Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

babu Dark City, come this way uangalie huyu mjukuu.....
natamani sana kukuuliza "how old are you?" lakini naona siyo sahihi

Hapa nimechoka mkubwa mwenzangu....

Yaani kama kuna mtu anaweza kuwa na guts za kufanya kitendo kama hicho basi huyu anahitaji kuundiwa sayari yake mwenyewe...lol!!

Babu DC!!
 
saudari mdogo wangu, siyo kama napenda mashahidi ila sidhani kama unajua uhalisia wa haya maisha. siyo kila ambaye amekaa kimya akiwa anaibiwa hajui kama anaibiwa......
katika kile kikao na wamama wangu mmoja aliniambia kuna kipindi walikuwa wanaishi na mumewe Dar, ikatokea mume alikuwa na mipango ya kando.... yule mama alijua lakini hakuwa na la kufanya, akaamua KUVUMILIA.
kuna siku moja mama mmoja akaenda kwa yule mama kumwambia kuhusu tabia ya mumewe na mipango ya kando, huyo mama alikuwa jirani yake na wana mazoea sana tu, ndo maana akajitolea kumwambia. Yule mama akapata uchungu zaidi lakini kwa vile hakuwa na jinsi akamjibu yule mama kuwa "afadhali kuna watu huko nje wananisaidia, Mume wangu ni ngangari sana kiasi kwamba nikiwa peke yangu ntakufa. kuwa na mwingine kunanisaidia apunguze vingine huko na akirudi home yanabaki ya kawaida (nimejaribu ku-dilute kidogo lakini naamini ninaeleweka)"
ukweli ni kwamba siyo kama yule mama alikuwa anafurahia mumewe kuwa na mpango wa kando, hana la kufanya.... wewe kuniambia hakunisaidii lolote zaidi ya kuniumiza

Umeeleweka dada @FP, I like that.
 
Halafu akitengana na mume wake unamwoa wewe na kulea watoto wao au unamtafutia mume mwingine??

Hapa kusema kweli nimeishiwa nguvu...Kama dunia ingekuwa rahisi kiasi hicho basi hata maiti wasingeoza!!

Babu DC!!

Haya babu nimekosa, shika fimbo unichape au kama utaamua kunikemea jukumu ni lako.
 
Umeeleweka dada @FP, I like that.

Na hapo ndipo ujue kuwa dunia siyo duara wala mstatiri...!!

Kuna watu wanalea hadi watoto ambao siyo wao (tena wamezaliwa kwenye ndoa) lakini wana amani kwa sababu wamekubali kubeba misalaba yao hapa duniani....

Acha mchezo na ndoa kijana...

Babu DC!!
 
Haya babu nimekosa, shika fimbo unichape au kama utaamua kunikemea jukumu ni lako.

Wala sikuchapi na pia siwezi kukukemea....nikifanya hivyo nitakunyima nafasi ya kujifurahia siku utakapokuwa una-rewind movie ya maisha yako!!

Ni kama nilivyosema kwenye post moja, kwamba niliwahi kumshauri dada yangu mkubwa aachane na mume wako aliyekuwa anamtesa na kumchanganya na wanawake wengine. Nilimweleza kuwa nyumbani kwetu kulikuwa na kila kitu. Tena nilimuuliza kwamba alikuwa anakosa nini nyumbani?

Nikiyakumbuka maneno hayo niliyosema (when I was about 18yrs old) naishia kujicheka sana...lol!!

Babu DC!!
 
Hapa nimechoka mkubwa mwenzangu....

Yaani kama kuna mtu anaweza kuwa na guts za kufanya kitendo kama hicho basi huyu anahitaji kuundiwa sayari yake mwenyewe...lol!!

Babu DC!!

Akoseaye hufunzwa na sio kuwekwa sayari yake, kumtenga sio kumfundisha.

Anakuzuga tu kama "I am sorry mom" za watoto wa dotcom....

Zinaimbwa zaidi ya wimbo wa taifa..

Babu DC!!

Kama hutaweza kusamehe kwa hilo basi nawe wahitajika kuandaa moyo wako upy na kufany maandakizi mapya.
 
Anakuzuga tu kama "I am sorry mom" za watoto wa dotcom....

Zinaimbwa zaidi ya wimbo wa taifa..

Babu DC!!
ha haaaa, hapa umenichekesha sana babu...
mimi pale home nimepiga marufuku ya hiyo "I am sorry mom" kwa vitu vinavyojirudia.... wao wenyewe wanajua kwa hili sorry haikubaliki, lol!
sasa huyo mdogo wangu Erickb52 akifanya haya itakula kwake
 
Last edited by a moderator:
Hapa nimechoka mkubwa mwenzangu....

Yaani kama kuna mtu anaweza kuwa na guts za kufanya kitendo kama hicho basi huyu anahitaji kuundiwa sayari yake mwenyewe...lol!!

Babu DC!!
umeona eeh! afadhali kakubali sasa kuingia kwenye ulimwengu kihalisia
 
Hapo kwenye Red, je hauoni uchungu kumuona mwanamke mwenzako anaingizwa kwenye shimo lisilo stahili aingie.

Sasa nafanyaje ndugu yangu, nimwambie? hapo ni uchonganishi/umbea/ntasutwa, nayaweza mie hayo basi? na yeye makidai yamezidi, mara mume wangu hivi mara vile, yote ya nini, mie mara kibao tu watu wananiambiaga nishukuru nimepata mume, "mume wako wa kipekee, katulia kweli, hana makuu kaka wa watu", kimoyoni nasemaga makuu yake nayajua mie then natoa bonge la asante, hahahaha
 
saudari mdogo wangu, siyo kama napenda mashahidi ila sidhani kama unajua uhalisia wa haya maisha. siyo kila ambaye amekaa kimya akiwa anaibiwa hajui kama anaibiwa......
katika kile kikao na wamama wangu mmoja aliniambia kuna kipindi walikuwa wanaishi na mumewe Dar, ikatokea mume alikuwa na mipango ya kando.... yule mama alijua lakini hakuwa na la kufanya, akaamua KUVUMILIA.
kuna siku moja mama mmoja akaenda kwa yule mama kumwambia kuhusu tabia ya mumewe na mipango ya kando, huyo mama alikuwa jirani yake na wana mazoea sana tu, ndo maana akajitolea kumwambia. Yule mama akapata uchungu zaidi lakini kwa vile hakuwa na jinsi akamjibu yule mama kuwa "afadhali kuna watu huko nje wananisaidia, Mume wangu ni ngangari sana kiasi kwamba nikiwa peke yangu ntakufa. kuwa na mwingine kunanisaidia apunguze vingine huko na akirudi home yanabaki ya kawaida (nimejaribu ku-dilute kidogo lakini naamini ninaeleweka)"
ukweli ni kwamba siyo kama yule mama alikuwa anafurahia mumewe kuwa na mpango wa kando, hana la kufanya.... wewe kuniambia hakunisaidii lolote zaidi ya kuniumiza

Mie niliambiwa na dada yangu, najua alikuwa anaumia akimuona huko misele na huyo kiazi wake, huwa nawaambiaga mashost zangu kwamba siku mtu akilogwa aje aniambie oohh msukuma nimemuona hivi na vile, naanza nae, ntamcharaza akome kiherehere, ni ngumu kulipokea ati, kisa cha kuniumiza?
 
mie niliambiwa na dada yangu, najua alikuwa anaumia akimuona huko misele na huyo kiazi wake, huwa nawaambiaga mashost zangu kwamba siku mtu akilogwa aje aniambie oohh msukuma nimemuona hivi na vile, naanza nae, ntamcharaza akome kiherehere, ni ngumu kulipokea ati, kisa cha kuniumiza?

Leo hii Yesu angekuwepo, si ajabu angeenda saluni kupunguza sharubu, angeenda kwa Maumba kushona Tuxedo na angekua na IPAD....TIMING
 
mie niliambiwa na dada yangu, najua alikuwa anaumia akimuona huko misele na huyo kiazi wake, huwa nawaambiaga mashost zangu kwamba siku mtu akilogwa aje aniambie oohh msukuma nimemuona hivi na vile, naanza nae, ntamcharaza akome kiherehere, ni ngumu kulipokea ati, kisa cha kuniumiza?

Ha haaaa, siku hizi wala hakuna anayekuja live, utapokea tu sms au email toka kwa unknown, wewe utajua cha kufanya.

We unafikiri kwenda kumwambia muhusika ni swala dogo.... hujui hata atalichukuaje halafu wewe unajipeleka tu.
Jingine ni hili, kuna rafiki yangu alikuja kuambiwa na rafiki yake mwingine kuhusu mumewe, yule dada akaenda kumwashia moto mumewe wakagombanaaaaa mpaka wakachoka. sasa wakaamua kuliongea wakasameheana maisha yakaendelea.

Yule kaka katika mapenzi yao akambembeleza shosti amtajie informer, si akamtaja.....weweeeeee, sitaki kusema yaliyotokea hapo. mimi hata rafiki zangu nimewaambia kabisa, hata nimkute shem hapo na vipi sijui, hatalisikia toka kwangu. mimi nabaki na kazi yangu ya usuluhishi tu wakifumaniana huko
 
ha haaaa, siku hizi wala hakuna anayekuja live, utapokea tu sms au email toka kwa unknown, wewe utajua cha kufanya.
we unafikiri kwenda kumwambia muhusika ni swala dogo.... hujui hata atalichukuaje halafu wewe unajipeleka tu.
Jingine ni hili, kuna rafiki yangu alikuja kuambiwa na rafiki yake mwingine kuhusu mumewe, yule dada akaenda kumwashia moto mumewe wakagombanaaaaa mpaka wakachoka. sasa wakaamua kuliongea wakasameheana maisha yakaendelea. yule kaka katika mapenzi yao akambembeleza shosti amtajie informer, si akamtaja.....weweeeeee, sitaki kusema yaliyotokea hapo. mimi hata rafiki zangu nimewaambia kabisa, hata nimkute shem hapo na vipi sijui, hatalisikia toka kwangu. mimi nabaki na kazi yangu ya usuluhishi tu wakifumaniana huko

Hahaha siku dada aliyokuja kuniambia msukuma yupo sehemu fulani na yule kiazi wake,akaniambia basi mie nipo bar fulani ukishamaliza kuwasha moto njoo upunguze hasira, na kitakachotokea huko nijulishe chap chap, basi nikamaliza uvamizi nafika aliponiambia naanza kumwelezea na vicheko juu jinsi nilivyotimuliwa vumbi, hapo hapo akamuingilia msukuma hewani kwana anapokea sasa, akamtumia msg "mie ndio nimechora hilo deal, ulitaka kupitiliza sasa"...hahaha leo hii u best wao umekomaa zaidi na zaidi kabla ya kufumania, ama kweli fumanizi linakuza mapenzi, hahahahh.
 
hahaha siku dada aliyokuja kuniambia msukuma yupo sehemu fulani na yule kiazi wake,akaniambia basi mie nipo bar fulani ukishamaliza kuwasha moto njoo upunguze hasira, na kitakachotokea huko nijulishe chap chap, basi nikamaliza uvamizi nafika aliponiambia naanza kumwelezea na vicheko juu jinsi nilivyotimuliwa vumbi, hapo hapo akamuingilia msukuma hewani kwana anapokea sasa, akamtumia msg "mie ndio nimechora hilo deal, ulitaka kupitiliza sasa"...hahaha leo hii u best wao umekomaa zaidi na zaidi kabla ya kufumania, ama kweli fumanizi linakuza mapenzi, hahahahh.
cc. Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:

[TD="class: style6"][/TD]
Habari zenu wana jamvini.

Ni muda kitambo tangu niwasilishe mada yangu ya mwisho na kupotea kutokana na majukumu ya maisha. Hivyo nalazimika kuwasilisha jamvini mada hii ili sote tuchangie maoni na tafakari zetu kwa kina.

Inaaminika kuwa moja ya nguzo kuu za kudumu kwa Mahusiano na Ndoa tangu zama zilizopita ni "uaminifu". Na hii ni moja ya sababu za msingi kwa wazazi wetu walio wengi kuendelea kuishi pamoja hadi sasa.

Kutokana na nyakati kubadilika katika vipindi kadhaa hadi sasa,uaminifu ktk Mahusiano na Ndoa vimekuwa adimu sana tofauti na hapo awali. Hali hii haihitaji utafiti wa kina sana kulithibitisha kwani liko wazi kwa namna ambavyo migogoro ilivyokuwa sehemu ya maisha ya Mahusiano na Ndoa za nyakati hizi hususan kwa vijana.

Inawezekana "Utandawazi" ukawa umechangia kwa kiasi kikubwa sana ktk hili kutokana na namna tulivyogeuzwa majuha wa kuamini kila tunaloliona kutoka nchi za magharibi. Matokeo yake tumetekwa na jinamizi la tamaa na wakati mwingine ulimbukeni wa kuona hivyo ndivyo namna sahihi ya kuishi ili kuonekana shujaa machoni mwa jamii.

Jambo moja ni dhahirikuwa asilimia kubwa ya migogoro inayotokea kwenye Mahusiano na Ndoa chanzo kikubwa ni kukosekana kwa uaminifu. Na ndio maana imekuwa mtindo wa kawaida kwa vijana kuchanganya wapenzi na wanandoa kutengeneza nyumba ndogo pasipo wao kujijua.

Mbaya zaidi tumefikia hatua ya kuhalalisha haya na kuyaona kuwa ni kawaida na hata wakati mwingine kujisifia mbele za watu pasipo "soni". Sawa, kila mmoja ana uhuru wa kufanya analotaka lakini tujiulize kuwa tunajijengea taswira gani kwa jamii na mustakabali wa vizazi vijavyo.

Uaminifu umekuwa ni changamoto ambayo kila mmoja inamlazimu kujitafakari kwa nafasi yake.

Nawasilisha kwa majadiliano.

​
(Uaminifu umekuwa ni changamoto ambayo kila mmoja inamlazimu kujitafakari kwa nafasi yake.) Nimechukua nafasi yangu natafakari kwa kina "BRB" nitarudi
 
Back
Top Bottom