Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Jirani kanizibia njia ya kupitisha gari langu. Nimetoka asubuhi narudi jioni nakuta bonge la fence ukuta umepanda kozi 6. Tangu siku hiyo sina hamu nae, nikaongea na jirani wa pembeni akaniuzia njia TZS 1,000,000/= ndiko napitisha gari yangu siku hizi. Sasa kuna ujirani hapo
Hiyo njia ilikuwa kwenye kiwanja chake au, ulimpa hela akagoma?
 
Hiyo njia ilikuwa kwenye kiwanja chake au, ulimpa hela akagoma?
Njia haikuwa kiwanja chake. Ni njia ilitengwa na uongozi kwamba watu tuchangie hatua kadhaa kila mmoja. Sasa kwakuwa kanizibia mimi na wengine wengi wa nyuma yangu ikanibidi nimuombe jirani yangu mwingine wa mbele yangu aniuzie barabara ndipo nipate kupita.
 
Mi jirani yangu ananisumbua kwa kitu kidogooo ila kinanitesa.napenda chai ya mchai chai...kila napo panda mchai chai yeye hua anaukata haukui kabisaa.nimeshajaribu kupanda mchai chai zaidi ya miaka minne haikuii hata kidogo. Shida ni kua hata sitawai kumkamata maake ninapotoka kwenda kazini yeye ndo hukata,yani sitawai mushika akiukata.mwaka wa tatu huu sisemeshani nae
 
Mi jirani yangu ananisumbua kwa kitu kidogooo ila kinanitesa.napenda chai ya mchai chai...kila napo panda mchai chai yeye hua anaukata haukui kabisaa.nimeshajaribu kupanda mchai chai zaidi ya miaka minne haikuii hata kidogo.shida ni kua hata sitawai kumkamata maake ninapotoka kwenda kazini yeye ndo hukata,yani sitawai mushika akiukata.mwaka wa tatu huu sisemeshani nae
Sasa kwann anaukata au unapanda kwenye eneo lake?
 
Wakati nanunua kiwanja,huyujirani alikuwepo na muuzaji akaniambia njia hiihapa kwa jirani nayeye yupo hapohapo anasikia.

Ila palikuwa na shimo kwenye eneo alilo nionyesha njia.
Jirani kwa kauliyake akaniambia nifukie shimo nipate njia nikaagiza roli la kifusi nikafukia shimo.
Nikampa na pesa kama laki na sabini hivi mana alikuwa kama hatakiela anajifanya ni ujurani mwema.

Baada ya miaka kama miili akauza kiwanja eneo la mpakani kwenye njia, aliemuzia akajenga mbaka akamaliza njia, wife akanipigia cm nikiwa kazini akaniambia njia inazibwa sikuamini.

Nikaomba ruhusa fasta kufika home nakutakweli mafundi wapo kozi ya nne.

Daaah jasho likanitoka nikamuita jamaa pale kwenye ujenzi na mnunuzi akiwepo nikamuuliza vp jirani mbona unazibanjiatena.

Akasema alisahau kumuambia aliemuuzia kwamba aache njia.

Mwisho wakakubali kuniachia kama futi 5 hivi kwa masharti kwamba niwalipe mafundi kuvunja ukutauliozidi, ninunue sement na kulipa mafundi kujenga upya nikalipa pesa tena waka vunja.

Baada ya miezi kadhaa tena huyu jirani alienunua akapanda mnazi na mpapai kwenye njia.

Yani siwezi kuelezaninavyo wachukia hawa jamaa.

Nikaamua kununua kiwanja kingine nakujenga sasa nasubiri umeme tu nihamie huko mana hapa gari haiingii.
Upande mwingine kwenye mpaka kuna kinjia kidogo ambacho nirahisi kufika maeneo ya madukani na hospitali, chaajabu wao wanapita kilasiku kwenye njia niliyoacha mimi hapa kwangu najiuliza sipatijibu.
 
Kero yangu nilinunua kiwanja jirani niliyepakana naye alikua amezungushia eneo lake fens baada mda akaongeza tofali ile fensi akafanya nyumba alipopauwa maji yanamwagikia kwangu nilimtuma balozi akadai alikua kazini hivyo mafundi walikosea maagizo nilimsamehe nikamwambia afunge gata na asirudie tena.
 
Mkorofi tu fundi hawezi kufanya tofaut
 
Nakaa kwangu jiran anakaa kwake kila familia inatoka geti lake na kwenda kazin kurud jion
Weekend tunashinda na familia zetu huyo jiran tunakutana wap?

Mimi majiran nilionana nao wakat nahamia hapa kwangu miaka mingi iliyopita nilipokuwanatambulishwa

Baada ya hapo tumekuwatukikutana kwenye misiba ya hapa karb tu

Wengine hata siwajui
 
Sasa kwann anaukata au unapanda kwenye eneo lake?
Eneo sio lake.eneo ni LA baba yangu na Mimi nasimamia ufyatuaji na uuzaji wa Tofali afu kuna ufugaji Nguruwe pemben kwahio Niko nasimamia kazi za Mzee wangu.huyu mama anaekata mchai chai ni Mke wa huyu Jamaa anaelisha na kufanyia usafi Nguruwe wetu.yani basi tu sijui anafanyaga kunikomoa tu make sinaga story nae wala hata salamu hatupeani....ila kila akiona mchai mchai wangu anaukata tuu.yani haka ka mwanamke sijui nikafanye nn.yani ninapoishi kuna ardhi Kubwa sanaaaa tena kuna mbolea nyingi ila mchai mchai haujawai kukua.
 
Mimi kuna jirani alishirikiana na watu wa ardhi kumega kiwanja changu niliuwasha moto balaa mpaka wakakirekebisha, toka kipindi hicho sina time nae.
 
Eneo sio lake.eneo ni LA baba yangu na Mimi nasimamia ufyatuaji na uuzaji wa Tofali afu kuna ufugaji Nguruwe pemben kwahio Niko nasimamia kazi za Mzee wangu.huyu mama anaekata mchai chai ni Mke wa huyu Jamaa anaelisha na kufanyia usafi Nguruwe wetu.yani basi tu sijui anafanyaga kunikomoa tu make sinaga story nae wala hata salamu hatupeani....ila kila akiona mchai mchai wangu anaukata tuu.yani haka ka mwanamke sijui nikafanye nn.yani ninapoishi kuna ardhi Kubwa sanaaaa tena kuna mbolea nyingi ila mchai mchai haujawai kukua.
Nakupa mbinu, tafuta zile shanga za waganga halafu panda huo mchaichai, zungusha vijiti vya miti pembeni au tairi kuulinda then weka shanga hiyo na pia tengeneza kipande cha nguo nyeusi iwe kama hirizi nyeusi then itundike hapo pembeni!
Wakati wa kupanda huo chaichai upande usiku!
Huo lazima ustawi
 
Kwakweli kero nyingi zipo kwenye maeneo yasiyopimwa. ukiweza nunua kiwanja kilichopimwa au nunua hlf pimisha fasta uwe na impala yako. hii inasaidia kupunguza baadhi ya kero km za majirani kuingia kiwanja chako, njia ya kutokea, wapi maji yapite.

Jengine nunua sehemu ambayo hali yako ya kiuchumi, kijamii n.k inaendana na hao unaowakuta hapo vinginevo utajutra.
 
Eneo sio lake.eneo ni LA baba yangu na Mimi nasimamia ufyatuaji na uuzaji wa Tofali afu kuna ufugaji Nguruwe pemben kwahio Niko nasimamia kazi za Mzee wangu.huyu mama anaekata mchai chai ni Mke wa huyu Jamaa anaelisha na kufanyia usafi Nguruwe wetu.yani basi tu sijui anafanyaga kunikomoa tu make sinaga story nae wala hata salamu hatupeani....ila kila akiona mchai mchai wangu anaukata tuu.yani haka ka mwanamke sijui nikafanye nn.yani ninapoishi kuna ardhi Kubwa sanaaaa tena kuna mbolea nyingi ila mchai mchai haujawai kukua.
Huu nimeupanda miezi sita nyuma.hapa vimetokeza majani wiki hii kwakua nimeshinda hapa karibu nusu Siku kwa wiki nzima
Najua anaumezea mate akate majani yaliyokua na akikata unadumaa.yani haka ka mama badala kaache mchai mchai utoe majani mengi ata ukiuchuma unaendelea kubaki
Hapo nikitoka tu aaaah ntarudi na picha ya utakavoonekana ukikatwa.huyu mama matako ya nyoka kabisaa
1616734814021-1989468728.jpg

Nakupa mbinu, tafuta zile shanga za waganga halafu panda huo mchaichai, zungusha vijiti vya miti pembeni au tairi kuulinda then weka shanga hiyo na pia tengeneza kipande cha nguo nyeusi iwe kama hirizi nyeusi then itundike hapo pembeni!
Wakati wa kupanda huo chaichai upande usiku!
Huo lazima ustawi
Duh mkuu hio ni noma.hapo si watu watajua mi mchawi na hapa wanakuja vijana karibu nane kila Siku kupiga kazi.kuna jirani alinishauri niumwagie Maji ya mchele ili majani yawe na rangi nyeupe kama yametemewa mate yenye dawa ya mswaki....
 
Huu nimeupanda miezi sita nyuma.hapa vimetokeza majani wiki hii kwakua nimeshinda hapa karibu nusu Siku kwa wiki nzima
Najua anaumezea mate akate majani yaliyokua na akikata unadumaa.yani haka ka mama badala kaache mchai mchai utoe majani mengi ata ukiuchuma unaendelea kubaki
Hapo nikitoka tu aaaah ntarudi na picha ya utakavoonekana ukikatwa.huyu mama matako ya nyoka kabisaa
View attachment 1734614

Duh mkuu hio ni noma.hapo si watu watajua mi mchawi na hapa wanakuja vijana karibu nane kila Siku kupiga kazi.kuna jirani alinishauri niumwagie Maji ya mchele ili majani yawe na rangi nyeupe kama yametemewa mate yenye dawa ya mswaki....
Usiogope watu, wafanye watu wakuogope wewe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom