Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,385
- 100,492
Mpwa mie mzima namshukuru Mwenyezi Mungu kumekucha oohh sorry kumekuchwa nipo hapa Kwa Mtogole nauza gahawa kwanzaMpwa wangu, mzima weye?
Mpwa mie mzima namshukuru Mwenyezi Mungu kumekucha oohh sorry kumekuchwa nipo hapa Kwa Mtogole nauza gahawa kwanzaMpwa wangu, mzima weye?
rafiki asante kwa hii kitu......
inabidi niishie hapa hapa nisije nikatoa machozi bure, lol!
Kweli kabisa FP,
Mie kuna siku nilitania kabinti kamoja hivi kakasema kuwa katanipigia simu baadaye... Hadi naondoka mahali hapo hakakupiga......Nilipata taabu usiku mzima, hadi nakumbatia simu utadhani nimeokota kitita cha dola 1mil!!
Ilipofika asubuhi nikamwambia asipige na kwamba nimeenda nje ya nchi kikazi....
Ni biashara ya mateso sana hii... Laiti wangejua!
Babu DC!!
[TD="class: style6"][/TD]
Habari zenu wana jamvini.
Ni muda kitambo tangu niwasilishe mada yangu ya
mwisho na kupotea kutokana na majukumu ya maisha. Hivyo nalazimika
kuwasilisha jamvini mada hii ili sote tuchangie maoni na tafakari zetu
kwa kina.
Inaaminika kuwa moja ya nguzo kuu za kudumu kwa
Mahusiano na Ndoa tangu zama zilizopita ni "uaminifu". Na hii ni moja ya
sababu za msingi kwa wazazi wetu walio wengi kuendelea kuishi pamoja
hadi sasa.
Kutokana na nyakati kubadilika katika vipindi kadhaa
hadi sasa,uaminifu ktk Mahusiano na Ndoa vimekuwa adimu sana tofauti na
hapo awali. Hali hii haihitaji utafiti wa kina sana kulithibitisha kwani
liko wazi kwa namna ambavyo migogoro ilivyokuwa sehemu ya maisha ya
Mahusiano na Ndoa za nyakati hizi hususan kwa vijana.
Inawezekana "Utandawazi" ukawa umechangia kwa kiasi
kikubwa sana ktk hili kutokana na namna tulivyogeuzwa majuha wa kuamini
kila tunaloliona kutoka nchi za magharibi. Matokeo yake tumetekwa na
jinamizi la tamaa na wakati mwingine ulimbukeni wa kuona hivyo ndivyo
namna sahihi ya kuishi ili kuonekana shujaa machoni mwa
jamii.
Jambo moja ni dhahirikuwa asilimia kubwa ya migogoro
inayotokea kwenye Mahusiano na Ndoa chanzo kikubwa ni kukosekana kwa
uaminifu. Na ndio maana imekuwa mtindo wa kawaida kwa vijana kuchanganya
wapenzi na wanandoa kutengeneza nyumba ndogo pasipo wao
kujijua.
Mbaya zaidi tumefikia hatua ya kuhalalisha haya na
kuyaona kuwa ni kawaida na hata wakati mwingine kujisifia mbele za watu
pasipo "soni". Sawa, kila mmoja ana uhuru wa kufanya analotaka lakini
tujiulize kuwa tunajijengea taswira gani kwa jamii na mustakabali wa
vizazi vijavyo.
Uaminifu umekuwa ni changamoto ambayo
kila mmoja inamlazimu kujitafakari kwa nafasi yake.
Nawasilisha kwa majadiliano.