Tuwe wakweli: Tusimnange Wema Sepetu; wengine wanagombea, kwanini asigombee?

11406982_861561753918334_6519914178628524682_n.jpg


Yote Tisa: Kama watu wanaogombea wako hivi, kwanini Wema naye asigombee? Ukikubali kina fulani wagombee, basi na kina fulani nao waachwe wagombee. Watanzania wakiwachagua wataishi na uchaguzi huo kwa miaka mitano. Kama ana mashabiki wake katika Bongo Movies na hata nje ya Bongo movies, kwanini asigombee?

Nina uhakika kama ingekuwa ni marehemu Kanumba watu wangeunga mkono tu - na alitangaza nia ya kugombea kwa wanaokumbuka.

Tusimnyanyapae kwa sababu ni mwanamke au ametumia vipaji vyake jinsi alivyotumia. Mbona Sugu aligombea akashinda na hajahukumiwa kwa Bongo Flava yake huko Mbeya bali kwa uwakilishi wake kwa wananchi wa Mbeya?

Tumesikia Profesa J, Afande Sele, wote wanania ya kugombea, lakini sidhani kama wamehukumiwa kwa sababu ya muziki wao. Kwanini iwe kwa Wema?

Ilimradi anatimiza vigezo vya msingi - raia wa Tanzania, miaka 18 na hajawahi kufungwa kwa zaidi ya miezi sita (I think) basi aachwe agombee tu.

Lakini upande wa pili una ukweli pia; yeyote anayetangaza kugombea ajue pia ametoa haki ya wananchi kukosoa, kubeza na hata kutounga mkono kugombea kwake. Ndio raha ya demokrasia; sio wote wanapaswa kumuunga mkono; haijalishi cheo gani. Ndio maana tupo wengine hatuwaungi mkono kina Lowassa na wengine.

Inawezekana tungependa agombee kwa chama kingine isipokuwa CCM; well, ndio uzuri mwingine wa demokrasia pia. Wengine wa Bongo Flava na Bongo Movies wamegombea nje ya CCM na ni haki yao; na wengine wenye kuamini CCM wagombee, vinginevyo tutakuwa taifa lenye mawazo ya aina moja tu kama mashine.

MMM
Habari wadau wa JF.

Mnakumbuka msiba wa DC Mtwara aliyefariki wiki iliyopita? Nauliza hivi kwa sababu Watanzania ni wepesi wa kusahau aidha kutokana na pilika za maisha au matukio kuwa mengi.

Inasemekana Rais Magufuli amemshirikisha Mama Samia kumtafuta mwanamke ktk tasnia ya bongo muvi au bongo flavour ili achukue nafasi ya DC Mtwara ambayo ipo wazi. Inadaiwa nafasi hiyo ilikuwa zitangazwe ktk uteuzi wa Jana wa waziri wa sheria na katiba wakati moja.

Inadaiwa pendekezo hilo la Mama Samia lilimfikia Magufuli jioni saa 12 Jana na haikujulikana kwanini Rais hakuambatanisha uteuzi wake wa Mwigulu na Mwanabongo Muvi Wema Sepetu. Hata hivyo ushauri huo wa Mama samia au Mama wa Busara unadaiwa kuridhiwa na Rais.

Stay tuned muda wowote kitu kitarushwa hewani.
Duh...!, hata kama ingekuwa kweli, sasa ndio umeharibu!, umemharibia kwa kuitoa nje hii siri, hivyo umemponza na jina lake sasa limeondolewa, hateuliwi tena yeye, sasa atateuliwa mtu mwingine tuu ila ni mwanamke!.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom