Tuwakumbuke wanachama wa JamiiForums waliotutoka

Tuwakumbuke wanachama wa JamiiForums waliotutoka

kuna wakati fulani mwaka jana mimi na baadhi ya member fulani wa jf tulipanga tukutana pale samaki samaki mlimani city kwa lengo la kufahamiana vizuri.

"huyu bwana" alipoanzisha mambo yake ya kishamba ya kutekana tekana kila mtu akaingiwa na uoga, matokeo yake hatukuweza kufanikisha lengo letu, maana jf ni kichaka kizito, hujuwi nani ni nani.

na kama ingetokea tungekutana basi ingekuwa ni fursa nzuri ya kufahamiana na hata kama mtu kapatwa na tatizo la maradhi au msiba ingekuwa ni rahisi kufahamu.

nasema hivi kwasababu baadhi ya ID hazipo active kwa mrefu na hatujui wahusika walipatwa na masahibu gani.

Mungu azilaze mahala pema peponi roho zote za wanajf waliotangulia mbele ya haki. Amina
Kuna memba anaitwa mpk aliandika tread ya anayejua JPM anatupeleka wapi atuambie.....nadhani ana muda haonekani humu
 
Na nisingeijua Jambo Forums kama si Lemutuz. Kila nikishuka kijiweni baadhi ya mazungumzo ni kuhusu kilichoandikwa humu na Mzee ES ndiyo ilikuwa ID yake wakati huo. Ukiwauliza watu hawasemi wanakwambia nenda Jambo Forums kama aina fulani hivi ya promo. Basi nikasema isiwe tabu siku moja nikaingia humu basi nikalowea.

Tanzatl.org
 
nakumbuka kuna mdada alikuwa anaitwa lara one. watu walikuwa na usongo nae sana wa kumfahamu. ila baadae ikaja kubainika kumbe ni mange kimambi.
Heeeee kumbe nilikuwa sijui
 
Back
Top Bottom