Tuwe sehemu ya Msaada kwa Walemavu wa Macho (Vipofu) hasa Vituoni na Barabarani kwani hata Wewe ni Kipofu Mtarajiwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
GENTAMYCINE huwa Nakereka mno kuona Mlemavu wa Macho Kipofu (tena yuko na Fimbo yake) anaomba Msaada wa ama Kupandishwa katika Dala Dala au Kumvusha Barabara au kutaka Kukaa mahala kisha unawaona Watu wanamkwepa au kujifanya hawamuoni.

Waswahili tuna Roho Mbaya mno halafu ni Wanafiki sana japo kila Siku huwa tunajifanya Kusali na Kuswali katika Nyumba zetu za Ibada.

Hivi Kumpa tu Ushirkiano Mlemavu huyo wa Macho (Kipofu) utapungukiwa na nini?

Mbona Mimi GENTAMYCINE huona sana Faraja Kuwavusha Watoto wa Shule (ambao Wengine ni sawa na Wajukuu zangu) pale wakiwa wanataka Kuvuka katika Barabara Kubwa na Hatarishi kwao Kiusalama na huwa Wanafurahi na Kunipenda zaidi?

Halafu akina GENTAMYCINE tukiwa tunapendwa na kukubalika sana JamiiForums mnachukia mkisahau kuwa Wema ambao huwa nautoa kwa Watu (Makundi mbalimbali) na Wao Kuufurahia huishia Kunishukuru na Kuniombea Dua Njema na Mafanikio mengi na kunifanya muda Wote niwe nang'aa tu.

Acheni Kuwadharau Walemavu wa aina yoyote ile kwani Mimi GENTAMYCINE na Wewe hakuna ambaye ana HATIMILIKI na Mafanikio yake Kimaisha na aliyeambiwa kuwa kamwe hatokuja kuwa / kupatwa na Changamoto za Ulemavu hivyo ukiona kuna Mlemavu yoyote anahitaji Msaada wako jitoe kwa 100% huku ukiwa na Moyo Mkunjufu katika Kumsaidia.

Baraka siyo lazima uzipate Msikitini, Kanisani, kwa Waganga wa Kienyeji au kwa Mizimu ya Mababu na Mabibi bali hata Wema wako kwa Walemavu pia ni Tiketi Tukuka tosha ya Wewe Kubarikiwa, Kufanikiwa na Kulindwa dhidi ya Maadui zako.

Kuna Wadada Wawili wamenikera mno Asubuhi hii katika Kituo kimoja cha Basi kwa Kushindwa kutoa Msaada wa Kumvusha Mlemavu wa Macho (Kipofu) kisha wakimkwepa huku Wakimnyali ( Wakimbagua ) kama vile ni Mchafu na ananuka huku wakiwa Wanacheka bila hata Chembe ya Utu Mioyoni mwao.
 
Back
Top Bottom