Kenya ni sawa na banda la uani la Tanzania

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
KENYA NI BANDA LA UANI KATIKA TANZANIA

Leo 10:30am 01/08/2020

Kenya ni sawa na banda la uani la Tanzania,Kenya anapofunga mpaka wake wowote na Tanzania,maana yake anajifungia njia yeye mwenyewe kupita nyumba kubwa na kwenda kujitafutia mahitaji yake,Kenya anahitaji chakula toka Tanzania, Kenya anahitaji kupita Tanzania kuleta Watalii wake Mlima Kilimanjaro baada ya kuutangaza Mlima Kilimanjaro na watalii kushukia Kenya.

Naijua Kenya, nimemaliza darasa la nane pale Muguga High School miaka 1998. Niseme sasa tena tukiwa na JPM hakuna tena tunalotegemea Kenya kusema kuwa tutaathirika sana ikiwa sote tutaamua kuuonesha uanaume. Kenya anaitegemea mno Tanzania kuendesha maisha ya Wananchi wake. Kenya haina tena eneo la soko wala Uwekezaji,mfumo wao wa kibepari umewaruhusu watu wachache kuimiliki ardhi yote ya Kenya na kuwaacha Wananchi wa Kenya kuwatumikia mabepari wachache.

80% ya nchi ya Kenya haizalishi chakula wanaitegemea sana Tanzania. Hivi jamani kuna bidhaa, kubwa kuliko misosi
Kenya imekuwa ikinunua mahindi, mchele, viazi, vitunguu, nyanya kutoka Tanzania. Uwepo wa soko na Viwanda vya mazao ya kilimo mfano pale Longido, kumewanufaisha wakulima na Wafanyabiashara wote wa Kenya na Tanzania.

Wananchi wa Kenya hawana tofauti na Wananchi wa China, hawawezi tena kuendesha maisha yao kwa kutegemea ardhi yao ya Kenya, ni lazima watoke ili wakatafute nje ya Kenya. Tanzania ndio kimbilio lao baada ya mabepari kuinunua Kenya yenye kilomita za mraba laki tano, hivyo kusababisha Wakenya kukosa ardhi na kubaki makupe kutumikia mabepari ndani ya nchi yao.

Tanzania ina kilomita za mraba laki tisa na nusu huku kilomita za mraba laki tatu zikiwa bado bikira kwa maana hazijatumiwa zikiwa bado ni pori la akiba na eneo ambalo tukilima tunaweza kuilisha Afrika yote, hivyo hivyo kwa population ya watu ya Milioni sitini tofauti na population ya Kenya ya watu Milioni hamsini na mbili bado Tanzania ni soko na sehemu ya kuwekeza kwa maana ya place of investment.

Wakenya wengi wanafurahi kuja kuishi Tanzania,Furaha ni kuja kuishi kifalme hapa Tanzania huku wakiigeuza Tanzania kuwa koloni lao. Actually, wao ndio lead investors hapa Tanzania cha ajabu hata kupaka rangi jengo basi fundi lazima atoke Kenya kuja kupaka rangi jengo walilokodi hapa Tanzania, wanaongoza kwa kuhonga ili wapate kuishi Tanzania, Wakenya wengi muda wao ukiisha wanajificha jificha mitaani, hawataki kurudi kwao, adabu hawana wanapenda kuishi Tanzania lakini wanadharau Watanzania.

Yes,Watanzania ni wapole sana kutokana na malezi ya Ujamaa kupitia sera ya Mwalimu Julius Nyerere. Watanzania ni wapole kwa sababu tumezoea kuwakarimu wageni wote wajao Tanzania, Tanzania imekuwa nyumbani kwa kila Taifa la Afrika tangu wakati wa kupigania Uhuru,lakini isiwe mgeni akifika akiona kilomita za mraba laki tatu ziko tupu aanze kununua kupitia watu, hapana.

Mwalimu Nyerere alitenga eneo hilo kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu,kitu ambacho Kenyatta alishindwa kufanya kwa Wakenya, vivyo hivyo Mwalimu Nyerere alitunza madini hadi tupatapo akili, na leo Rais Magufuli ametupa akili na tumemuona mtanzania Ndugu Saniniu Laizer akiwa bilionea wa kwanza kutokana na madini yetu.

Yes, Watanzania ni wapole wamelelewa Kijamaa na si kibepari. Naomba upole wa Watanzania sasa ubadilike kwa maana kwa muda mrefu Wakenya wametumia upole wetu kututawala na kutupanda kichwani. Napenda upole wetu uwe kwenye undugu na jirani zetu, jirani yetu anapobadilika na kuwa mtu unayeweza kula mtu mwenzie basi Watanzania tubadilike hata ikiwezekana kumpiga kwa maneno tu kumshikisha adabu kama ilivyomshikisha adabu Nduli Iddi Amini.

Kwenye vita ya maneno tunaweza kuwatumia Wazaramo na Waluguru tu,Niseme tu Tanzania haihitaji Kenya kama Kenya inavyohiitaji Tanzania, We don't need them at all. Baada ya wao kupanga vikosi uchumi katika anga, radar zimeona na tayari tumedhibiti, na sisi kwa tahadhari hiyo hiyo, tukiwa makini sana kutokusababisha capita damage, napendekeza mara moja twende na infantry, vikosi uchumi vya ardhini vifanye kazi usawa wa mipaka yetu kulinda Uchumi wetu na Wananchi ambao wanawauzia chakula Wakenya hadi Corona iishe Kenya.

Niwaambie Wakenya ya kwamba Tanzania si wepesi kama wanavyodhani, kidiplomasia Tanzania inaongoza sana ndio maana tumekuwa nyumbani kwa kila Mwafrika, Kiintelijensia Tanzania is very smart, Kivita ni Wakongwe, muulizeni Nduli Iddi Amini Dada. Sasa mkifanya fuu sisi tutafanya fwaaa, mnaonaje tukifunga biashara zenu zote hapa Tanzania, Mabenki yenu NBC iyanunue na kufanya branch zake, Hakuna kuuza wala kununua. Inawezekana katika biashara tunazowaruhusu wafanye huku Tanzania wakatufanyia hata hujuma ili kuonesha kuwa Tanzania kuna maambukizi makubwa ya Corona na kusababisha uchumi wetu kuyumba.

Heshima haiji isipokuwa kwa kujiheshimu kwanza. Wakenya wameongea sana, wametuponda sana kwa dharau miaka nenda rudi sisi tumekuwa kimya tu. Sasa ufike wakati waelewe kuwa hata bubu kuna hatua akifika anaweza tamka maneno machache, kwa wale Watanzania wanaodhani wao wana Ukenya mwingi ndani yao basi wahamie Kenya tu, maana kuna wapuuzi ambao wanapenda sana kujipendekeza mataifa mengine.

Kiuchumi Tanzania si wachanga ndio maana hivi leo kila Mkenya anataka kuja kuwekeza Tanzania. Sasa Niwaambie tusifatane fatane. Tanzania ndio taifa baba, taifa ambalo liliwahi kutoa ndege yake kubwa kuacha safari za biashara na kupeleka Jeshi la Wananchi wa Tanzania,kwenda kuikomboa Msumbiji toka kwa Mkoloni. Tanzania imekuwa nchi ya diplomasia sana na kusababisha kujiumiza, ndio diplomasia zimeumiza nchi hii sana wakati wenzetu wakiweka jeuri na sura ya kazi. Sasa hapana; you do me I do you, simple.

Watanzania tumekuwa na huruma na majirani zetu na Afrika nzima kwa ujumla,Kenya hawana hii huruma tuliyokuwa nayo. Wakenya wako kwa ajili ya Kenya Kwanza halafu Tanzania baadaye. Wakenya katika akili zao jinsi wanavyoongea Kiingereza wanajiona Tanzania kama koloni lao wakati media za Kenya zikitangaza kwa mbwembwe watu watakaoingia nchini kwao bila kutaja Watanzania walidhani mahusiani yataendelea kuwa sawa. All of this its because of that drunkard spoiled kid aliyekulia Ikulu na kuja kuwa Rais, anatikisa kiberiti bila kucheck situation ya pande zote akijua yeye anaitegemea sana Tanzania. Kila akisikia kauli kuwa mikopo ya China, mikopo ya corona yeye ulewa na kwenda kuisaini huku akitaka Jirani wam-support.

Bado tupo kwenye domination ya mzungu!
Ni wao ndio waliokata mipaka ya nchi huku Afrika! Ninyi vichwa panzi mmelisahau hilo na kuwa waenda hovyo! Niliwauliza mara ya kwanza Uhuru alipotangaza kufunga mpaka,mnajua maana yake? na athari zake hasa kwake yeye Uhuru na Kenya yake. Mimi naiamini Serikali yangu ya Tanzania na Rais wangu John Magufuli kwa sababu nnazozijua Mimi! na kamwe hatutakaa tudharauliwe na watu wanaotutegemea sisi hata kwa chakula, wengi hawaelewi kuwa kuna vita za maneno tu na zinatosha kushusha hadhi ya nchi pamoja na uchumi!

Tunaendelea kurekebishana na kwa baadhi ambao wanaona kila kitu kitakachofanywa na serikali huwa wanaona serikali inawaonea waendelee kuvumilia tunapoendelea kulinda heshima yetu na kuitokomeza dharau. Watanzania ni baba lao, ukitazama Burundi mpaka sasa mafuta ya kupikia wanaimport toka Kigoma, unga unatoka Kigoma, Rwanda hiyo mbali na kuipora Congo, hakuna walicho nacho kabisa maana kama Ng'ombe sisi ndio wazalishaji wakubwa Afrika Mashariki na pengine Afrika nzima.

Uganda kidogo ndio tunaenda nao sambamba ila bado hawatukuti kwa madini,Sasa turudi Kenya mpaka mbao na nguzo za umeme bila Tanzania wanawasha koroboi. Leo hii wanajitangaza na Mlima wetu wa Kilimanjaro, yaani hawana kitu cha kujivunia ni kuibia ibia tu na kuishi kimkanda mkanda,Naipenda Tanzania na ninajivunia kuwa Mtanzania kweli kweli. Kenya wanajionaga wao ni special sana, wazungu weusi, na Tanzania wanaionaga kama koloni lao, kwa JPM hiyo stop. Wakenya mtapapaswa kila kona, hadi mseme poo!

Kenya wanavyo tu treat wanaonyesha hawapo tayari kwa mazungumzo, wao wapo katika harakati za kuharibu na kuhujumu uchumi wa Tanzania, maana Tanzania inapiga indiketa kuupita Uchumi wa Kenya. Kiuchumi Kenya wanajua wanachofanya siyo kwamba hawajui, tutazungumza vizuri baada ya kuwa tumebanana mbavu kisawa sawa, hapo tutakuja jadiliana kwa heshima. Nchi hizi si lazima ziwe na urafiki. Kenya kakataa Urais kitambo tu toka ilipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuteka ndege, treni na Mali zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizokuwa Nairobi badala ya kugawa Mali kwa kila aliyekuwa mwanachama.

Kuna Mkenya anasema mbona KQ pekee, si mungefungia hata Jambo Jet ambayo ni mtoto 100% wa KQ, pia precision air ambayo ni 50% mtoto wa KQ? Yaani hapo hakuna kazi imefanyika ni vitisho tu. Hata mufungie KQ na Jambo Jet bado KQ itapata pesa kupitia Precision Air. Nikujibu tu Jambo Jet haifiki Tanzania, haina kibali cha kuja Tanzania, shirika Pekee la Kenya linalofika Tanzania ni KQ,

Hii ni warm up bado kazi yenyewe haiwezekani wazuie ndege zetu kwa sababu ya corona halafu za kwao zinakuja kana kwamba zenyewe haziwezi kuambukizwa hiyo corona,hilo ni pigo kubwa sana kwa KQ kupoteza International Airports 3 kwa mpigo, kuanzia Jumatatu utasikia vilio toka Kenya,KQ ina operate 5 flights per day,v32 flights week and 128 flights per month in Dar only achana na znz and KIA kwahiyo wao wanajua watapoteza revenue kubwa compared to Entebbe and Kigali.

Inabidi serikali iende mbele zaidi kwa kupiga marufuku takataka zote zinazoingia kutoka Kenya bidhaa na raia. Ukikutwa na chochote "Made in Kenya" au kimethibitishwa na KEBS ni uhujumu uchumi, na hii sheria isiishie tu kipindi hiki cha mpito, Viongozi waape kuilinda kama ilivyo kwenye kuulinda Muungano,Newton's 3rd Law of motion on a straight line inahitaji amendment. ACTION AND REACTION hazipaswi kuwa equal.

Baada ya Kenya kukataza ndege za Tanzania kutua Kenya, nasi kwa lugha ya beberu tunasema: Due to the persistence of the corona epidemic in Kenya where it is clear that the Kenyan government has failed to control it so the Tanzanian government has decided to use discretion not to allow any flights from Kenya, Nairobi or Mombasa even kisumu especially for airlines that transport passengers from Kenya such as KQ Jambo jet and even Precision air this implementation will involve the transportation of passengers in those airlines that plan to transport passengers to our airports especially Dar es Salaam, Kilimanjaro and Arusha as well as Mwanza. This ban officially starts today 01 -08-2020.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Leslie Oscar Mbena classmate wa SPS nimesoma vizuri andiko lako na pia nimesoma comment za watu kuhusu andiko lako.Thanks niishie hapo kwa leo.
 
Nyie ndiyo wenye PhD halafu mko Lumumba mnalipwa laki 5 kwa miaka lukuki mkisubiri uteuzi. Kazi yako kuandika utopolo huu.

Na PhD yako umeshindwa kujiajiri. Siku ukipewa cheo unaanza kusisitiza wahitimu wajiajiri
 
Tusiangalie itikadi zetu, tujiunge kwa pamoja kumsaidia kamanda Lissu tumpe Nchi ipige spana .

Tupate nchi yenye mifumo mizuri ya sheria hata ikitokea wewe unakua Rais utaweza kutuongoza bila shida hata ikita Kenya iwe frem ya mbele ya Nyumba itakua tumalize moja kwanza Tumpe Nchi .
 
CCM na serikali yenu kama mnaweza anzisheni vita kamili na Kienya, siyo mnakalia kumbwela mbwera tuu kelele zenu tumezichoka.
 
Unaweka educational background yako Ili uteuliwe?
All in all muathirika mkubwa wa huu mgogoro Ni Precision Airways PW ambaye yeye ana Safari za Kenya.
ATCL hana Cha kupoteza kwasababu hana biashara Kenya.
Sio kila upuuzi wa Kabudi macho ya bundi tuunge mkono.
Muathirika ni KQ anayeleta ndege DAR, JRO na ZNZ kila siku
 
Museveni alisema Kenya na Tanzania ni sebule za Nyumba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uganda , Rwanda na kadhalika ni vyumba vya jumuiya hiyo. Na alitumia mfano huo kwa nia njema tu wakati wa harakati za kukabiliana na Corona.
===
Nimeandika maelezo hayo hapo juu kwa kusoma kichwa cha habari cha uzi huu. Sasa ngoja nirudi nisome posti ya kwanza ya uzi huu kwa makini.
 
..tuache SIASA.

..wananchi wa kule mipaka wanachotaka ni kufanya BIASHARA.

..Wakenya ni wateja wa bidhaa zetu za viwandani au mashambani.

..ndio majirani wenye uwezo wa kiuchumi kuliko majirani zetu wote.

..tujielekeze zaidi kwenye kukuza BIASHARA na Kenya.

NB:

..nilisikitika kuona waTz wanahangaika kwasababu bidhaa zao zimekwama baada ya Mkuu wa mkoa kufunga mpaka na Kenya.

..tunapo-deal na Wakenya tujaribu kuhakikisha hatuumizi wa-Tz wenzetu.

..hakuna nchi inapenda kuwa na jirani masikini au mwenye matatizo na migogoro.
 
Asante mkuu.
Umeongea kwa hisia sana, Naunga mkono hoja zako kwa maslahi ya nchi na wananchi wa Tanzania.
Kenya si lolote kwetu.
 
Nawaomba wanaosoma andiko hili waelewe kuwa yaliyoandikwa ni maoni ya mwandishi mwenyewe sio ya watanzania.

Sisi tunaamini katika ushirikiano na majirani kwa sababu mahitaji yetu mhimu yanafanana.

Kama tunatofautiana katika mambo Fulani tunauwezo wa kuyamaliza kwa ungwaana sio kujimwambafay kama mwandishi alivyofanya.

Mbona sisi tulichoma kuku wao? Je walionyesha vitisho kwetu?

Je tulishindwa kuzungumza au kuwarudisha kwao? Mungu alitupa akili na hekima ili tuzitumie kuelewana
 
MK254 huyu Mtanzania amepigwa sana na Watanzania wenzake kwa kuandika kuwa TZ inastahili kuendeleza migogoro na Kenya. Aisee kumbe Watanzania wengi humu Jf ni wangwana hivi? Wale Watanzania wachache ambao huchangia Kenya section ndio wabishi. Hawa wa huku wamestaarabika.
 
Back
Top Bottom