Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Uaminifu na changamoto za mahusiano na ndoa

Wanaibiana au mmoja anaibwa? Kweli unatelekeza familia (finacially na socially) kwa ajili ya OW halafu waweza sema unamuibia huyo OW? Si kuibwa tu huko!


Ukifikia kwenye kutelekeza familia bwana mie naona unaelekea kwenye uchizi....

Hata wazee wetu pamoja na kwamba tunasema hawakuwa waaminifu ila ni wachache sana waliotelekeza familia...

Na hapa naongelea kule kwetu bondeni ambako mila zilikuwa juu ya kila mtu!!

Babu DC!!
 
ha ha haaa, sasa unakuwaje na nyumba ndogo ambayo haijui mipaka rafiki? tafuta ambaye anajua sasa upo kwa mamsap hakuna simu wala sms..... mambo yanaishia juu kwa juu, lol!


Hapo sasa,

Yaani hata mimi nashindwa kuelewa kama mtu mwenye akili zako unaweza kumwachia huru small house hadi awe na 100% access kiasi cha kukutumia sms wakati wewe unapata dina takatifu..

Sielewi kwa kweli..

Babu DC!!
 
uaminifu unapungua kwa sababu ya tamaaa

Sidhani kama kuna tofauti ya uaminifu kati ya sasa na zamani....

Tatizo ni kwamba siku hizi kila mtu kawa mjanja kiasi kwamba inakuwa rahisi kukamatana!

Na pia akina dada naoa wamekuwa tofauti na mama zetu...wanajirusha utadhani bado ni mabinti!

Babu DC!!
 
Hapo sasa,

Yaani hata mimi nashindwa kuelewa kama mtu mwenye akili zako unaweza kumwachia huru small house hadi awe na 100% access kiasi cha kukutumia sms wakati wewe unapata dina takatifu..

Sielewi kwa kweli..

Babu DC!!
ha haaaa,
tatizo hawa wadogo zetu hawajui nini kinatakiwa kuendelea huko nje ya nyumba....
wenzao wa zamani walikuwa wanaenda nje kwa mambo mengine tu lakini wanajua yule mama nje hatathubutu kumzukia mke wake, hata iweje....... wakikutana kisimani ni heshima na adabu
 
Sidhani kama kuna tofauti ya uaminifu kati ya sasa na zamani....

Tatizo ni kwamba siku hizi kila mtu kawa mjanja kiasi kwamba inakuwa rahisi kukamatana!

Na pia akina dada naoa wamekuwa tofauti na mama zetu...wanajirusha utadhani bado ni mabinti!

Babu DC!!
hapo kwenye red mnataka tufanyeje sasa? tukikaa kama wamama hamtutaki, inabidi tuwe kama mabinti ili kuweza ku-compete, lol!
(hapa sijaandika mimi jamani, kuna aliyeiba pwad yangu)
 
kwa nini usikubaliane na sisi babu wakati tunaongea uhalisia!
salama lakini babu?
kuna siku nilitumwa na baba kwa rafiki yake. nikamkuta mama wa nyumba, nikamwambia shida yangu akaniambia "baba hayupo kaenda kwa mke wake sehemu fulani"
huyu mama alokuwa anajua kabisa kuwa baba ana nyumba ndogo sehemu...... kumbuka kuwa hii nyumba ndogo si halali maana walikuwa Wakristo..... lakini ndo hivyo yametokea, nakimbia nyumba?
tena mimi naweza kusema wababa wa zamani hawakuwa waaminifu kabisa. huko ambako mimi nimekulia wababa karibia woote walikuwa na nyumba za pembeni (including baba yangu, lol!)


Mie niliokuwa mkubwa, nilikuja kujua kuwa baba naye alikuwa anachacharika...ila nikaambiwa kwamba mama alikuwa anajulikana kwamba ni mkali sana kiasi kwamba hakuna mwanamke alikuwa anakubali kuingia kwenye anga zake...

Hata kuna kipindi kila mtu aliishi kivyake vyake na bado hatukuweza kupata mama wa kambo...

Nasikia hata wadogo zetu wa huko mtaani wamepotelea hewani!!

Babu DC!!
 
hapo kwenye red mnataka tufanyeje sasa? tukikaa kama wamama hamtutaki, inabidi tuwe kama mabinti ili kuweza ku-compete, lol!
(hapa sijaandika mimi jamani, kuna aliyeiba pwad yangu)


Umesamehewa mkubwa mwenzangu,

Ndiyo maana kuna watu wanaamini kuwa dunia ya sasa hivi imevaa pensi nyanya.....

Babu DC!!
 
Mie niliokuwa mkubwa, nilikuja kujua kuwa baba naye alikuwa anachacharika...ila nikaambiwa kwamba mama alikuwa anajulikana kwamba ni mkali sana kiasi kwamba hakuna mwanamke alikuwa anakubali kuingia kwenye anga zake...

Hata kuna kipindi kila mtu aliishi kivyake vyake na bado hatukuweza kupata mama wa kambo...

Nasikia hata wadogo zetu wa huko mtaani wamepotelea hewani!!

Babu DC!!
wewe nani anataka kuingia kwenye mdomo wa mamba?
hata kama mimi nikiona nina mimba kwanza wala simwambii huyo mwenye mimba yake maana asije akaja kudai mtoto halafu nikajikuta napambana na mamba. hiyo itakuwa siri yangu.....
 
Babu Funguka enzi zenu ilikuwaje ili tuige kama kuiba au kuwa wapole!


Hahaahhahahah,

Unataka nikueleze nini wewe mtoto??

Enzi zile tunakua, tulikuwa tunasimuliwa na kaka zetu kwamba ukitaka raha sana tembea na mama mtu mzima...ila pia wazazi wetu walikuwa wanapinga sana mambo ya kuonja onja hovyo...

Nakumbuka kuna siku mie na mama tulitaka kuzuliana kosovo...alikuwa ananikanya niache kutembea usiku usiku na mie ndo nimeshaingia sekondari... Nikamwambia kwamba, kwani unaogopa nitapata mimba??

Timbwili lake hadi sitaki kukumbuka...lol!!

Babu DC!!
 
wewe nani anataka kuingia kwenye mdomo wa mamba?
hata kama mimi nikiona nina mimba kwanza wala simwambii huyo mwenye mimba yake maana asije akaja kudai mtoto halafu nikajikuta napambana na mamba. hiyo itakuwa siri yangu.....


Hapa umenikumbusha maneno ya yule bibi wa movie ya Titanic....

Kweli moyo wa mwanamke ni hatari kwa kuficha siri....

Ila kwa wazee wetu, hilo lilikuwa siyo tatizo kwani naye alikuwa anawachezea faulo wengine!

Babu DC!!
 
Hapa napita tu. Kukosa uaminifu kunachefua roho haswaaa. Unakuwa na mwenza asie muaminifu na unajua kabisa kuwa sio mwaminifu! Kuna mapenzi hapo? Yale.ya kuipenda tanzania ama kuivumilia tanzania!


Haya mambo yasikie kwa wengine mdogo wangu...
Inapotokea mtu akawa amejitoa wakati mwenzake anashinda uchochoroni akiwinda inakera sana...

Ila kwa mama zetu, naona walikuwa na uwezo mkubwa wa kuhimiri michomo kama hiyo..

Babu DC!!
 
Hapa umenikumbusha maneno ya yule bibi wa movie ya Titanic....

Kweli moyo wa mwanamke ni hatari kwa kuficha siri....

Ila kwa wazee wetu, hilo lilikuwa siyo tatizo kwani naye alikuwa anawachezea faulo wengine!

Babu DC!!
ha ha haaa chezeya mwanamama weye.......
mnavyofanya madudu yenu sisi tunawacheck tu....
unasema mke wangu mvumilivu sana hujui kumoyo kwake kunawaza nini
 
Hapa FP Dark City Kaunga na snowhite mnapozungumzia UVUMILIVU Mnatakiwa muangalie na nyakati.
'
Mtu akitoka nje ya ndoa hana kawaida ya kuacha,atarudia tu
'
Sasa kwa mazingira ya sasa kuwa mvumilivu ni kujitafutia kaburi la mapema
'
Mahawara hawaachani
sosi: Fidel80 !
 
Last edited by a moderator:
Heheheheee yan ukiwa umejidunga ndovu ukapitiwa na kausingizi kameseji kakiingia tu wife anaanza nako lol
Utashangaa umezabwa kofi ukiwa usingizini lol utakurupukaje heheheheee kakutana na ka sms kameanza na Baby.....!

Utandawazi noma mi nataka kuachana na simu!

Kha bro Erickb52, nilidhani unataka kuachana na mpango wa kando kumbe...:A S 39:

Ukifikia kwenye kutelekeza familia bwana mie naona unaelekea kwenye uchizi....

Hata wazee wetu pamoja na kwamba tunasema hawakuwa waaminifu ila ni wachache sana waliotelekeza familia...

Na hapa naongelea kule kwetu bondeni ambako mila zilikuwa juu ya kila mtu!!

Babu DC!!

Babu DC, naomba kufahamu hao wazeee unaowaongelea hapa ni wa umri gani.

1. Huyu ni msomi kabisa mwenye mtoto wa kwanza wa 1972. Aliacha familia kabisaaaa akahamia kwa bi mdogo. Aliiacha familia wakati mtoto wa mwisho (1980) ana miaka 18. Akiwa mzee kabisa pale unapodhani ashazeeka maini.

2. Babu huyu wa 1922 alibahatika kusafiri sana alipokuwa kijana hadi Mombasa ana watoto. Aliporudi kijijini akaamua kuoa kila baada ya nyumba tano. Akaiacha familia yake ya watoto nane akahamia kwa wake wadogo.

Ni wazee wapi hao tunaowaongelea hapa wasioacha familia zao??

Niachojua tu ni hiki: "Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa." (Mithali 6:32)

Hata kwangu na ujana huu nimejionea the moments I played around nothing productive went on with my life.
 
Last edited by a moderator:
Kikubwa ni Kuomba Uzima tu panapokuwa na uaminifu hata mafanikio katika maisha huchangiwa sana na uwepo wa uaminifu katika ndoa. Dini ni kichocheo kizuri sana katika kudumisha uaminifu, muogope muumba wako na uheshimu ndoa yako ndipo hayo mema ya Mbingu yatakapowekwa mikononi mwenu
 
saudari sasa wewe teacher,
darasa lako limetokaje kwanza?

Unataka uaminifu gani wakati ukifanya kimoja ndo
unaanza kukoroma hata wapita njia wanasikia
akuvumilie tu?
 
Last edited by a moderator:
FP, Kaunga, Dark City, snowhite, Mentor na Mamndenyi.

Watu wa zama hizo walikuwa wakifunzwa sana namna ya kuishi katika ndoa kwa uvumilivu.Msichana alifunzwa namna ya kukaa na mumewe na alifunzwa majukumu muhimu aliotakiwa mwanamke ayamudu.

Hivyo basi ilikuwa rahisi sana kukaa katika ndoa.Pia zama hizo maadili yalitunzwa sana katika jamii,kutoka kabila na kabila kila moja laikuwa amekuzwa katika maadili mema sana yaliyojali sana kutunza mila na desturi.Hii ilikuwa kwa namna zote,kivazi, kimwenendo, kiusafi,kufanya kazi kwa bidii, heshima,kujali nk.

Pia katika kabila zingine kama kabila ninalotoka mimi mwanaume alikuwa huru kuoa zaidi ya mke mmoja na kulikuwa na makubaliano na mke/wake alio nao ndani na sababu zilielezwa wazi.Kwa mfano mke alipokuwa mja mzito haikuruhusiwa mwanaume umguse mkeo kindoa,hadi anajifungua nakijifungu labda mwaka upite ndipo akujulie hali.Hiyo ilikuwa kama kinyaa kutembea na mwenye mimba na ambaye ana mtoto mchanga.

Kwa ajili hiyo basi ilikuwa lazima kuwa na mtu mwiongine mbadala ambaye ni mke wa pili au wa tatu ili kutimiza mapenzi hayo.Pia kutokana na maadili ya kijamii yaliyokuwepo ilikuwa ni nuksi sana kwa mwanaume kukamatwa ugoni.Na jambo hilo lilishughulikiwa kijamii hapohapo kijijini kwa adhabu kali sana na yamkini hata kutengwa.Pia mtoto wa kike aliyepata mimba alihesabika ni mdhambi na hafai kijijini hata kuolewa, maana ameiabisha familia yake. Ili kukwepa hayo yote na balaa za kijamii watu walijitunza na kuheshimu sana maadili ya kiukoo,kijamii,kikabila pia.
 
Well said FP kilichopungua siku hizi ni UVUMILIVU; na kilichoongezeka ni ACCESS to Information kiasi kwamba wazinzi wanakamatwa kirahisi.

Ila mtoa mada namsupport Lack of UAMINIFU ni kirusi cha mahusiano hadi inachefua when thinking of it.

Mi nadhani kama mtu si mwaminifu huwezi kuwa mvumilivu.
Lazima uwe mwaminifu kwanza ndio uvumilivu ufuate. Lakini FP anakazia sana kwenye uvumilivu bila kuangalia upande wa uaminifu.
 
Last edited by a moderator:
Utandawazi noma mi nataka kuachana na simu!

Tunapoongelea utandawazi mara nyingi tunaongelea picha zinazoonekana kwenye TV, na internet. Watoaji wakubwa wa content za TV na internet zinazolalamikiwa sana ni Wamarekani. Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa watu wanapolaumu utandawazi kuharibu maadili huwa wanailaumu Marekani.

Lakini nimefuatilia kidogo historia ya Marekani ni taifa ambalo limeundwa kwenye msingi wenye nguzo mbili tu. Nguzo ya kwanza ni UHURU (Liberty) na UTAFUTAJI WA RAHA (Pursuit of happiness).

Lilikuwa ni taifa la majaribio lililoundwa na wazungu waliokuwa wanakimbia tawala za kidini na zenye mila na desturi kali za Ulaya, ambako ndiko chimbuko la wazungu, na hivyo kutokana na wao kuwa wameishi Ulaya muda mrefu sana wakajikuta wamejitwika mila ambazo wengine zilikuwa zinawakandamiza.

Sasa ukiangalia hivyo utagundua kwamba misingi ya Marekani ni misingi ya binadamu wengi tu duniani. Kila mtu anapenda uhuru na anapenda kupata raha. Ndio maana mambo mengi wanayofanya Wamarekani yanapokelewa vizuri hata nje ya Marekani. Na hata ukiangalia taifa lenyewe la Marekani hivi sasa ni mkusanyiko wa watu toka kila pande ya dunia, hivyo waweza kusema ni wawakilishi wa dunia. Imefikia steji wanaongozwa na raisi mwenye damu ya Kenya. Hata sisi weusi wa Afrika tunaona kabisa kuwa kumbe Marekani inatuhusu.

Sasa utakuta hali kama iliyotokea Marekani inatokea sehemu nyingi. Watu wanapohama toka vijijini kwenda mijini ni sawa sawa na wazungu waliohama toka Ulaya kwenda Marekani.

Vile vifungo vya mila vilivyokuwa vinawabana vijijini huku mijini havipo, maana huku ni mkusanyiko wa watu toka pande zote Tanzania. Hakuna anayeweza kusema mila za kwao ndio zitawale mjini, kwa hiyo watu wanakuwa huru zaidi, na wanakuwa na uwezo zaidi wa kufanya ile kitu roho inapenda.
 
naomba nichangie kidogo hapo nilipoweka RED. sidhani kama ni sahihi kusema kuwa wazazi wetu waliweza kudumu katika ndoa sababu ya uaminifu waniokuwa nao katika ndoa, hii si kweli hata kidogo. Naamini wazazi wetu waliweza kudumu sababu ya UVUMILIVU waliokuwa nao wazazi wetu, hasa wamama zetu + usiri waliokuwa nao wamama zetu wanapoamua kutoka nje ya ndoa. hapa labda ninachoweza kusema tu ni kwamba kwa sasa sababu ya haya mambo ya utandawazi basi kila kitu ni rahisi sana kugundulika. Usiri haupo tena ndo maana wenza inawawia rahisi sana kuwabamba wenzao..... lakini haya yalikuwepo tangu zamani
Ndio maana nikasema ndoa nyingi za zamani mpaka sasa zinaishi vizuri huku zikijawa na amani tele pamoja na furaha isiyo na kifani, yote hayo yametokana na uaminifu wao katika ndoa ambao unazalisha kitu kingine kiitwacho uvumilivu.. Kumdanganya mpenzi mara kwa mara, kumsaliti mara kwa mara na kuvunja ahadi zako mara kwa mara huufanya uhusiano kudhoofika na hatimaye nguzo yake muhimu yaani uaminifu kuanguka.

Hapo ndipo uhusiano hufika kikomo.
 
Back
Top Bottom