Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Wadau, siku hizi moyo wa kusoma vitabu vya aina zote-vya Taaluma na Riwaya umepungua sana na imepelekea Watunzi wa Riwaya kutoandika tena vitabu. Leo nawakumbuka baadhi ya Waandishi/ Watunzi wa Riwaya wa Tanzania.

Hamie Rajab
1. Miujiza ya Mlima Kolelo
2. Dunia Hadaa

S.M.Bawji
1. Usiku wa Blaa
2. Kisiwa cha Mayuku

1. Njama
2. Hofu
3. Kufa na kupona
4. Hujuma
5. Kikosi cha Kisasi
(All by A.E. Musiba)
 
Kamlete akibisha Mlipue
HAini
Mbali na Nyumbani
Msako wa Hayawani
Rosa Mistika
Dunia Uwanja wa Fujo
Sanda ya Jambazi
 
Wakuu mi nina kiu ya kufa kwa vitabu vya Edi Ganzeli. Nilisoma kazi zake nikiwa bado mdogo na nyingi sikua nimezianzia mwanzo ama kuzimaliza.

Mwenye kuweza kunisaidia namna ya kuvipata hivyo vitabu ani-pm tafadhali.
 
Dah! nafurahi jitihada zangu za kukusanya vitabu inazidi kufanikiwa.
baada ya kuipata vitabu vya alfu lela ulela cha kwanza hadi cha nane, vya Shafi A. Shafi vitano, Shaabani Robert sita, Allan Quarterman viwili, Ben mtobwa Saba, juzi kati nimepata Unyama wa Mafia cha Zahir Ally Zorro, Jamaa hodari kisiwani, kisiwa cha hazina, safari za gulivers, oliver twist, na kubwa lao NJAMA cha marehemu A.E. Musiba.

bado navisaka na kununua. maktaba yangu inazidi kunawiri.
mkuu unavipata wapi hivi vitabu.?
 
Back
Top Bottom