Tuzo ya Demokrasia na Utetezi wa Haki za Binadamu aliyotunukiwa Tundu Lissu iwe neema kwa chama

Mbogo nyeusi

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
233
540
Chadema kwa muda mrefu imesemwa sana kwa kushindwa kujenga majengo yake Kama ofisi kuanzia ofisi ya makao makuu, kanda, mkoa na hata majimbo ya uchaguzi na kata.

Nakubaliana na hoja kuwa ruzuku waliyo kuwa wanapokea kama chama isingeweza kujenga ofisi, kulipa mishahara ya wafanyakazi na kufanya operation za chama,

Kwa Sasa natambua Chadema wapo hoi kifedha hawana ruzuku, njia waliyo nayo kwa sasa ili waweze kupata fedha za kujiendesha ni kuendelea kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi na kutengeneza nadharia ya kuonewa (japo ni kweli wanaonewa) kwa wahasimu wa serikali hii ya awamu tano.

Ni ukweli ulio wazi nchi yetu kwa sasa tuna mahusiano mabovu na ubaguzi na mataifa mengine hususani mataifa ya mabeberu ambao walikuwa wakiisaidia Tanzania kwa kufanikisha miradi mingi ya kimaendeleo, hakuna wa kuweza kupuuza hilo tunajua Kuna barabara, miradi ya maji, shule na hospitali zimefadhiliwa na mabeberu.

Baadhi ya hao mabeberu wameonekana kuwanyemelea chadema na nimesikia wengine wakitishia kusitisha fedha zilizo kuwa zinatolewa kama msaada na zawadi Tanzania na kuweka nguvu kuimarisha vyama makini vya upinzani Tanzania.

Kama serikali itaendelea kuwa wababe itaendelea kuwa neema kwa Chadema, hivyo nakishauri Chadema ikifanikisha kuwanasa mabeberu, na pesa zilizokuwa zinaelekezwa kwa serikali zikapelekwa kwao Kama nilivyo sikia kwa mjumbe wa kamati ya bunge la ulaya, chadema pamoja na Mambo mengine ijikite kujenga ofisi nzuri na za kisasa kuanzia makao makuu, majimbo, mikoa wilaya na majimbo ya uchaguzi, kata na hata mashina, nashauri nguvu kubwa ielekezwe huko.

Mh. Tundu Lissu tuzo uliyopewa tumia nafasi hiyo kuondoa aibu inayorudiwa rudiwa kila Mara kuwa chadema isichaguliwe kwa kuwa haina ofisi na wakipewa nchi watatumia Kodi za wananchi kujenga ofisi, japo najua hilo nalo watasema msiwachague hao kwa kuwa mkiwachagua watauza nchi kurudisha pesa walizo kopa kujenga ofisi.

Mh. Rais wa mioyo ya Watanzania tuzo yako ilete faida kwanza ndani ya chama kwa kujenga makao makuu ya chama ya kipekee ya kufunika jengo la CCM la Jakaya Kikwete Kule Dodoma.

Inawezekana hata kura tunaibiwa kwa vile tumekaa kiumasikini sana, tutumie sitofahamu iliyopo kati serikali na mabeberu kujinufaisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom