Tuwaite watoto wetu majina ya asili

Tuwaite watoto wetu majina ya asili

Tuache kuvaa nguo za pamba pia na turudie asili yetu ya kuvaa magome ya miti

Mchango huu umetoka nje kabisa, ina maana kuwa na jina la kitaliano au kiingereza ndo maendeleo? Kuamini hivyo kunaonesha jinsi ambavyo tumetekwa na kuwa watumwa. Kuwa mtumwa siyo lazima uvalishwe NIRA!! Ni tatizo lililoenea. Utakuta sehemu ya kuoshea magari inaitwa California car wash, Miami blah blah!? Ukiita Msata au jina kijijini kwenu linakuwa na historia nzuri zaidi.
 
Tatzo bongo tunaaminishwa kuwa wazungu wanapesa na watatusaidia kutuondoa kwenye wimbi la umasikini kuanzia kwenye familia zetu hadi taifa.
 
TUNAPOTEA NA PIA TUNAPOTEZA ASILI JAMAN. TAZAMA WACHINA, WAHINDI,WACHAGA , WAHAYA, WAKITAJA KITOSHELEZO TU UNAWAJUA KUWA NI KUTOKA WAPI. UKOO SIYO BABU NI CHAPA YA KUWATAMBULISHA.
 
Huu ni wakati digital bwana!
Kwahiyo Wahindi,Wajapan,Wachina,Wakorea hawamo kwenye kizazi hiki cha digital ?? Mbona majina yao ya asili wanayatumia kwa 100% na technology yao ipo juu kwa sana tu.....tatizo tumezoea ku-copy kila kitu pasipo kutafakali....kwanza nikueleze majina ya ki-Africa ni mazuri sana na yapo unique na yanatukuza asili yetu,,,najivunia u-Africa wangu till the end of this world,,,big up Okoth P'Bitek,Chinua Achebe,Bujaga Izengo Kadago na wengineo wenye majina mazuri kama hayo,,,viva Africa ,viva Tanzania, viva my black colour....
 
Kweli mkuu, hii ni mbaya sana. Kama huyu msanii alie jifungua juzi, amenichafua kweli, kamwita mtoto wake cookies! Ni ujinga sana, kwanini asimwite majina Mazuri tu ya kiswahili kama bahati, furaha etc, au ya kikabila.
Teh basi pole, tunza hayo majina ukipata wanao utawapa
 
Watoto wengine wanakosaga Amani na hayo majina ya asili mengine ni mabaya kwakweli, nmesoma na mdada mmoja mzuriiii anaitwa "mashavu" yani ikifika muda wa kutaja jina lake dada wa watu anakosa pozi kabisa inaonekana hapendi jina lake kisa cha kumnyima mtu Amani?!
 
mimi naona tusiwape ya kizungu wala ya kilugha bali tuwape ya KISWAHILI mfano NEEMA, DAIMA,BARAKA, BAHATI, PENDO, SHUKRANI, SUBIRA, MASHAKA n.k
 
Siku hizi imekuwa kawaida watoto kuitwa majina kigeni kama Joyce, Jocktan, Mary,John,Abdallah,Mohammed, Yusuphu huku tukiacha majina yetu ya asili yaliyotumiwa na wazazi wetu, haiwezekani nimetembelea shule nyingi unakuta mtoto anatumia majina yote ya kigeni mfano Michael John, Joseph tunaacha majina ya asili yetu yanapotea huku tukiendelea kutukuza majina ya kizungu.

Hakikisha mtoto anatumia jina la asili la ukoo wako kwa kufanya hivyo tutazidi kudumisha majina ya kiafrika yanayopotea kwa kasi vile vile tuhakikishe watoto wetu wanafahamu lugha za asili kama Kikurya, Kisukuma, Kinyakyusa, Kinyamwezi sio mtoto anakuwa mpaka anafika mkubwa hata hajui lugha yake ya asili pelekeni watoto wakakae na bibi zao hasa nyakati za likizo wakajifunze lugha na ni vizuri kuwapeleka wakiwa wadogo zaidi maana itakuwa rahisi kushika lugha.

Wewe ni mpumbavu. Huwezi kulazimisha bichwa lako tupu liwe kipimo kwa kila mtu. Kama unataka kuwaita watoto ita wa kwako. HUWEZI KUWA MWAMUZI WA MAISHA BINAFSI YA WATU.

PUMBAVU SANA KAZI KUJAZA NAFASI MTANDAONI TU. ETI WATOTO WAWE MALI YA UMMA.
 
Mzee una akili sana. Duniani watu wakitaja majina yao utajua huyu mkolombia, mchina, mdenish ila sisi waafrika tunaiga majina ya watu utamsikia mtu anakutajia jina halielekei hata kuwa jina mara Precious, Emaculate ujinga mtupu.

Mimi mwanangu amezaliwa ulaya, nimeishi naye Dar kwa muda ambapo lugha ni kiswahili na kiingereza lakini nimefanikiwa kumfundisha kilugha. Usisahau mama yake ni mzungu na dogo anaongea kilugha chao pia.

Kiswahili nimekataa kumfundisha maana mazingira yatamlazimisha ila hayo mazingira hayawezi kumlazimisha aongee kilugha changu mbele ya safari.

Lazima tujitambue waafrika
 
Utakuta mijina kama-
1. Johnson McDonald
2. Jimyson Adamson
3. Exavery Duncan
4. Viana Gratian
5. Dustan Milton Davis
6. Christopher Dalton
7. Mike Louis
8. Nickson Mark
...................

Wakuu Mimi naitwa Emmanuel Massawe..
 
Wewe ni mpumbavu. Huwezi kulazimisha bichwa lako tupu liwe kipimo kwa kila mtu. Kama unataka kuwaita watoto ita wa kwako. HUWEZI KUWA MWAMUZI WA MAISHA BINAFSI YA WATU.

PUMBAVU SANA KAZI KUJAZA NAFASI MTANDAONI TU. ETI WATOTO WAWE MALI YA UMMA.
wewe si mlokole wewe? mbona matusi mengi hivi? mimi nilikua nadhani watu wanaoendekeza sana dini I.Q yao ndogo na leo nazidi kuthibitisha
 
Kuna majina ya kiswahili wenye nayo hawayapendi kwa mfano unamkuta kijana mtanashati anaitwa Haleluya, Ebenezer, Tumsifu..... Sio rahisi kulikubali jina Lake kwa sababu anaona kama linamfedhehesha. Wengi sana wamebadili majina wakiyaona majina YAO ya kiswahili ama kikabila kuwa ni mabaya. Binafsi nina jina langu la kabila letu, mwanzoni nilikua nalichukia na kuona aibu kulitaja, lakini baadaye nikatokea kulipenda sana kwa sababu that's my name no matter what. Simshauri mtu amwite mwanae jina la kikabila wala kigeni. Mtoto ni wako na maamuzi ni yako ila chunga asije kukuchukia baadaye kwa jina utakalompatia
 
Mm mwanangu nimempa jina la babu...."angwenji".
 
Nilishawahi kutoa uzi kama huu humu mwaka juzi. Sio kulazimisha bali kiuwasihi watu watumie majina yao ya asili kiswahili au kilugha kuenzi utamaduni wao.

Hakuna nchi inayoongoza kwa kuiga kila kitu Africa kama Tanzania. Watu wa West Africa waligundua hili mapema sana na huwezi kuta upuuuzi wa mtu kuitwa Kelvin Edgar James au Mohamed Ali Abdul hata wawe wamezaliwa Ulaya huwa wanatumia majina yao, angalia wachezaji mpira wa Nigeria waliotoboa wote wanamajina yao. Sisi sababu tunataka uzungu sana tunafanya kila jitihada majina yetu yapotee kabisa tubaki na ya kigeni ili tujione wazungu. Hapo Kenya tu au Zambia Bado wanaenzi majina yao sio rahisi mtu kuwa na surname ya kigeni let alone his first name

Watanzania ndio watu pekee wakienda nje kama anaitwa Musa atasema anaitwa Moses kama anaitwa Hashimu Thabiti atasema anaitwa Hasheem Thabeet. Smh
 
Molembe kwa Watu wa Ujiji kigoma maana yake Jivi la mwisho.
Sasa mkuu nikikuita Jivi la Mwisho mtaani si utaanza kirusha ngumi au?

Chunguzeni majina yenu kabla ya kuyatumia. Hata yule Matola hajajua mpaka leo kuwa Matola kwa Kihehe ni Vinyweleo vya chini ya Makende!
Ni hatari sana haya majina.
Unajua wewe ni mpotoshaji, ndio maana wa ajabu na mambo yako ya ajabu ajabu.

Mie naitwa ntamaholo kwa kikwetu, maana yake hakuna amani. Hii inatosha kujulisha kuwa nilizaliwa wkt aman imetoweka.

Sasa kosa unalolifanya, ni kuchukua jina langu na kulipeleka kwa lugha za makabila mengine. Utaishia kupata matusi tu.

Mfano majina yetu ya Nkundimana, ukiyapeleka kwa kihaya ni matusi lkn kwetu ni nampenda Mungu.
 
Last edited by a moderator:

Sasa nakuuliza hao wazazi wako kukuchagulia jina la "Shari" wanakutakia mema? Yaani ktk majina yooooote duniani Wakaamua Kukuita "vurugu"! Teh teh teh.
Hizi pombe za Moshi hazifai Kunywa wakati wa kuchagulia watoto majina.

We hata mtu akitaka kukuajiri inabidi akubatize upya. Na wafanyakazi wenzako lzm wakatishe hilo jina.
Wakuiite mtama.

Acheni kuwapa watoto wenu majina ka dawa za kienyeji.
 
Back
Top Bottom