2025DG
JF-Expert Member
- Jan 30, 2023
- 519
- 1,553
Habari.
Kumekuwa na changamoto ya watu kulalamika maisha magumu.
Ila yote juu ya haya kama mzazi una mtoto jitahidi sana uweke ubahili pembeni mpelekeni mtoto wako shule ya English medium.
Watanzania tumekuwa tukipishana na Fursa nyingi sana kuanzia Utalii, uhusiano na mataifa mengine kwa sababu ya kutokuwa na ufasaha katika kuandika na kuongea lugha hii.
Leo hii kwenye interview tu kijana imekuwa ngumu sana kutumia hata dakika 10 kujieleza kwa kiingereza.
Viongozi wa nchi,watu mashuhuri,wanamziki wamekuwa wakishindwa kusimama kwenye warsha au makongamano kuongea kiingereza kwa ufasaha.
Maelezo mengi sana yamewekwa katika lugha ya kiingereza kuanzia mabango barabarani, matumizi ya simu binafsi, maelezo katika vipeperushi baadhi.
Kiukweli kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwekeza lugha ya kiingereza kwa Watoto wetu maana samaki mkunje angali mbichi.
Kwa muingiliano wa watu nchini na fursa mbalimbali katika soko la ajira inahitaji sana mtu mwenye kuweza kuongea na kuandika lugha ya kiingereza fasaha.
Rai yangu Tuwapeleke watoto wetu wakasome kiingereza.