John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,239
"Lakini tusiishie kuwazomea tu. Hawa ni wahalifu, watu wanaofanya matendo ambayo tayari yanatambulika kama rushwa na ambayo hayakubaliki kisheria kwa sababu ni makosa ya jinai. Pamoja na maelezo yangu kuhusu dhana ya munkari (ukiweza ondoa kwa mkono wako; huwezi kemea usikike; huwezi hata hilo, nuna uonekana umechukia), bado kuwazomea watu wanaotenda makosa ya jinai hakutoshi.
Iko sugu iliyojengeka hivi leo, na sugu hiyo wamejivisha mafisadi wa kila aina nchini kama kinga dhidi ya mashambulizi yote yanayoelekezwa kwao alimradi tu mashambulizi hayo ni ya maneno matupu na wala hayawasababishii maumivu ya kimwili wala hasara ya kifedha.
Wanazisikia shutuma dhidi yao; wanasoma magazeti, au hata kama wameacha kusoma kwa kutotaka kujiona wanavyodhalilishwa, bado wanaambiwa na ndugu zao na maswahiba zao jinsi wanavyoandikwa na kusemwa na kulaaniwa, lakini wao wamekuwa wasadiki wakubwa wa falsafa ya maneno matupu hayavunji mfupa au watasema mchana, usiku watalala. Alimradi hakuna hatua madhubuti za kuwafanya walipe na waumie kutokana na matendo yao hawatakuwa na motisha wa kuyaacha, hasa kama yanawaletea manufaa fulani fulani, na manufaa haya tunayajua.
Dawa mujarrab ya kuwafanya wakome kufanya upuuzi wao ni wa kuwafanya walipe gharama kubwa ili upuuzi wao uwe ghali. Hii ndiyo njia pekee ya kutokomeza utamaduni wa kutoadhibika (impunity) ambao umetawala mwenendo wa siasa katika Tanzania."
Chanzo: http://www.raiamwema.co.tz/07/12/5/4.php