Kwa taarifa zilizopo maambukizi yameongezeka hivi karibuni. Leo nimemsikia mkuu wa wilaya ya karatu akilizungumzia hili kwa wilaya yake. Kipekee amesisitiza halmashauri yake kuongeza mabango ya kampeni ya kujikinga na UKIMWI.
Hata hivyo, kampeni za kujikinga na UKIMWI zinapaswa kwenda sambamba na kampeni dhidi ya vilevi. Watu wengi sasa hivi wanao uelewa wa kujikinga na UKIMWI, tatizo linabaki pale tunapokuwa tumeshatumia vilevi. Under influence ya vilevi ni rahisi mtu kufanya maamuzi yatakayoharibu maisha yake yote.