Tuwapeleke watoto wakasome kiingereza

Tuwapeleke watoto wakasome kiingereza

Habari.

Kumekuwa na changamoto ya watu kulalamika maisha magumu.

Ila yote juu ya haya kama mzazi una mtoto jitahidi sana uweke ubahili pembeni mpelekeni mtoto wako shule ya English medium.

Watanzania tumekuwa tukipishana na Fursa nyingi sana kuanzia Utalii, uhusiano na mataifa mengine kwa sababu ya kutokuwa na ufasaha katika kuandika na kuongea lugha hii.

Leo hii kwenye interview tu kijana imekuwa ngumu sana kutumia hata dakika 10 kujieleza kwa kiingereza.

Viongozi wa nchi,watu mashuhuri,wanamziki wamekuwa wakishindwa kusimama kwenye warsha au makongamano kuongea kiingereza kwa ufasaha.

Maelezo mengi sana yamewekwa katika lugha ya kiingereza kuanzia mabango barabarani, matumizi ya simu binafsi, maelezo katika vipeperushi baadhi.

Kiukweli kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwekeza lugha ya kiingereza kwa Watoto wetu maana samaki mkunje angali mbichi.

Kwa muingiliano wa watu nchini na fursa mbalimbali katika soko la ajira inahitaji sana mtu mwenye kuweza kuongea na kuandika lugha ya kiingereza fasaha.

Rai yangu Tuwapeleke watoto wetu wakasome kiingereza.
Na hisabati vile vile.
 
We mwenyewe hujaja na trust source kuthibitisha idadi uliyotoa, halafu unataka uletewe trust source ya kipinga, una wazimu bila shaka.
Screenshot_20230202-081017_Google.jpg
 
Unasumbuliwa na uvivu wa kufikiri na kutenda kuhusu kupenda lugha yako
Kuna course ili upate sifa za kuzisomea lazima uwe unajua kingereza vizuri,points zako zina maana tukiangalia mlengo wa kizalendo,but kwa point ya kusema wachina hawaongei kingereza Pole sana,wataalamu wasomi wakubwa wa China 95% wamesoma vyuo vya Marekani,,angalia television ya Taifa ya China inaitwa CGTN,labda utajifunza kitu..kingine ndugu yangu hujatembea,tembea uyaone
 
Sijasisitiza kwamba wachina hawaongei kiingereza bali nimesisitiza kuwa wanakipenda na kukienzi kichina. Tofauti na wabongo inakuja hivi "tunashindwa kuipenda na kuienzi lugha yetu" na badala yake tunashobokea lugha ya mwingereza, hujiulizi utajenga lini lugha yako ya nyumbani?

Wachina pamoja na kusomea ktk vyuo vikuu USA hawajawahi kukidharau kichina na mara nyingi uvumbuzi wao huwasilishwa ktk lugha ya kichina kisha hutafasiriwa ktk lugha zote ulimwenguni na sio kiingereza peke yake.

Jifunze hilo ndugu.
point ya kusema wachina hawaongei kingereza Pole sana,wataalamu wasomi wakubwa wa China 95% wamesoma vyuo vya
 
Unaweza tengeneza source kwa kuweka idadi ya namba uitakayo na usiwe na uthibitisho wowote kuhusu hiyo kitu.

We endelea tu kukifagilia kiingereza maadam unaamini kuwa ni lugha ya 'wajanja' kitu ambacho sio kweli.
Nimesema lugha ya wajanja??kusoma kiswahili huwezi??
 
Sijasisitiza kwamba wachina hawaongei kiingereza bali nimesisitiza kuwa wanakipenda na kukienzi kichina. Tofauti na wabongo inakuja hivi "tunashindwa kuipenda na kuienzi lugha yetu" na badala yake tunashobokea lugha ya mwingereza, hujiulizi utajenga lini lugha yako ya nyumbani?

Wachina pamoja na kusomea ktk vyuo vikuu USA hawajawahi kukidharau kichina na mara nyingi uvumbuzi wao huwasilishwa ktk lugha ya kichina kisha hutafasiriwa ktk lugha zote ulimwenguni na sio kiingereza peke yake.

Jifunze hilo ndugu.
Kwani hatukipendi na kukienzi kiswahili??au ulitaka nini kifanyike ili uone kiswahilj kimepewa heshima yake??
 
Kutojua Kiingereza kumeongeza ujinga sana Tanzania.
Kuna wajinga wengi tu Tanzania na wanazungumza kiingereza swafi kabisa, acha kuwaza kikoloni 😁.

usemi wako kwamba "kutojua kiingereza kumeongeza ujinga....." ni kinyume chake.
 
ulitaka nini kifanyike ili uone kiswahilj kimepewa heshima yake??
Tukieneze kwa mataifa mengine. Wasomi wetu wakivumbua kitu Kipya wakielezee kwa kiswahili fasaha kisha huo uvumbuzi ufasiriwe kwa lugha za mataifa mbalimbali duniani.
 
Tukieneze kwa mataifa mengine. Wasomi wetu wakivumbua kitu Kipya wakielezee kwa kiswahili fasaha kisha huo uvumbuzi ufasiriwe kwa lugha za mataifa mbalimbali duniani.
Mbona ndio kinafanyika hadi vyuo vikuu uingereza,marekani,Ujerumani,Ethiopia, kuna courses za kiswahili na wanafunzi sio watanzania???kiswahili sio lugha ndogo ila ukubwa na impact ya kingereza hujajua tu au hutaki kujua, English ni dunia nzima..
 
Back
Top Bottom