Mkuu wacha poverty mentality. Siyo kila mwenye account Uswiss ni mwizi wa hela za Magufuli. Wengine walisoma huko..kwa hiyo baada ya kuondoka account wakaamua wasizifunge. Wengine walizifungua kwa ajili ya urahisi wa kulipa karo za watoto wao wanaosoma nje.....(siyo kila mtu anasomesha mtoto shule za kata) na wengine wamefungua kwa ajili ya biashara zao.
Kwa mtu kama MO kuwa na account Uswiss, US na kwingineko ni kitu cha kawaida maana anafanya transactions za kimataifa..so kufanya miamala inakuwa rahisi kama una account huko. And mostly don't forget....watu wanataka security ya utajiri wao!
Hizi nchi zetu JPM akiamka amekasirika unaweza kuta account zako zote 'zinafanyiwa uchunguzi' whatever that means! ...Tanzania tumefika sehemu hata ukiendesha mtumba wa Range rover utaambiwa wewe ni fisadi!
Mkuu kuna wenye account zao Dubai, Uswiss na kwingineko with clean money! so usifanye assumptions based on your economic situation au ambavyo umeaminishwa na watawala.