Tuzo ya Mo Ibrahim yakosa tena mshindi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,133
164,556
Hiyo imetangazwa na DW radio

========
Tuzo ya Mo Ibrahim 2016 yakosa mshindi
Wakfu wa Mo Ibrahim umetangaza kwamba hakutokuweko na mshindi wa tunzo yake uongozi bora barani Afrika kwa mwaka 2016.

17966471_303.jpg

Tangazo hilo lilitolewa Jumanne ( Februari 28 ) kutokana na mkutano wa kamati uhuru ya tuzo hiyo, chini ya Uweyekiti wa Dr Salim Ahmed Salim pamoja na mkutano wa bodi ya wakfu huo uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa kamati ya tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, Dr Salim alisema " kama ninavyosisitiza kila mwaka , paliwekwa kipimo cha hali ya juu, wakati tukizindua tuzo hii 2006.

Tunatambua na kupongeza mchango muhimu unaotolewa na viongozi wengi wakiafrika kuleta mabadiliko katika nchi zao . Lakini tuzo hii inakusudiwa kumulika na kusherehekea uongozi wa aina yake, jambo ambalo si la kawaida ukizingatia kielelezo halisi."

Dr Salim akaongeza kusema kwamba baada ya zingatio makini, kamati hiyo imeamua kutomzawadia yeyote tuzo hiyo kwa mwaka 2016.

Wagombea wote wa tuzo ya Ibrahim ni ama Viongozi wa taifa au Serikali waliondoka madarakani katika kipindi cha miaka mitatu iliopita na ambao walikuwa wamechaguliwa kidemokrasi na kutumikia vipindi vyao kwa mujibu wa katiba.

Tangu ilipoanzishwa 2006, tuzo ya Mo Ibrahim imeshatolewa mara nne. Washindi waliopita ambao wote walikuwa marais wa nchi zao ni, Hifikepunye Pohamba wa Namibia (2014), Pedro Pires wa visiwa vya Cape Verde (2011), Festus Mogae wa Botswana (2008) na Joaquim Chissano wa Msumbiji (2008). Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela alitunukiwa tuzo ya heshima 2007.

Wakfu wa Mo Ibrahim unatarajia kuwa na tamasha maalum , " Wikiendi ya Utawala," mjini Marrakech Morocco kuanzia Aprili7-9 2017. Tamasha hilo litafunguliwa Ijumaa jioni kwa mjadala wa ngazi ya juu uliopewa jina, " Mazungumzo kuhusu Uongozi ", yakizingatia changamoto za uongozi duniani katika karne ya 21 .

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman / Mtandao wa Mo Ibrahim

Mhariri:Iddi Ssessanga

Chanzo: Dw Kiswahili
 
Nina uhakika JPM atachukua. Mark my words.
Huwezi kukandamiza DEMOKRASIA kwa namna yo yote na ukashinda tuzo hii. Haitatokea Rais kupitia CCM akaipata kwa sababu wote fikira mna mitazamo yao ni ile ile: kuhakikisha CCM inaendelea kutawala milele at 'any cost' - mfano hai ni ule ukabaji wa mchana kweupe wa uchaguzi wa Zanzibar 2015. JPM hana hata pretense ya kuipa demokrasia ipumue.
 
Kwani Kikwete alikuambia au alishatutangazia kuwa anaigombea Mkuu?
Hiyo tuzo haigombewi bali inatolewa kwa kiongozi yeyote aliyestaafu ndani ya miaka mitatu na anayetimiza vigezo. Kikwete angetimiza vigezo angeitwa kuipokea bila kuigombea. Zawadi yenyewe ni $5m tu ambazo sidhani kama ni nyingi za kumfanya mtu kama Kikwete asononeke kutozipata, nadhani la muhimu hapa ni ile heshima inayoendana nazo tu.
 
Hakuna rais wa Africa aliyefanikiwa kupata tuzo ya Mo Ibrahim pengine Rais Kikwete angefanikiwa kutupa katiba mpya angeshinda tuzo hii.
Meaning the whole of Africa id ruled by dictators/takataka! under the iron fist
 
.....unasahau anakandamiza demokrasia na kufuta mikutano siasa hataki kukosolewa...tuzo itaendelea kukosa candidate kila mwaka
 
Hiyo imetangazwa na DW radio

========
Tuzo ya Mo Ibrahim 2016 yakosa mshindi
Wakfu wa Mo Ibrahim umetangaza kwamba hakutokuweko na mshindi wa tunzo yake uongozi bora barani Afrika kwa mwaka 2016.

View attachment 475541
Tangazo hilo lilitolewa Jumanne ( Februari 28 ) kutokana na mkutano wa kamati uhuru ya tuzo hiyo, chini ya Uweyekiti wa Dr Salim Ahmed Salim pamoja na mkutano wa bodi ya wakfu huo uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa kamati ya tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, Dr Salim alisema " kama ninavyosisitiza kila mwaka , paliwekwa kipimo cha hali ya juu, wakati tukizindua tuzo hii 2006.

Tunatambua na kupongeza mchango muhimu unaotolewa na viongozi wengi wakiafrika kuleta mabadiliko katika nchi zao . Lakini tuzo hii inakusudiwa kumulika na kusherehekea uongozi wa aina yake, jambo ambalo si la kawaida ukizingatia kielelezo halisi."

Dr Salim akaongeza kusema kwamba baada ya zingatio makini, kamati hiyo imeamua kutomzawadia yeyote tuzo hiyo kwa mwaka 2016.

Wagombea wote wa tuzo ya Ibrahim ni ama Viongozi wa taifa au Serikali waliondoka madarakani katika kipindi cha miaka mitatu iliopita na ambao walikuwa wamechaguliwa kidemokrasi na kutumikia vipindi vyao kwa mujibu wa katiba.

Tangu ilipoanzishwa 2006, tuzo ya Mo Ibrahim imeshatolewa mara nne. Washindi waliopita ambao wote walikuwa marais wa nchi zao ni, Hifikepunye Pohamba wa Namibia (2014), Pedro Pires wa visiwa vya Cape Verde (2011), Festus Mogae wa Botswana (2008) na Joaquim Chissano wa Msumbiji (2008). Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela alitunukiwa tuzo ya heshima 2007.

Wakfu wa Mo Ibrahim unatarajia kuwa na tamasha maalum , " Wikiendi ya Utawala," mjini Marrakech Morocco kuanzia Aprili7-9 2017. Tamasha hilo litafunguliwa Ijumaa jioni kwa mjadala wa ngazi ya juu uliopewa jina, " Mazungumzo kuhusu Uongozi ", yakizingatia changamoto za uongozi duniani katika karne ya 21 .

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman / Mtandao wa Mo Ibrahim

Mhariri:Iddi Ssessanga

Chanzo: Dw Kiswahili
Hivi hiyo tuzo ni muhimu sana?je kama wameishiwa pesa tutajuaje?
 
Mo siku hizi hana pesa tu. Aache ubishoo aseme ukweli

Sio pesa bali hawakidhi vigezo! Au wewe unadhani nani alistahili? Wengi wao wanastahili kuwa The Hague korokoroni badala ya kuwa shortlisted!
 
Back
Top Bottom