saudari
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 2,655
- 2,783
Habari zenu wana jamvini.
Ni muda kitambo tangu niwasilishe mada yangu ya mwisho na kupotea kutokana na majukumu ya maisha. Hivyo nalazimika kuwasilisha jamvini mada hii ili sote tuchangie maoni na tafakari zetu kwa kina.
Inaaminika kuwa moja ya nguzo kuu za kudumu kwa Mahusiano na Ndoa tangu zama zilizopita ni "uaminifu". Na hii ni moja ya sababu za msingi kwa wazazi wetu walio wengi kuendelea kuishi pamoja hadi sasa.
Kutokana na nyakati kubadilika katika vipindi kadhaa hadi sasa,uaminifu ktk Mahusiano na Ndoa vimekuwa adimu sana tofauti na hapo awali. Hali hii haihitaji utafiti wa kina sana kulithibitisha kwani liko wazi kwa namna ambavyo migogoro ilivyokuwa sehemu ya maisha ya Mahusiano na Ndoa za nyakati hizi hususan kwa vijana.
Inawezekana "Utandawazi" ukawa umechangia kwa kiasi kikubwa sana ktk hili kutokana na namna tulivyogeuzwa majuha wa kuamini kila tunaloliona kutoka nchi za magharibi. Matokeo yake tumetekwa na jinamizi la tamaa na wakati mwingine ulimbukeni wa kuona hivyo ndivyo namna sahihi ya kuishi ili kuonekana shujaa machoni mwa jamii.
Jambo moja ni dhahirikuwa asilimia kubwa ya migogoro inayotokea kwenye Mahusiano na Ndoa chanzo kikubwa ni kukosekana kwa uaminifu. Na ndio maana imekuwa mtindo wa kawaida kwa vijana kuchanganya wapenzi na wanandoa kutengeneza nyumba ndogo pasipo wao kujijua.
Mbaya zaidi tumefikia hatua ya kuhalalisha haya na kuyaona kuwa ni kawaida na hata wakati mwingine kujisifia mbele za watu pasipo "soni". Sawa, kila mmoja ana uhuru wa kufanya analotaka lakini tujiulize kuwa tunajijengea taswira gani kwa jamii na mustakabali wa vizazi vijavyo.
Uaminifu umekuwa ni changamoto ambayo kila mmoja inamlazimu kujitafakari kwa nafasi yake.[/FONT]
Nawasilisha kwa majadiliano.