Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Uaminifu duniani haupo, ila waaminifu tuna thawabu yetu mbinguni


Kweli kabisa,

Kwa wale wataoushinda huu mtihani, graduation yao lazima MC na mgeni rasmi awe ni Mungu mwenyewe!!

Ni kazi kubwa sana ila inawezekana!

Babu DC!!
 
jitu zima eti baby, mxsiii, sema bwana wanaume sijui mpoje, nasemaga mngekuwa na koromeo la kike maisha ya ndoa yangekuwa matamu sana, mpaka ujue mkeo anafanya,utakesha, na mwanamke yoyote anaefanya mpaka ashtukiwe huyo ni kiazi, sasa nyie limtu upo na mkeo kitandani unatuma msg kwa hawara eti" baby nitumie msg nzuri nilale" ovyo zenu.

Hayo ni miongoni mwa mambo ambayo siamini kama kweli yanaweza kufanywa na mtu ambaye hajaukaribia uchizi...

Anyway....dunia ina vichaa wengi!

Babu DC!!
 
Mkuu Mentor,

Hapo (blue) umepaona kweli??

Babu DC!!

Bondeni wapi mwa Tanzania au mwa Afrika au mwa Dunia??


Hahahahaaa Mentor kumbuka FP kasema mpango wa kando upo toka zamani ila sema inatakiwa usiri wa hali ya juu sasa nikiendelea kukomaa na kitochi changu si ntakamatwa aisee bora nikaache nirudi analogy!

Mh..kwa hali hiyo mi sioi!
 
Inawezekana kabisa sikuelewe hiyo UAMINIFU ina maana gani....
ni kwamba mimi nipo mwaminifu sana kwa mwenza as sitoki nje ya ndoa hata iweje lakini yeye anatoka tu nje naamua kuvumilia au ni vipi?
mimi nadhani kama wewe ni mwaminifu sana ni rahisi sana kushindwa kuvumilia mambo kama haya yanapojitokeza; unaweza kuvumilia mara moja au mbili baada ya hapo uvumilivu unaweza kupotea.
sijui labda mtu mzima mwenzangu Dark City aje kunisaidia hapa

Je ndoa gani zimedumu kwaajili ya uvumilivu wa mama/baba kwa matendo ayafanyayo mmoja kati yao?
Je ni zamani au sasa ambapo uvumilivu ulukua ni mkubwa sana?
 
jitu zima eti baby, mxsiii, sema bwana wanaume sijui mpoje, nasemaga mngekuwa na koromeo la kike maisha ya ndoa yangekuwa matamu sana, mpaka ujue mkeo anafanya,utakesha, na mwanamke yoyote anaefanya mpaka ashtukiwe huyo ni kiazi, sasa nyie limtu upo na mkeo kitandani unatuma msg kwa hawara eti" baby nitumie msg nzuri nilale" ovyo zenu.
ha haaa, umenichekesha sana Nyamayao, hayo yapo kabisaaa.
kuna siku mtu aliandika hapa yupo kwa kitanda na mkewe, mke yupo busy na simu, basi mara ajigeuze kushoto mara kulia mume anadhani anajilaza vizuri kumbe jamaa anafwata maelekezo kwa njemba huko nje, nilicheka sana.
 
Last edited by a moderator:
Duniani hamna uaminifu ila waaminifu tupo. Tukifanya uaminifu wetu tunaambiwa sisi ni waongo, wanafiki na wazugaji, but only God knows our hearts.

Hapo sasa nimekuelewa yakwamba watu hawataki kuamini kama waaminifu wapo katika dunia hii ila ukweli utabaki kuwa uvumilivu bila uaminifu ni bure.
 
Wakubwa wenzio tunakuelewa kabisa....

Hawa vijana inabidi ama waache hayo mambo ya nje kama sie au watumie akili kubwa, hekima na busara....

Vinginevyo, huku Ta wanaita kuhesabiwa vyuo......idadi inaweza kusoma hadi speed metre ikakatika!!

Babu DC!!
siku hizi naona kila kitu kimeshindikana....
imeshindikana kuwa wavumilivu na usiri pia umeshindikana, lol!
kila mtu anajua kila kitu, hakuna kificho.
Juzi mtoto wangu kaja kumsemelea mwenzie kuwa anaharibu pampers za dada yao :A S 39:
 
Kweli kabisa FP,

Mie kuna siku nilitania kabinti kamoja hivi kakasema kuwa katanipigia simu baadaye... Hadi naondoka mahali hapo hakakupiga......Nilipata taabu usiku mzima, hadi nakumbatia simu utadhani nimeokota kitita cha dola 1mil!!

Ilipofika asubuhi nikamwambia asipige na kwamba nimeenda nje ya nchi kikazi....

Ni biashara ya mateso sana hii... Laiti wangejua!

Babu DC!!
he he heee, hukawii kupata ugonjwa wa moyo.....
sasa babu ulikuwa umekumbatioa simu kwa sababu hutaki ku-miss call yake au sababu mida hiyo sasa upo na bibi unaogopa ikiwa mbali bibi anaweza aione kabla yako? maana hapo kuna utata, lol!
all in all hayo ni mateso jamani asikwambie mtu
 
ha haaa, umenichekesha sana Nyamayao, hayo yapo kabisaaa.
kuna siku mtu aliandika hapa yupo kwa kitanda na mkewe, mke yupo busy na simu, basi mara ajigeuze kushoto mara kulia mume anadhani anajilaza vizuri kumbe jamaa anafwata maelekezo kwa njemba huko nje, nilicheka sana.

Hapo ndipo tunasema uaminifu ni "0" yaani mnashindwa kuaminia,
umelala na mumeo/mkeo ila unahangaika na bashashi wengine nje huoni kama ni ukosefu wa uaminifu,
either mume alianza kukitembeza sasa mke anamalizia au wote wako katika ile hali ya kukomoana na mwisho wa siku inakuwa majuto yasiyo na tegemeo.
 
Naunga hoja mkono, uliyoyaandika ni sahihi kabisa. Cha muhimu ni kuacha ulimbukeni na kuwa strategic

[TD="class: style6"][/TD]
Habari zenu wana jamvini.

Ni muda kitambo tangu niwasilishe mada yangu ya mwisho na kupotea kutokana na majukumu ya maisha. Hivyo nalazimika kuwasilisha jamvini mada hii ili sote tuchangie maoni na tafakari zetu kwa kina.

Inaaminika kuwa moja ya nguzo kuu za kudumu kwa Mahusiano na Ndoa tangu zama zilizopita ni "uaminifu". Na hii ni moja ya sababu za msingi kwa wazazi wetu walio wengi kuendelea kuishi pamoja hadi sasa.

Kutokana na nyakati kubadilika katika vipindi kadhaa hadi sasa,uaminifu ktk Mahusiano na Ndoa vimekuwa adimu sana tofauti na hapo awali. Hali hii haihitaji utafiti wa kina sana kulithibitisha kwani liko wazi kwa namna ambavyo migogoro ilivyokuwa sehemu ya maisha ya Mahusiano na Ndoa za nyakati hizi hususan kwa vijana.

Inawezekana "Utandawazi" ukawa umechangia kwa kiasi kikubwa sana ktk hili kutokana na namna tulivyogeuzwa majuha wa kuamini kila tunaloliona kutoka nchi za magharibi. Matokeo yake tumetekwa na jinamizi la tamaa na wakati mwingine ulimbukeni wa kuona hivyo ndivyo namna sahihi ya kuishi ili kuonekana shujaa machoni mwa jamii.

Jambo moja ni dhahirikuwa asilimia kubwa ya migogoro inayotokea kwenye Mahusiano na Ndoa chanzo kikubwa ni kukosekana kwa uaminifu. Na ndio maana imekuwa mtindo wa kawaida kwa vijana kuchanganya wapenzi na wanandoa kutengeneza nyumba ndogo pasipo wao kujijua.

Mbaya zaidi tumefikia hatua ya kuhalalisha haya na kuyaona kuwa ni kawaida na hata wakati mwingine kujisifia mbele za watu pasipo "soni". Sawa, kila mmoja ana uhuru wa kufanya analotaka lakini tujiulize kuwa tunajijengea taswira gani kwa jamii na mustakabali wa vizazi vijavyo.

Uaminifu umekuwa ni changamoto ambayo kila mmoja inamlazimu kujitafakari kwa nafasi yake.

Nawasilisha kwa majadiliano.

​
 
Hayo ni miongoni mwa mambo ambayo siamini kama kweli yanaweza kufanywa na mtu ambaye hajaukaribia uchizi...

Anyway....dunia ina vichaa wengi!

Babu DC!!

Tunasemaga watu wote ni vichaa ila tumetofautiana ukichaa wetu.
 
Naunga hoja mkono, uliyoyaandika ni sahihi kabisa. Cha muhimu ni kuacha ulimbukeni na kuwa strategic

Iwapo kuaminiana kwa msingi kabisa katika uhusiano kutavunjwa mara kwa mara, hasira za mpenzi kwa mwenzake zitalimbikizwa na hamu ya wapenzi/wenza kuendelea kuishi pamoja itapungua. Wapenzi walio katika uhusiano wenye mizizi na afya njema wanaweza kukubaliana kumaliza tofauti zao na kusonga mbele.

Kama wataheshimu ahadi na viapo vyao vipya mambo yataendelea.
 
Hakika saudari
Iwapo kuaminiana kwa msingi kabisa katika uhusiano kutavunjwa mara kwa mara, hasira za mpenzi kwa mwenzake zitalimbikizwa na hamu ya wapenzi/wenza kuendelea kuishi pamoja itapungua. Wapenzi walio katika uhusiano wenye mizizi na afya njema wanaweza kukubaliana kumaliza tofauti zao na kusonga mbele. Kama wataheshimu ahadi na viapo vyao vipya mambo yataendelea.
 

Iwapo itatokea kuwa mmoja wa wapenzi/marafiki au wote wawili akawa hajitambui na kufuata matakwa yake, mahitaji yake, matamanio yake, mipango yake ya baadaye, malengo yake, msimamo wake, hulka yake na vipaumbele vyake, haitakuwa rahisi kwa watu hawa wawili kuwa na uhusiano wenye afya.
 
Kweli kabisa FP,

Mie kuna siku nilitania kabinti kamoja hivi kakasema kuwa katanipigia simu baadaye... Hadi naondoka mahali hapo hakakupiga......Nilipata taabu usiku mzima, hadi nakumbatia simu utadhani nimeokota kitita cha dola 1mil!!

Ilipofika asubuhi nikamwambia asipige na kwamba nimeenda nje ya nchi kikazi....

Ni biashara ya mateso sana hii... Laiti wangejua!

Babu DC!!

si ulikapa no mwenywe, wewe utakuwa mtaalamu, unakula unafuta mdomo, hahaha,jokes aside, haya mambo yanakera sana, kuna mkaka tupo nae ofisini,ana mobile anaiachaga ofisini ni special kwa uzinifu tu, anakwambia simpi mpango wa nje no yangu halisi hata siku moja, anavyowabadili sasa, na mkewe anavyojisifia kuhusu mume wake, yaani namwangaliaga kimoyoni nasema laiti we mwanamke ungelijua usingekaa ujidai mbele za watu mume wangu hivi wala vile, mie ndio mana nikiingiaga ofisini kwa msukuma sitaki kuchekewa mara mbili, kusanifiana tu, sijui kwanini sikwendaga u sister, lol
 
Back
Top Bottom