Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,210
Reaction score
23,255
Kuna watu hawapendi ujirani wa amani kabisa. Na kundi hili la majirani wagomvi ni kubwa sana kuliko tudhaniavyo!

Binafsi ugomvi mkubwa na jirani yangu ilikuwa ni kwenye kununua Umeme. Huyo umeme ukiisha tu alikuwa hawashi taa na hapandishi mapazia anajifungia kimya!

Tulikalishwa vikao hadi vya mjumbe lakini wapi! Ikabidi nihamie nyumba nyingine! Huku nako nilikutana na mama mmoja jirani mchafu hatari, watoto wake walikuwa wanajisaidia kwenye corridor! Halafu hajali wala nini, ukiweka kanyagio la kufutia miguu ukitoka baadae unarudi unakuta wamelichukua wao kufutia miguu!

Nikadhani mtu aliyejenga hana kero ya ugomvi na majirani kumbe huku ndiko kuna balaa zaidi! Huku nako kuna watata vilevile, usipoangalia unaweza pata presha. Wapo majirani mabingwa wa kusogeza mipaka ya viwanja! Huu ugomvi ni mwingi sana umeharibu mahusiano ya majirani wengi sana!

Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!

Yote tisa, wapo majirani wafugaji wenye mifugo inayoharibu mali za jirani yake na wala hawajali.

Nisiseme mengi. Leo Naomba tushirikishane, ni mgogoro gani hasa ulionao wewe na jirani yako hapo?
 
Majirani zangu ni kitoweo changu.

images%20(13).jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majirani zangu wawili ni wakorofi sana lakin sijawahi kugombana nao hua nawaacha tu

Wakwanza huyu nilipovuta maji kwa gharama zangu kutoka mtaa wa pili na yeye akaombe aunge tela nikakubali kiroho safi , ikafikia kipindi akashindwa kulipa bill akakatiwa maji kwa hasira zake alichukua jembe na kukata ile pipe inayoleta maji home kwamba tukose wote.

Wapili yupo nyuma yangu jamaa ni mkuria mbabe sana, kiburi , fedhuri maruhuni kabisa anaweza kuangua nazi kwake zinakuja kugonga katika bati home na aombi radhi.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Majirani zangu wawili ni wakorofi sana lakin sijawahi kugombana nao hua nawaacha tuu,
Wakwanza huyu nilipovuta maji kwa gharama zangu kutoka mtaa wa pili na yeye akaombe aunge tela nikakubali kiroho safi , ikafikia kipindi akashindwa kulipa bill akakatiwa maji kwa hasira zake alichukua jembe na kukata ile pipe inayoleta maji home kwamba tukose wote...
Wapili yupo nyuma yangu jamaa ni mkuria mbabe sana, kiburi , fedhuri maruhuni kabisa anaweza kuangua nazi kwake zinakuja kugonga katika bati home na aombi radhi

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Aisee pole sana
 
Jirani kanizibia njia ya kupitisha gari langu. Nimetoka asubuhi narudi jioni nakuta bonge la fence ukuta umepanda kozi 6. Tangu siku hiyo sina hamu nae, nikaongea na jirani wa pembeni akaniuzia njia TZS 1,000,000/= ndiko napitisha gari yangu siku hizi. Sasa kuna ujirani hapo
 
"Unapopata shida usiku wa manane ,jirani yako ndio wa kwanza kukusaidia ,hata vitabu vya Mungu viliandika mpende jirani yako kama unavyojipenda,Jirani yako ndio nduguyo" - African Stars - Jirani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom