SoC03 Tuwakumbuke Viongozi wa halmashauri za vijiji, Vitongoji na mitaa katika kuumega mkate

Stories of Change - 2023 Competition

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
36
36
utangulizi

Utawala wa vijiji ,vitongoji na mitaa
ni miongoni mwa tawala katika serikali za mitaa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni utawala wa chini kabisa kimuundo ukitanguliwa na utawala wa Kitongoji.

Kuwa utawala wa chini haimaanishi kuwa na umuhimu mdogo; isipokuwa ni kupitia utawala huu ndiko ambako mambo mengi yanayoamuliwa au kupangwa na tawala za juu kama serikali, hutekelezwa.

Utawala wa vijiji, vitongoji na mitaa huelekeza wananchi katika kutumia madaraka yao ya kidemokrasia kuamua juu ya mambo yanayowahusu kama wanakijiji moja kwa moja bila kupitia mlolongo au urasimu mrefu. Kumbe tumeona kwa namna gani tawala hizi zilivyo chachu ya utenda kazi wa serikali kuu katika kuwafikia wananchi wake.

Pamoja na hayo serikali imewasahau sana viongozi wa tawala hizi ikiwa licha ya umhimu wao lakini hawa mshahara, hawana ofisi za kueleweka,hawapewi semina elekezi na mafunzo yanayo wawezesha kuwapatia uwezo wa kiutendaji na hawana posho za vikao kama wabunge na wengine, hawana kinga ya kiulinzi kama wengine hali inayozorotesha utendaji na uwajibikaji wao katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Umuhimu wa viongozi wa halmashauri za vijiji , mitaa na vitongoji nchini.

Viongozi hawa wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya kila mahali katika taifa letu, kwani wana wajibu wa.
  • Kupokea taarifa za mikutano ya vitongoji na kamati zake kufanyia kazi na kupeleka Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kupokea, kutafakari na kufanyia kazi maagizo na mapendekezo kutoka kamati ya maendeleo ya kata (WDC) na halmshari ya wilaya.
  • Kubuni na kuendekeza sera na mwelekeo wa kijiji kwa mkutano mkuu wa kijiji.
  • Kuandaa na kupendekeza mipango ya maendeleo ya muda mrefu kwa Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kutunga sheria ndogondogo kwa kushauriana na Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kuwaalika wataalamu panapokuwa na haja ya kufanya hivyo ila hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
  • Kupokea, kutafakari na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa kijiji maombi ya ugawaji wa ardhi zaidi ya ekari 100 hadi 500 rasilimali zingine kwa maamuzi.
  • Kupokea, kutafakari na kuamua ugawaji wa ardhi chini ya ekari 100.
  • Kutoa taarifa za utendaji kwa Mkutano Mkuu wa Kijiji.
  • Kumiliki mali na kuingia mikataba kwa niaba ya kijiji.
  • Kusuluhisha migogoro mbali mbali katika jamii inayo wazunguka
Changamoto walizo nazo katika kutimiza majukumu yao.

kutokana ukosefu wa mazingira wezeshi kwa viongozi wa serikali vijiji ,vitongoji na mitaa tumekuwa tukishuhudia kwa nyakati tofauti tofauti viongozi hawa wakihusishwa na mambo yasiyo ya kimaadili(maovu)kama vile.
  • Rushwa na ubadhilifu wa mali za umma
  • Wizi wa mali za umma
  • Uonevu na kuchochea migogoro katika jamii kwa masilahi yao binafsi
  • Kufanya maamuzi yenye upendeleo
  • Kuchelewa katika ofisi zao kwani wanalazimika kufanya pia shughuli zingine waweze kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
Nini kifanyike ili kuamsha ari ya kiutendaji na uwajibikaji kwa viongozi hawa.

serikali kuu inapaswa kuwakumbuka kuumega mkate wa taifa na kuwajari viongozi hawa kwa kuwawekea mazingira wezeshi ili waweze kuwajibika ipasavyo katika shughuli za kimaendeleo kwa wananchi
  • Serikali ianzishe mpango wa malipo ya mishahara kwao kama ilivyo kwa wabunge na raisi kwani na wao wanachaguliwa kama wao
  • Wajengewe ofisi na kuboreshewa zilizopo katika maeneo yao
  • Sera za nchi zinazowahusu ziboreshwe ili waweze kuwa na utendaji mzuri wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na tuzo kwa viongozi wanaofanya vizuri katika kila halimashauri ya wilaya
  • Serikali ije na mpango endelevu wa semina na mafunzo yatayowajengea uwezo wa kiutendaji kama ilivyo kwa wengine
  • Uanzishwe mpango wa kuwaalika katika maeneo muhimu kama ikulu na bunge walau mara mbili katika kipindi cha uongozi wao kama sehemu ya motisha
  • Wapewe motisha ya vyombo vya usafiri
  • Wapewe haki ya kiulinzi itakayo wasaidia kuwa na uhakika wa kiusalama hata kwa sheria ya ulinzi shirikishi
Hitimisho
Ushiriki wa viongozi wa serikali za vijiji ,vitongoji na mitaa ni muhimu sana kwasababu wao hushughulikia moja kwa moja mambo ya wananchi na ni jambo la msingi sana katika kujiletea maendeleo yao katika vijiji na mitaa.

Mazingira wezeshi kwa viongozi yatawafanya kuwahamasisha wanachi kuwajibika, watejenga shule serikali italeta waalimu, watajenga hospitali serikali italeta wataalamu na kadharika, kumbe tuwakumbuke katika kuumega mkate kwa manufacturer ya taifa zima.
 
Andiko zuri sana. Sasa mbona viongozi wa kijiji wanaoajirika kisheria wanalipwa mishahara mkuu? Au unataka hata wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji walipwe mishahara?
 
Exactly tunataka walipwe pia walau , mbunge kwa mfano analipwa na amepigiwa kula, raisi amepigiwa kula analipwa , sheria ya nchi katika ujira imeelekeza mshahara wa kima cha nchi kwa wafanyakazi hadi wale wa majumbani lakini viongozi hawa wanasahaurika kabisa kama sio wafanyakazi, lakini kimsingi ni wafanyakazi kazi wa serikali hivo wanapaswa kuwa na atleast malipo kidogo au posho ya uhakika
 
Back
Top Bottom