Tuwathamini, Tuwaendeleze. One individual can make a Difference | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwathamini, Tuwaendeleze. One individual can make a Difference

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Entrepreneur, Mar 16, 2012.

 1. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Wazo hili limekuwa linajia kichwani mara kwa mara hasa baada ya kukutana na Mtanzania mwenzetu, ndg,Zacharia Zamokewakati anaanza kufanya utafiti wake juu ya namna ya kutengeneza Incubator, nilivutiwa zaidi baada ya kukutana na Dada mmoja aitwaye Vida Mahimbo, na kujua historia ya namna alivyoanza kwenye designing and Fashion hususani khanga Jeans. Na sasa baada ya kusoma kitabu cha William naona ni wakati muafaka.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Labda kwanza tujiulize; Ni vijana wangapi wanaogundua vitu vyenye maana na kazi zao zinapotelea angani? Ni vijana wangapi wameshindwa kuziendeleza tafiti zao zenye manufaa kwa jamii kwa ukosefu wa elimu? Ni vijana wangapi tunawaona kama ni vichaa wanapoanza kutengeneza vitu vyenye manufaa, na badala ya kuwasaidia tunawakatisha tamaa? Je hatuna uwezo wa kuwaendeleza watu hawa, au hatutaki kuwaendeleza watu hawa? Na ni vijana wangapi, ambao kama wangesaidiwa, kazi zao zingeweza kuboresha hali ya maisha ya Jamii zetu? [/FONT][FONT=&amp]Ndugu mwanaJF wakati ukiwa unatafakari maswahi hayo, naomba unipe muda wako na tusafiri pamoja ili tukakutane na;[/FONT]

  [FONT=&amp]1. [/FONT][FONT=&amp]Zacharia Zamoke- Imberruz[/FONT]
  [FONT=&amp]Huyu kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa kibiashara, aliamua kuwekeza nguvu zake kwenye utengenezaji wa Incubators za kienyeji kwa kutumia malighafi zilizomzunguka, lakin baada ya miezi tisa akafanikiwa kuja na Mashine yake. Baada ya kuonekana na kusaidiwa, now he is making a Brand na amebalisha namna Watanzania walivyokuwa wanauangalia utotoleshaji wa vifanga hasa maeneo yasiokuwa na umeme. Anapatikana HAPA kwa sasa
  [/FONT]
  [FONT=&amp]2. William Kamkwamba - Moving Windmill[/FONT]
  [FONT=&amp]Huyu ni school dropout, ambaye alikosa ada, lakini akiwa na umri wa miaka 14 aliweza kutengeneza mtambo wa kuzalisha umeme, kwa kutumia local resources na blueprint ya kwenye kitabu cha Fizikia. Kama bado hujapata kitabu chake THE BOY WHO HARNESSED THE WIND, nakushauri ukitafute kwani hutajutia fedha yako. It had a profound impact on me.[/FONT]

  [FONT=&amp] Huyu nae aliweza kufanikiwa baada ya kusaidiwa na wamerekani. Unaweza ukampata kwenye CLIP HII lakini anza HII[/FONT]

  [FONT=&amp]3 . Vida Mahimbo – Khanga Jeans[/FONT]
  Tanzanian designer Vida Mahimbo has set her sight towards conquering the fashion world with her creative khanga jeans collections. She now conquer Europe,African and US market, with the same collection. Huyu ni mtengenezaji maarufu wa Jeans za akina Dada maarufu kama "khanga jeans", (hii ni Brand mpya kabisa katika ulimwengu wa fashion), [FONT=&amp]lakin nae aliweza kufanikiwa baada ya kupata Msaada kutoka kwa Waitaliano. Unaweza ukampata HAPA[/FONT]

  [FONT=&amp]WanaJF,kwa kutambua uwepo wa wadau wetu katika sehemu kubwa ya nchi hii, na kwa kutambua uwepo wa watu (innovators) wanaojihusisha na uvumbuzi, huko vijijini na uvumbuzi wao unapotelea angani bila kuendelezwa au kuwa inspiration kwa watu wengine. Ninaomba yeyote mwenye taarifa za watu wa aina hii wawe wanatupia taarifa hizo kwenye thread hii ili tuweze kuwathamini na kuwaendeleza [/FONT]

  [FONT=&amp]Did I hear everyone say "Amen?"[/FONT]
  [FONT=&amp]Thank you.
  Tunahitaji kuwatambua ili tuwathamini na kuwaendeleza
  [/FONT][FONT=&amp]One individual can make a Difference. [/FONT]
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  basi huyu dada vida kajitahidi sana yaani ukiwa na mawasiliano mazuri na hawa FTV kwenye mambo ya ulimbwende umeula..
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu NDETICHIA bora wewe umeliona hilo. Hakika Mdada huyu ameleta/analeta mabadiliko. Lakini hapo kwenye red, huyu Vida alishaula awali pale wazo tu lake lilipopata kutambuliwa, kuthaminiwa na kuendelezwa. Na ndio maana tunasema tunahitaji kuwatambua hawa watanzania wanaofanya innovation huko vijijini (locally) i[FONT=&amp]li tuwathamini na kuwaendeleza[/FONT]
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  MKUU KWA HUYO NO MOJA

  1. Nijuavyo mimi wavumbuzi wano tengeneza vitamishi vya mayai ya kuku wako wengi sana sasa swali linakuja je waendelezwewote au huyo mmoja tu?

  Mimi nilitembeleaa monyesho ya kilimo ya nane nane, nilikutana na wavumbuzi tofauti 10 wa viatamishi sasa mimi nzani ni bora kuwaendeleza wote

  2. Mkuu kingine hata hawa wavumbuzi wana makosa mengi sana na wanatakiwa kujifunza kwanza na uvumbuzi huchua miaka mingi sana hata wakina HENRY FORD iliwachua miaka mingi sana mpka kuja na real Car

  - Cheki kwenye post yangu hapa wambuzi wa ndege iliwachua miaka

  - Sasa Watanzania tunagundua kitu leo kesho mtua anaanza kukiuza tena kwa bei ya juu sana yaani yeye anatageti faida, mimi nilimhoji mmoja wa watengeneza viatamishi nikamuuliza Una muda gani tangu kugundua hii kitu?
  ALINIJUBU NI MIEZI 9 NA HAPO ALIPOMKUWA ANAIUZA HIYO ALIYO GUNDUA YA KWANZA, NDO MAKOSA TUNAYO FANYA, NI LAZIMA KWANZA WALENGE MIAKA HATA 20 IJAYO NA SI KUGUNDUA LEO NA KESHO WANATENGENEZA TENA WANAANZA NA UCHAKACHUAJI KABISA,

  - Kuna jamaa mmoja aligundua jiko zuri sana na yeye alikuwa na muda mfupi sana, cha kusikitisha alianza kutengeneza order za watu kwa kuchakachua vitu sana hebu fikilia mtu kama huyu ana tageti nini?
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hatuhitaji kumuendeleza huyo namba moja pekee kwani yeye ameshapata watu wa kumuendeleza na sasa ana brand yake ya Imberruz. Nadhani hao wengine kumi (uliowasema) ndio wanaohitaji huu msaada wa kuendelezwa zaidi kuliko huyo Bw. Zakaria niliyemtaja. Sasa tungepata kujua their side of story ingekuwa ni muafaka sana.

  Halafu watanzania wengi, wanaojihusisha na uvumbuzi, wanakosa msaada mhimu katika kujiendeleza ndio maana product zao zinakuwa za mashaka. Hata maswala ya Intellectual Property protection hawayajui ndio maana uvumbuzi wao unaishia kuchakachuliwa baada ya muda mfupi. Lakin pamoja na haya yote bado tunahitaji kuwajua watu hawa ili tuwathamini na kuwaendeleza

  Hapo kwenye RED ndio matatizo ya kutokuwa na R&D Institution kwani utafiti unagharama kubwa sana. Sasa kwa kuwa wavumbuzi wengi wanakosa finacing katika tafiti zao na piloting, matokeo yake ni kulipua kazi ili kufidia gharama. Wengi wao wanatumia kile kidogo walichonacho na wakifanikiwa tu kuzalisha wanachokihitaji, basi wanafikiria kwanza kurudisha gharama zao, kabla watoto wa mjini hawajaanza kuchakachua utaalamu wake. Hili ni tatizo kubwa, lakin pamoja na hayo bado tunahitaji kusikia historia zao
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  1. Ni kweli wanakosa msaada ila tatizo kubwa kwao ni kwamba wanawaza pesa mara tu baada ya kuvumbua, hawawai kuja kuwa watu muhimu katika Dunia hii wao wanawaza pesa,

  2. Kuna yale mashirika ya Serikali nazani ndo wanahusika kuwa endeleza ingawa hawa watu wa serikali wako kiulaji sana,

  3. Na kingine ili wafanikiwe ni lazima na sisi tupende vitu vya Tanzania hata kama havina Ubora, Watanzania wanachikia sana vitu vya ndani ya nchi na hata wewe jiulize ndani mwako sufuria unazo pikia zimetengenezwa wapi? je Meza ya komputa?

  China kwa mara ya kwanza walivyo tengeneza JEIFONG YAO/ TIPER YAO walichekwa sana na nchi za ulaya kwamba ina sura ya ajabu lakini kiongozo wao wa mapinduzi alisha sema hawatakaa waagize kitu kutoka nje labuda malighafi tu na wachina waliunga mkono kwa kununua vitu vya kwao hata kama vilikuwa havina ubora
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye RED unanikumbusha jana kwenye Guided Democracy & Guided Economy. Sasa sisi kwa mfumo wetu tulioingizwa tukiwa tumefumba macho tunaweza?
   
 8. G

  GenX Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri sana kuwatangaza na kuwaendeleza wavumbuzi na wafabiashara wetu wa ndani. Shida kubwa ni pale SERIKALI YETU inapataka watu waagize mpaka vibiriti, sukari, maboga, machungwa, maembe, nk wakati vinaweza kuzalishwa hapa hapa nchini kwetu.

  Once mtu anapogundua kitu na kuweza kutumika, the next big thing is market. Kama huna soko, huo ndio mwisho wako. Kwa hiyo inabidi tuanze kuibana serikali yetu iache hii tabia ya kutoa vibali vya kuagiza kila kitu.
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kwenye RED umenikumbusha mbali mwaka jana mwezi wa 11. Niliona taarifa ya Habari kupitia TBC1, kuwa kijana mmoja aitwaye Petro a.k.a.Mzimu amekamatwa na kuwekwa ndani kwa sababu amefanikiwa kutengeneza bunduki aina ya Gobore kwa malighafi zinazomzunguka.

  Yaan badala SERIKALI imchukue na kumpeleka jeshini, akaendelezwe, yenyewe inamtupa lupango! Sasa kama inaweza kuwachukua wachezaji hodari wa mpira na kuwaingiza jeshini inashindwa vipi kwa watu kama hao? Anyway, hayo tuyaache, kwani kwa sasa si wakati wa kulaumiana bali ni wakati wa kuendelezana na kuthaminiana ndio maana tunahitaji kuwatambua na kuwaendeleza. Mkuu weka taarifa za watu hao hapa jamvini kama unazo tafadhali
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  After spending a year experimenting with converting wasted vegetable oil (WVO) into usable biodiesel fuel in a New York City garage, Mwakilasa launched Mafuta Sasa Ltd, the first WVO-to-biodiesel company in East Africa.

  Based in Dar es Salaam, Tanzania, the company collects their WVO from hotels, restaurants, and street cart vendors from across Dar es Salaam for a small fee and brings it to their refinery, where it undergoes a carefully calculated process of mixing, heating, cooling, settling and sifting before it is turned into clean burning biodiesel that meets the exacting specifications of local petroleum diesel.

  The biodiesel is then sold back to hotels, bakeries, apartments, other establishments around the city seeking cheaper, cleaner burning fuel.

  With the price of petroleum diesel hovering at around 1,800-2,000 TSH ($1.40 USD) per liter, Mafuta Sasa’s biodiesel is the cheaper alternative at 1,250 TSh.
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Captain Athumani Msekeni (retired)- invented an air-driven generator. He won the first best invention award in the industrial rights back in 2006. His invention is recognized by the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) and the Business Registration and Licensing Agency (BRELA)from that year he has been struggling single-handedly to have his invention benefit Tanzanians. Sijui kafikia wapi kwa sasa?

  Source; The guardian of 19th October 2009. [FONT=&amp]Ex-army officer-cum-inventor struggles for recognition[/FONT]. By Lucas Lukumbo
   
 12. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Akili ya viongozi wetu ipo kwenye KUOMBA so hawaoniumuhimu wa kuwaendeleza watu wenye mawazo ya ubunifu kama hawa, labda wangekuwawatoto wao, hapo, lalalalala..... tungesikia filimbi zinavyopigwa.
  Lakini wapi, mtoto wa kigogo au fisadi hawezi kuwa mbunifu ki hivyo kwaniubunifu aghalabu huambatana na shida aliyonayo mtu jambo ambalo kwa wenyeukwasi halipo.

   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unayoyasema ni ya ukweli Kamuzu, ndio maana ninapendekeza sisi kwa sisi tuwatambue, tuwathamini na kuwaendeleza bila kuwawetegemea hao viongozi wetu. Kwani kwa miaka hamsini hapa ndipo walipoweza kutufikisha. Yaan hata tooth pick na cotton buds tunaagiza kutoka china!
  Kama unataarifa zao tafadhali tuwekee hapa
   
 14. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,611
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Wakuu, mimi kama mjasilimali swala la Kuleta Venture Capitalist (Business incubator) bado ninaliwaza kila siku. Nadhani Tanzania kuna idea nyingi na innovators wengi lakini hakuna capital allocation system nzuri. Mitaji ipo sababu surplus zipo lakini allocation of capital to entrepreneurs ndio hakuna na hapo ndipo ninapowaza kuwekeza.

  Hawa innovator wanatakiwa kupewa mtu ambae atawapa capital na atawapa business strategy "know how". Nikimaanisha, kuumpa mtaji, kumuongoza kwenye hatua ya Research & Development, kisha kwenye hatua ya kutafuta patent na mwisho kwenye hatua ya kuzalisha na kuleta product sokoni. Venture Capitalist ndio walio sababisha dot com business inyanyuke kwa haraka ndani ya muda mfupi.

  Sikubaliani na wale wanaotaka serikali iwape mitaji hawa wajasilimali, bali nakubaliana na wale wanaosema serikali itakiwa iondoe ukiritimba kwenye sehemu zote muhimu kuanzia kusajili biashara yako mpaka kuondolewa tax kwa muda fulani. Watanzania wanaweza wakiwezeshwa.
   
 15. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna watu walidhani business incubators ni lazima zianzishwe na serikali au kwa msaada wa NGO kubwa za kimataifa. Lakini nimeshuhudia private enterprise zikifanya hii kitu South Africa, tena kwa faida na mafanikio makubwa sana. Sasa Mkuu Mtanganyika, kikwazo kwako ni nini? Mbona huanzi?
  Kwa sasa nimeona watu wa COSTECH wanafanya hii kitu hasa kwenye maswala ya ICT. Lakini bado kuna watu wengi sana out there ambao ubunifu wao unapotea kwa kutokuendelezwa
   
 16. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Mnamo tarehe 23/08/2011 TBC1 walirusha taarifa kumuhusu Kijana wa Kitanzania mwenye elimu ya darasa la saba aliyefanya uvumbuzi, alitengeneza magari manne kwa kutumia vipuri vya pikipiki na vyuma chakavu!!!!![/FONT]
  [FONT=&amp]Huyu kijana ni wa huko Mbinga. Jamani wana JF wa Mbinga mna taarifa za huyu kijana?[/FONT]
   
 17. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mwaka 2011, wakati naangalia kipindi cha Ruka Juu na FEMA TV Talk show, nilimuona kijana ajulikanaye kama Rajab Mnyamisi Mgongwe, kwao ni wa huko Gombero Kilindi, Tanga. Alikuwa akielezea namna mtambo wake unavyofua umeme. Yeye anazalisha na kusambaza umeme.

  Alitengeneza mtambo wa kufua umeme na kuwagawia wanakijiji wenzake huduma hii. WanaJF wa kilindi mpoo? Tunaomba taarifa za huyu jamaa
   
 18. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,611
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Entrepreneur kuna mambo mawili matatu yamesimama njiani lakini mpango huo upo. Nadhani hatuitaji serikali kwenye swala hili.
   
 19. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu. Tukiweka nia (kama private sector) tunaweza
   
 20. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii nimeipata HUKU wadau nikaona ni vyema kuiunganisha hapa. Wanapatikana http://www.simgas.com
   
Loading...