za kimapenzi na mtu mkiwa katika daladala. Ipo mifano mingi pengine itaendelea kuletwa na wachangiaji wengine
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ungemwambia kwamba mume wakao analizungusha mtaani kama dala dala??

Babu DC!!

Ningetafuta njia mbadala ya kumfanya mkewe alitambue hilo lakini sio kumtell moja kwa moja kwama mwumewe anakigawa kama biskuti.

Kwanza, ningejenga urafiki na mkewe yaani ili nitengeneze mazingira ya malewano baina yangu na mkewe.

Pili, tungekaa na kuyazungumzia maisha ya ndoa huku tukiongelea matatizo yanayowapata wanandoa huku nikiendelea kumfariji kisaikoloji kwa kmjenga kulizoea tatizo pamoja na kukubaliana nalo.

Tatu, kwa kupitia process hizo ningeweza kumuandaa vizuri na kumfanya awe amelizoea tatizo, hivyo ningechukua muda kidogo na mwisho kumweleza anayoyafanya mumewe.
 
rafiki mpango wa kando ulikuwepo tangu zamani lakini siyo lazima kila mtu awe nao....
wewe unaweza kuchagua kutokuwa na mpango wa kando. believe me utaishi kwa amani sana na itafurahia maisha yako usipokuwa na mpango wa kando. Jaribu kuacha, utakuja kunihadithia
Mpango wa kando FP ninao kwenye keyboard tu na si duniani!
 
Last edited by a moderator:
Kumiss call tena na wewe?

Yaani hapo natamani usiku uingie mapema nizime simu...(huwa nazima simu usiku)....kwa sababu nilihisi kanaweza kupiga simu halafu kakaleta utani....Na jinsi Bibi alivyo namba mbaya....duhhhhhhhhhhhhhhh...sikuwa na hamu na dunia kabisa!!

Ndiyo maana kila siku nawasahauri wadogo zangu, kama huna ubavu wa ku-control magari basi achana na kazi ya udereva!! Babu niliamua kustaafia mie!

Babu DC!!
ha haaa, yaani hapa sina mbavu babu, lol!
hiyo ndo tunataka.... angalau kujua uwepo wetu, hakuna ruhusu mtu anakulazimisha ujibu "I love you too" (as if I love you ni swali) wakati bibi yupo jirani yako.... unaishia "mimi pia", lol!
hilo la kuzima simu usiku limenishinda, naogopa kukosa simu muhimu na za utekelezaji wa haraka. kwa hiyo kwangu simu ni on 24/7, hata nikiwa kwa mkutano........
ha haaaa, nimempenda sana bibi, hakuna kuchezewa sharubu..... michezo yooote iishie nje ya geti langu, ukishaingia ndani ni wangu, lol!
 
Ningetafuta njia mbadala ya kumfanya mkewe alitambue hilo lakini sio kumtell moja kwa moja kwama mwumewe anakigawa kama biskuti.

Kwanza, ningejenga urafiki na mkewe yaani ili nitengeneze mazingira ya malewano baina yangu na mkewe.

Pili, tungekaa na kuyazungumzia maisha ya ndoa huku tukiongelea matatizo yanayowapata wanandoa huku nikiendelea kumfariji kisaikoloji kwa kmjenga kulizoea tatizo pamoja na kukubaliana nalo.

Tatu, kwa kupitia process hizo ningeweza kumuandaa vizuri na kumfanya awe amelizoea tatizo, hivyo ningechukua muda kidogo na mwisho kumweleza anayoyafanya mumewe.
babu Dark City, come this way uangalie huyu mjukuu.....
natamani sana kukuuliza "how old are you?" lakini naona siyo sahihi
 
Last edited by a moderator:
Heheheheee yan ukiwa umejidunga ndovu ukapitiwa na kausingizi kameseji kakiingia tu wife anaanza nako lol
Utashangaa umezabwa kofi ukiwa usingizini lol utakurupukaje heheheheee kakutana na ka sms kameanza na Baby.....!

Utandawazi noma mi nataka kuachana na simu!

Tumia simu ambayo mkeo hajui kutumia applications zake,kama whatsapp,wkt yeye anakomaa na sms wewe unajimwaga na whatsapp.
 
Tumia simu ambayo mkeo hajui kutumia applications zake,kama whatsapp,wkt yeye anakomaa na sms wewe unajimwaga na whatsapp.
Heheheheee yeye yuko digitali kuliko hata mimi lol
Cheza na mabinti wa dot.com aisee mapozi kibaaooooo eti wanajidai wako up-to-date duh
Dawa ni kuwa mkali tu kila mtu na simu yake hakuna mazoea
 
babu Dark City, come this way uangalie huyu mjukuu.....
natamani sana kukuuliza "how old are you?" lakini naona siyo sahihi

Unapenda mashahidi.
Kueleza ukweli siku zote huonekana ni uchochezi ila sio rahisi kumuokoa mtu bila kupata makikimikiki.
Hilo ndilo ningelifanya mimi, sidhani kama mawazo huwa yanafanana kwa kila mtu ila hutofautiana.

Hivyo sio kila uwazalo wewe nami huwaza hivyo hivyo.
Je wewe ungefanyaje maana umechukua muda mrefu kullijibu swali langu.
 
saudari mdogo wangu, siyo kama napenda mashahidi ila sidhani kama unajua uhalisia wa haya maisha. siyo kila ambaye amekaa kimya akiwa anaibiwa hajui kama anaibiwa......
katika kile kikao na wamama wangu mmoja aliniambia kuna kipindi walikuwa wanaishi na mumewe Dar, ikatokea mume alikuwa na mipango ya kando.... yule mama alijua lakini hakuwa na la kufanya, akaamua KUVUMILIA.

kuna siku moja mama mmoja akaenda kwa yule mama kumwambia kuhusu tabia ya mumewe na mipango ya kando, huyo mama alikuwa jirani yake na wana mazoea sana tu, ndo maana akajitolea kumwambia. Yule mama akapata uchungu zaidi lakini kwa vile hakuwa na jinsi akamjibu yule mama kuwa "afadhali kuna watu huko nje wananisaidia, Mume wangu ni ngangari sana kiasi kwamba nikiwa peke yangu ntakufa. kuwa na mwingine kunanisaidia apunguze vingine huko na akirudi home yanabaki ya kawaida (nimejaribu ku-dilute kidogo lakini naamini ninaeleweka)"

Ukweli ni kwamba siyo kama yule mama alikuwa anafurahia mumewe kuwa na mpango wa kando, hana la kufanya.... wewe kuniambia hakunisaidii lolote zaidi ya kuniumiza
 
Last edited by a moderator:
Uaminifu unaharibiwa na yule unayetaka kumfanyia uaminifu. Kama mtu unajitahidi unajibana na kujizuia mengi tu kwa ajili ya mwenzio, lakini ukifika home bado anakutazama kama nyanya mbichi na kukujibu utumbo hadi unajiuliza "hivi yale mambo kule nilikoyaona yanajileta yenyewe kwanini najibana". Hapo uaminifu utapatikana wapi?
 
Ningetafuta njia mbadala ya kumfanya mkewe alitambue hilo lakini sio kumtell moja kwa moja kwama mwumewe anakigawa kama biskuti.

Kwanza, ningejenga urafiki na mkewe yaani ili nitengeneze mazingira ya malewano baina yangu na mkewe.

Pili, tungekaa na kuyazungumzia maisha ya ndoa huku tukiongelea matatizo yanayowapata wanandoa huku nikiendelea kumfariji kisaikoloji kwa kmjenga kulizoea tatizo pamoja na kukubaliana nalo.

Tatu, kwa kupitia process hizo ningeweza kumuandaa vizuri na kumfanya awe amelizoea tatizo, hivyo ningechukua muda kidogo na mwisho kumweleza anayoyafanya mumewe.

Halafu akitengana na mume wake unamwoa wewe na kulea watoto wao au unamtafutia mume mwingine??

Hapa kusema kweli nimeishiwa nguvu...Kama dunia ingekuwa rahisi kiasi hicho basi hata maiti wasingeoza!!

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom