Tuzikatae propaganda za wanaccm, wanazodai kuwa watanzania chini ya asilimia 5 ndiyo wanaolipa kodi nchini!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,504
30,202
Kumekuwa na propaganda zinazoendelea, ambazo zinaongozwa na wanaccm, zinazodai kuwa watanzania wanaolipa kodi, eti ni kama milioni 3, ambapo ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wote milioni 60!

Mimi nazikataa propaganda hizo za wanaccm Kwa nguvu zote, Kwa kuwa watanzania wanakamuliwa Kodi kuliko nchi nyingi sana duniani!

Tukija Kwa upande wa "data" naweza kuzikana kabisa hizo propaganda zinazosambazwa na watawala hawa wa CCM, wanazodai kuwa watanzania wachache sana ndiyo wanaolipa kodi.

Niwaulize hao watawala wa CCM, hivi hizi Kodi zinazotozwa Kwenye miamala ya simu, ambazo Kwa taarifa zao TCRA, Kuna laini za simu karibu ya milioni 60, ambazo ni sawasawa na idadi ya watanzania wote, ambao Kila kukicha wanapambana na Makato ya Kodi, zokiwemo VAT ya asilimia 18 Kwa Kila muamala wa simu, hivi hizo siyo Kodi zinazoingia Kwenye hazina yetu ya Taifa??

Hivi hizi "data" wanazotoa hawa watawala wetu wa CCM, wanazitoa wapi??

Kwa kuwa Kwa "data" zangu ni kuwa Kila mtanzania analipa Kodi, tofauti na hizo propaganda wanazozieneza hao Wana CCM kuwa ni watanzania chini ya milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi hapa nchini
 
Kila Mtanzania analipa kodi/tozo/ushuru/unyang'anyi kila sekunde anayopumua.Hii ipo direct or indirect payments.Kila huduma apatayo mtu/mwananchi Mtanzania hulipa kodi. Ukinunua vocha,maandazi,bia,ukilipa nauli yoyote,chakula,kinywaji,huduma ya maliwato,nyumba ya wageni nk kote kuna kodi/tozo na unyang'anyi mtupu!Kuwaamini CCM na miuongouongo yao ni kujiunga na wendawazimu wanaofaidi mfumo wa kijambazi.
 
Kila Mtanzania analipa kodi/tozo/ushuru/unyang'anyi kila sekunde anayopumua.Hii ipo direct or indirect payments.Kila huduma apatayo mtu/mwananchi Mtanzania hulipa kodi. Ukinunua vocha,maandazi,bia,ukilipa nauli yoyote,chakula,kinywaji,huduma ya maliwato,nyumba ya wageni nk kote kuna kodi/tozo na unyang'anyi mtupu!
Sasa nawashangaa hawa watawala wetu wa CCM wanaodai kuwa watanzania walio wengi, eti hawalipi Kodi!

Je kwao "definition" ya Kodi ni ipi??

Wao waache waendekee kutukamua Ili waishi maisha ya starehe ya kuuendesha magari ya fahari ya ma- V8 lakini mwisho wao upo karibu sana, Kwa kuwa haya mateso wanayopitia watanzania, Kuna siku yatafika mwisho tuuu
 
Pengine wana tafsiri ya tofauti kwenye neno Kodi, lakini wasisahau Mo na Bakheresa sisi tunao nunua Nazi na sabuni zao za mia 5 ndio tunao sababisha walipe mabilioni au mamilioni ya kodi
 
Sasa,hapo wanalipa wao au tunachanga hela/kodi zetu na wao wanatuwakilisha kutuchukulia risiti tu?😂😂😂😂
 
Kumekuwa na propaganda zinazoendelea, ambazo zinaongozwa na wanaccm, zinazodai kuwa watanzania wanaolipa kodi, eti ni kama milioni 3, ambazo ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wote milioni 60!

Mimi nazikataa propaganda hizo za wanaccm Kwa nguvu zote, Kwa kuwa watanzania wanakamuliwa Kodi kuliko nchi nyingi sana duniani!

Tukija Kwa upande wa "data" naweza kuzikana kabisa hizo propaganda zinazosambazwa na watawala hawa wa CCM, wanazodai kuwa watanzania wachache sana ndiyo wanaolipa kodi.

Niwaulize hao watawala wa CCM, hivi hizi Kodi zinazotozwa Kwenye miamala ya simu, ambazo Kwa taarifa zao TCRA, Kuna laini za simu karibu ya milioni 60, ambazo ni sawasawa na idadi ya watanzania wote, ambao Kila kukicha wanapambana na Makato ya Kodi, zokiwemo VAT ya asilimia 18 Kwa Kila muamala wa simu, hivi hizo siyo Kodi zinazoingia Kwenye hazina yetu ya Taifa??

Hivi hizi "data" wanazotoa hawa watawala wetu wa CCM, wanazitoa wapi??

Kwa kuwa Kwa "data" zangu ni kuwa Kila mtanzania analipa Kodi, tofauti na hizo propaganda wanazozieneza hao Wana CCM kuwa ni watanzania chini ya milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi hapa nchini
swala la uelewa na ufahamu wa masuala ya kodi ni dhahiri liko chini ya wastani kwa kuzingatia tu, mfano wa mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji katika hoja hii mezani 🐒

nafurahi kuona wengi wanajipambanua kinagaubaga kwamba hawana uelewa wala ufahamu wa kutosha juu ya masuala mbalimbali ya kodi 🐒

Na huu utakua msingi au mwanzo muhimu sana, wa kuona kwamba ipo haja , sababu au ulazima wa somo la kodi kuwa ni la Lazima kuanzia chekechea, ili kuimpact nature ya kupenda kulipa kodi, kujenga msingi imara wa uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya kodi stahiki ambazo mlipakodi anawajibika kuzilipa, na sio hiki ambacho mnapeana matumaini ati ndio kodi 🐒
 
Mambo ya mawasiliano Yana alternative na sio sehemu kubwa inayotoa Mapato Kwa Serikali ukilinganisha na manunuzi ya bidhaa Moja kwa Moja ambapo naweza kukuonesha list ya biashara zinazotumiwa zaidi na ndio huko watu Hawalipi kodi.

Angalia hapa chini,hizi bidhaa bila kutoa na kudai risiti ni kazi bure Mapato yanapotea 👇👇

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1683735734795083776?t=xVqzpDitAcbQYKpXzTOkzQ&s=19

Just imagine bidhaa za Trilioni 36 ziliingizwa ndani kutoka Nje,Sasa kwenye manunuzi ya kawaida Serikali ilioata Kodi kiasi gani? Unakuta hata Trilioni 10 haijafika
 
Sasa wewe niambie, hiyo miamala ya simu ya Kila unapotoa pesa, unakatwa Kodi, hebu nipe tafsiri wewe "mjuaji" hiyo unaiita Nini??😎
 
Ma - CCM ni maongo sana aisee..

They are so strategic.

Ukiona Mbunge au wabunge wa CCM wanaropoka hivi ktk Bunge la bajeti, basi tambueni kuwa yanafagia njia ya kuiengenezea uhalali serikali kuingiza kodi zingine kandamizi na za maumivu kwenye bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na mamilioni ya wananchi wa kawaida.

Jiandaeni kwa bajeti ya kodi, Kodi, Kodi za maumivu.

Ni mwaka wa uchaguzi 2024 na 2025. CCM wanatafuta pesa za kampeni kupitisha vikaragosi wao kuwa viongozi wetu.

Just imagine, kuwa, Mbunge mtu mzima anasimama bungeni ndani ya chombo muhimu Cha kuishauri na kuielekeza serikali kwa niaba ya wananchi ifanye mambo yake kwa manufaa ya wananchi hawa, badala yake Mbunge huyu anakuwa source ya ukandamizaji wa wananchi waliomtuma, anasimama na kuropoka tu mambo pasipo kufanya utafiti wa kina kabla ya kusema.

Na inashangaza kuwa, serikali huchukua mawazo ya wajinga kama hawa na kuyafanyia kazi na matokeo yake huleta vurugu na mikinzano na malalamiko ktk jamii kiasi cha baadaye wabunge wenyewe Hawa kujiuliza: Tulipitishaje hiki kitu? Tulikuwa tumelala au tunasinzia?

Hapa Tanganyika kila mtu analipa Kodi. Hata mimba (watoto wakiwa bado tumboni) wanalipa kodi.

Tunatofautiana viwango tu vya kodi kulingana na tofauti ya vipato na hali ya uchumi ya mtu mmoja mmoja.

Na kanuni ya kodi inataka hivyo. Kuwa mwenye kipato kikubwa analipa zaidi ya mwenye kipato kidogo. Lakini Tanganyika ni tofauti. Wenye kipato ndio wakwepa Kodi wakubwa. Wasio nacho/wenye kipato kidogo wanakamuliwa hadi damu kulipa Kodi zao.

Na kusema kuwa Watanganganyika hatulipi kodi kama Marekani au ni asilimia 6 pekee ya Watanganganyika ndio wanalipa Kodi, huo ni uongo wa mchana kweupe.

Mfano VAT iko kwenye kila bidhaa na huduma inayotumiwa na mwanadamu, utasemaje watu hawalipi kodi?

Kodi za laini za Simu, LUKU METER, mafuta ya petrol ambapo hata kama mtu hana gari au pikipiki au chombo Cha moto, basi atakutana na kodi hiyo kwenye kwenye huduma ya usafiri na usafirishaji (nauli).

Huyu Mbunge Elibariki Kingu ni mwongo na hajafanya utafiti wake vyema. Apuuzwe tu..

Infact katika nchi ambayo watu wake wanatozwa kodi nyingi na kubwakubwa lakini pasipo kuona matunda ya kodi zao hizo ktk viwango vinavyotakiwa katika huduma wanazopatiwa na serikali yao, basi nchi hiyo ni Tanganyika.

Huko Marekani na nchi zingine zilizokwisha kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi ni kweli wanalipa kodi. Lakini tofauti yao na sisi ni kuwa, watu wanaona kwa uwazi matunda ya kodi zao. Hakuna viongozi kula au kuiba pesa za walipa Kodi na kuachwa free wakitamba na kufurahia utajiri wa wuzi. Vipi hapa Tanganyika?

Na sababu ya hiyo👆👆ni UFISADI na RUSHWA. Kwamba pesa nyingi za Kodi huibiwa na viongozi wa CCM kwa kushirikiana na matajiri wao wachache. Na huachwa wakitamba tu mitaani kulingishia watu.

Na ukiona kauli za wabunge wa dizaini ya Elibariki Kingu zikitangulia ktk kipindi hiki cha Bunge la bajeti, basi tambueni kuwa ni maandalizi ya kuingizwa kwa kodi mpya za maumivu kwa wananchi kwenye bidhaa na huduma muhimu zinazotumiwa na mamilioni ya watu kama umeme, simu, mafuta ya petrol nk huku serikali ikiacha eneo muhimu la Maliasili (natural resources) kama misitu, madini, bandari nk ambalo ndilo linalopaswa kuingiza mapato makubwa ya nchi pasipo kumbagaza mwananchi masikini yakiachwa mikononi mwa matajiri wa dunia bure kabisa.
 
Sasa wewe niambie, hiyo miamala ya simu ya Kila unapotoa pesa, unakatwa Kodi, hebu nipe tafsiri wewe "mjuaji" hiyo unaiita Nini??😎
nachelea kusisitiza ndugu mtoa hoja kwamba, bado unajipambanua ya kwamba, uelewa na ufahamu juu ya masula ya kodi bado ni chini ya wastani. ntawasanua wauhusika na bila shaka watafanya namna katika kukumbusha mara kwa mara juu jambo ya hili muhimu sana kwa jamii na ustawi wa Taifa letu 🐒
 
Pengine wana tafsiri ya tofauti kwenye neno Kodi, lakini wasisahau Mo na Bakheresa sisi tunao nunua Nazi na sabuni zao za mia 5 ndio tunao sababisha walipe mabilioni au mamilioni ya kodi
Kodi hulipwa na walalahoi, viongozi na wafanyabiashara wakubwa ni walaji wa jasho la walipa Kodi au kwa maneno rahisi ni wanyonyaji waliohalalishwa kisheria.
Wasipokuwepo walalahoi viongozi watakufa njaa (kodi itakosekana).
 
Kumekuwa na propaganda zinazoendelea, ambazo zinaongozwa na wanaccm, zinazodai kuwa watanzania wanaolipa kodi, eti ni kama milioni 3, ambazo ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wote milioni 60!

Mimi nazikataa propaganda hizo za wanaccm Kwa nguvu zote, Kwa kuwa watanzania wanakamuliwa Kodi kuliko nchi nyingi sana duniani!

Tukija Kwa upande wa "data" naweza kuzikana kabisa hizo propaganda zinazosambazwa na watawala hawa wa CCM, wanazodai kuwa watanzania wachache sana ndiyo wanaolipa kodi.

Niwaulize hao watawala wa CCM, hivi hizi Kodi zinazotozwa Kwenye miamala ya simu, ambazo Kwa taarifa zao TCRA, Kuna laini za simu karibu ya milioni 60, ambazo ni sawasawa na idadi ya watanzania wote, ambao Kila kukicha wanapambana na Makato ya Kodi, zokiwemo VAT ya asilimia 18 Kwa Kila muamala wa simu, hivi hizo siyo Kodi zinazoingia Kwenye hazina yetu ya Taifa??

Hivi hizi "data" wanazotoa hawa watawala wetu wa CCM, wanazitoa wapi??

Kwa kuwa Kwa "data" zangu ni kuwa Kila mtanzania analipa Kodi, tofauti na hizo propaganda wanazozieneza hao Wana CCM kuwa ni watanzania chini ya milioni 3 ndiyo wanaolipa kodi hapa nchini
Unajua maana "Kodi" au unajua tu kuanzisha nyuzi hata kwa jambo usilolijua?
 
Mambo ya mawasiliano Yana alternative na sio sehemu kubwa inayotoa Mapato Kwa Serikali ukilinganisha na manunuzi ya bidhaa Moja kwa Moja ambapo naweza kukuonesha list ya biashara zinazotumiwa zaidi na ndio huko watu Hawalipi kodi.

Angalia hapa chini,hizi bidhaa bila kutoa na kudai risiti ni kazi bure Mapato yanapotea 👇👇

View: https://twitter.com/TheChanzo/status/1683735734795083776?t=xVqzpDitAcbQYKpXzTOkzQ&s=19

Just imagine bidhaa za Trilioni 36 ziliingizwa ndani kutoka Nje,Sasa kwenye manunuzi ya kawaida Serikali ilioata Kodi kiasi gani? Unakuta hata Trilioni 10 haijafika

Hapo kwenye mafuta karibu kila siku nanunua mafuta na mashine zinatoa risiti
Karibu kila siku nafanya miamala ya kutuma, kutoa, na kulipa na huko nakatwa kodi moja kwa moja iwe ndogo au kubwa lakini nalipa kodi.

Sasa iweje mbunge asimame bungeni asema watanzania mil 3 tu ndio wanalipa kodi.
 
Back
Top Bottom