Tuwe wakweli: Tusimnange Wema Sepetu; wengine wanagombea, kwanini asigombee?

Wema atauweza ubunge kuliko hata kuigiza. Ana ujasiri mkubwa na ni yule mtu wa call a spade a spade. Siku zote haongei kumfurahisha mtu na ndicho anachotakiwa kuwa nacho mwanasiasa. Hataburuzwa au kufuata upepo. Aende atuwakilishe na Mungu amsaidie.
 
Mzee Mwanakijiji Kwa nini unamlinganisha Wema na akina Sugu, Afande Sele, na Prof. J? Kuna tofauti kubwa sana tu! Hawa wenzake kazi zao za kisanii za huko nyuma zina chembechembe za kiharakati na kisiasa tofauti sana na huyu Wema. Issue kwa wapigakura wengi siyo kazi ya mgombea, bali ni track record.
Kabisa yaani ukijudge ata social media posts fans wake utagundua ana qualities za kiongoz na tatizo watu atuna elimu na ambao walienda shule awakuzingatia form two civics inafundisha qualities of a good leader wema ana jamani
 
Last edited by a moderator:
Jamani huyu dada hajielewi kabisaaaa!!! hv unafikiriaga kile kipindi chake pale EATV(My Shoes) kina mlengo gani kwenye jamii?? Katika binadamu ambao cjawahi kuwaelewa ni huyu bixhost!!!

Watu kupitia iko kipindi tu wanashindwa kujudge lugha anazotumia censorship kibao strategy za ccm kama ujasoma lazima unase
 
Nimeiangalia hiyo picha inayoonesha wananchi wakiwa na nyuso za bashasha wakifurahia kumuona huyu mheshimiwa mtarajiwa. Hapa wameshindwa kutofautisha umaarufu wa huyu dada katika filamu na sifa za mtu wanayetaka awe mwakilishi wao bungeni. Nafikiri hii picha ni mfano mzuri wa ile kitu Karl Marx aliita "false consciousness". Na huyu dada atachaguliwa kwa kuwa ni "maarufu" and not necessarily kuwa amepimwa na kuonekana anafaa kuwa "mwakilishi" wa kundi fulani la watu.

"Hakuna sifa aliyopungukiwa"? Hao wengine tunaowakosoa kila siku wamepungukiwa sifa gani? Kwa kuwa anagombea uwakilishi, lazima awe scrutinized bila kujali umaarufu au jinsia yake. Mimi nafikiri si sawa yeye kwenda kuomba kuwa mwakilishi wa watu wa Singida wakati yeye si "mwana Singida" [wana Singida ni wakulima na wafugaji na wanaishi Singida]. Hiyo ni dharau kwa "wana Singida". Mwakilishi wa "wana Singida" ni vyema akatoka miongoni mwa "wana Singida".

Huwezi kutoka huko ulikotoka kama "outsider" kuja kuomba kutuwakilisha. In fact, "wana Singida" ndio wanatakiwa kumuomba mtu mmoja miongoni mwao awawakilishe. Hii dhana ya mtu kuomba kuwawakilisha wengine ina mapungufu. Kwa nini uombe kuwa mwakilishi wa watu ambao si "wenzako"? Kwa nini usisubiri uombwe na "wenzako" kuwa mwakilishi wao?

Double standard or not, nchi hii haihitaji kina "Wema" bungeni kutunga sheria.

TEAM WEMA SEPETU
Unafikiri watu kwa hiyo picha wanafurahi kumuonaa WEMA akitangaza nia ya ubunge????????? LA HASHA Bali wanamshangaa maana kitambo walipata kumuonaa kwa television na SIO LIVE
SO hiyo ulikua chans kwao kujionea kwa macho
Hivi, unapoona mkutano wa CCM ukiwa na lundo LA Raia Hua Unafikiri wote ni wanachama????????
Shame upon you, WEMA awe mbunge wa BONGO MOVIES AU fikir twice na SIO kukurupuka tu au ndo yule WANJERA hhahahhhhahhaahhahhahahaahah!!!!!!!!!!!!!!
 
To make something special you got to make people believe its special

Vyama vya siasa vimekuwa vinapeleka wabunge walio below par kwanini iwe tofauti kwa huyu.

Ni nchi pekee ambayo mmbunge ajui tofauti ya value added tax and profit tax (huyu kweli ataweza isimamia serikari au hata kutoa mapedekezo ya utawala bora) tena anasimama kifua mbele kuleta hoja yake: hapa namzungumzia yule mama aliyezaa na Mahiga apparently. Halafu watakuja mashangingi wa kisiasa hapa watatupa mlolongo mrefu wa wasifu wake.

If you ask me tukifanya makosa tena tuna miaka kumi mingine ya kulalama najua mwanakijiji atakuwa bado na moyo wengine we might as well start kupanga ustaarabu wetu to hell na hizi siasa uchwara.
 
11406982_861561753918334_6519914178628524682_n.jpg


Yote Tisa: Kama watu wanaogombea wako hivi, kwanini Wema naye asigombee? Ukikubali kina fulani wagombee, basi na kina fulani nao waachwe wagombee. Watanzania wakiwachagua wataishi na uchaguzi huo kwa miaka mitano. Kama ana mashabiki wake katika Bongo Movies na hata nje ya Bongo movies, kwanini asigombee?

Nina uhakika kama ingekuwa ni marehemu Kanumba watu wangeunga mkono tu - na alitangaza nia ya kugombea kwa wanaokumbuka.

Tusimnyanyapae kwa sababu ni mwanamke au ametumia vipaji vyake jinsi alivyotumia. Mbona Sugu aligombea akashinda na hajahukumiwa kwa Bongo Flava yake huko Mbeya bali kwa uwakilishi wake kwa wananchi wa Mbeya?

Tumesikia Profesa J, Afande Sele, wote wanania ya kugombea, lakini sidhani kama wamehukumiwa kwa sababu ya muziki wao. Kwanini iwe kwa Wema?

Ilimradi anatimiza vigezo vya msingi - raia wa Tanzania, miaka 18 na hajawahi kufungwa kwa zaidi ya miezi sita (I think) basi aachwe agombee tu.

Lakini upande wa pili una ukweli pia; yeyote anayetangaza kugombea ajue pia ametoa haki ya wananchi kukosoa, kubeza na hata kutounga mkono kugombea kwake. Ndio raha ya demokrasia; sio wote wanapaswa kumuunga mkono; haijalishi cheo gani. Ndio maana tupo wengine hatuwaungi mkono kina Lowassa na wengine.

Inawezekana tungependa agombee kwa chama kingine isipokuwa CCM; well, ndio uzuri mwingine wa demokrasia pia. Wengine wa Bongo Flava na Bongo Movies wamegombea nje ya CCM na ni haki yao; na wengine wenye kuamini CCM wagombee, vinginevyo tutakuwa taifa lenye mawazo ya aina moja tu kama mashine.

MMM

Akili ndogo kamwe haiwezi kuruhusiwa kuongoza akili kubwa. Ili upige picha za utupu ni lazima ujitoe ufahamu kwa maana hiyo lazima upungukiwe na akili.
Nilichogundua asilimia kubwa sana ya watanzania hawana akili timamu na uwezo wa kupambanua mambo wengi ni vichwa vitupu yaani mnajua vitu vichache.
Uongozi una sifa na utaratibu wake. Nyerere alisema mwanasiasa lazima ujiheshimu na hotuba hii hurudiwa sana ITV akitoa mfano wa mbunge aliyefukuzwa kwa sababu tu ya kulala na changudoa.
Wabunge wehu kama hawa ambao wanajaza server kwa picha za utupu mnaotaka kuwachagua ambao akili zao zinaonekana wazi zina mushkeli hawastahili kukaa meza moja na kina Tundu Lissu, Mbatia, Lipumba, Dr. Slaa, Zitto Kamwe au Kafulila eti wanatafakari mustakabali wa Taifa la Tanzania.
Aendelee na entertainment na kutafuta kick kwa kupiga picha za utupu lakini kwenye uongozi akae pembeni kwani hatupo tayari kuongozwa na mtu ambayo picha za makalio yake, matiti zimesambaa mtandaoni na watu wehu kama wewe mnakuja kuandika uharo kama huu.
Mpumbavu akinyamaza kimya anaonekana mwenye hekima.
 
tyranny of majority .
Tanzania tunafanya mambo kinyume na dunia inakoelekea.Kuna watu wanahalalisha uwepo wake kwa sababu tu kuna wapuuzi huko bungeni basi turuhusu wendawazimu wengine pia waende.AJABU.
nilitegemea tuhamasishe watu tuwatoe hao wajinga na kulisafisha bunge badala yake tunapanga kulichafua zaidi.INASIKITISHA

Sio demokrasia ni democrazy
 
tyranny of majority .
Tanzania tunafanya mambo kinyume na dunia inakoelekea.Kuna watu wanahalalisha uwepo wake kwa sababu tu kuna wapuuzi huko bungeni basi turuhusu wendawazimu wengine pia waende.AJABU.
nilitegemea tuhamasishe watu tuwatoe hao wajinga na kulisafisha bunge badala yake tunapanga kulichafua zaidi.INASIKITISHA

Sio demokrasia ni democrazy

Moyo wangu unasikitika sana kuona Taifa bado lina idadi kubwa sana ya watu wasio na uwezo wa kupambanua mambo na kwa style hii napenda kusema Tanzania bado ipo nyuma sana kwani idadi kubwa ya watanzania bado ni vichwa vitupu tena vitupu kweli kweli.
Mleta mada anafikiri siasa na uongozi ni entertainment basi mtu yeyote anafaa kuwa kiongozi imefikia hatua hadi wapiga picha za u tupu sasa wanataka kuwa wabunge.
Hivi wanajua sifa za kiongozi kweli.
Ni bora wajinga na wapumbavu wakafa tu tujue moja maana uwepo wao duniani unazidi kulipeleka pabaya Taifa letu.
 
TEAM WEMA SEPETU
Unafikiri watu kwa hiyo picha wanafurahi kumuonaa WEMA akitangaza nia ya ubunge????????? LA HASHA Bali wanamshangaa maana kitambo walipata kumuonaa kwa television na SIO LIVE
SO hiyo ulikua chans kwao kujionea kwa macho
Hivi, unapoona mkutano wa CCM ukiwa na lundo LA Raia Hua Unafikiri wote ni wanachama????????
Shame upon you, WEMA awe mbunge wa BONGO MOVIES AU fikir twice na SIO kukurupuka tu au ndo yule WANJERA hhahahhhhahhaahhahhahahaahah!!!!!!!!!!!!!!

Sijakuelewa.Punguza emotions. Kama hutajali, tafadhali fafanua ulitaka kusema nini? Na kabla ya kufanya hivyo, please read my post again. Maneno kama "chans", "hua", "wanjera" etc yameniwia magumu. Andika kwa utulivu ili upate kueleweka.
 
CCM hatutaki ma.laya.. hatuna nafasi ya kazi hiyo...!!!

Mwanakijiji tuombe radhi CCM... ASAP..!!

Umekidhalilisha chama sana... hatuna kazi za u.malaya CCM...!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom