Tutegemee Bunge lijalo kurushwa LIVE?

Kalamu ya Mwananchi

Senior Member
Oct 27, 2020
100
550
Ukweli ni kwamba bunge lijalo halina madhara. Ni bunge kibogoyo.

Kwahiyo hata likirushwa live redioni au kwenye tv, bado halitakuwa na effect mbaya kwa serikali. Kwasababu wale wakosoaji/waibua mijadala ambao wangepata airtime kama bunge lingekuwa live, kipindi hiki hawapo. Wamebaki wagonga meza na waimba mapambio ya serikali.

Sana sana inaweza kutumika ili kujipa credit kuwa Tanzania bado kuna 'demokrasia'.

So tutegemee bunge lijalo kuwa live?
 
Kusifia,kuomba na kumwabudu binadamu mwenzetu,hiyo dhambi haitawaacha salama.Yale ya mtukufu Moi yanajirudia.Hakuna jipya chini ya jua.
 
Ni bunge la kidada wa uani. Ni porojo na udaku. Hata yule spika dhaifu kachukua fomu kugombea usabuwufa tena. Akipita, litakuwa bunge la ukuda. Halina madhara kwa Serikali. Hivyo litaoneshwa mubashara wajioneshe walivyojipaka rangi midomo na kufuga kucha ndefu.
 
Hahaha hawatarusha hata wao CCM wanajijua hawawezi kujenga hoja.

Wakirusha utasikia naunga mkono hoja.
 
Kwa kuwa litakuwa Bunge la "Praise & worship" kwa Mtukufu.

Na kwa kuwa Jiwe, hakuna kitu anachoabudu zaidi ya hicho cha kusifiwa na kuabudiwa, basi tutegemee Bunge lijalo kuwa LIVE, kwa kuwa litakuwa limejaza watu Wa kusifu na kuabudu pekee
 
Naipongeza sana Serikali yangu sikivu ya CCM, lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhili kama sitamshukuru & kumpongeza sana Rais na mwenyekt wangu wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...hizo sentensi mbili zitavunja rekodi kwa kutamkwa mara nyingi zaidi bunge "kibogoyo" lijalo!!!.
 
Nachukia sana Demokrasia ya mavyama mengi, ndio inayotupa umaskini Africa

Mfumo wa vyama vingi ufutwe
Hili taifa sio la wasomi bado, wajinga nj wengi hivyo wanaweza fanya maamuzi ya hovyo
 
Hilo halitokei na hawalifanyi,suwbuwtuuw ,weeh ,waonyeshe bunge live,mijalada na mikaburasha hawawezi ,maana ni aibu ,halafu bunge lenyewe halina nguvu yeyote lipo lipo tu ,kupitisha siku,bunge la Tanzania halina nguvu ,huo ndio ukweli wakitaka wasitake,labda nguvu ya kumfukuza mpinzani bungeni,kumnyima posho mpinzani ,nguvu hiyo walikuwa nayo,sasa haipo ni wao kwa wao mtoto wa mjomba na shangazi.
 
Ni bora lionyeshwe Live,maana wanaoharibu Bunge letu kwa kuropoka hovyo,kupiga watu ngumi nakususasusa kama wanawake,wote hawapo.walilitia aibu Bunge letu.
sasa litakuwa Bunge la kujadili hoja kwakina na kwa hoja.
 
Back
Top Bottom