Twitter na Facebook zafuta akaunti zinazofadhiliwa na serikali kueneza uongo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mtandao wa kijamii wa Twitter umesema leo kuwa umezifuta akaunti 6,000 zilizokuwa sehemu ya juhudi kubwa ya serikali ya Saudi Arabia na watu binafsi ya kutanua maslahi ya kisiasa na kieneo ya taifa hilo.

Twitter imesema akaunti hizo zimekuwa zikisambaza maudhui ya kupigia upatu mamlaka za Saudia ikiwemo kushajihisha mjadala kuhusu vikwazo dhidi ya Iran.

Kwa upande wake mtandao wa Facebook umesema umeondoa mamia ya akaunti, makundi na kurasa zilizolenga kuwashambulia watu nchini Marekani na Vietnam.

Hatua hizo ni sehemu ya juhudi za kampuni kubwa za mitandao ya kijamii za kupunguza wimbi la taarifa potofu kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2020.

Hayo yanafuatia ufichuaji uliosema kuwa Urusi ilitumia akaunti bandia kufikisha matangazo ya uongo ya kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2016 nchini Marekani.
 
Siku Max akiamua kufuta kule Jukwaa la Siasa, CCM wataandamana.
 
Back
Top Bottom