Edo Kumwembe " Tuachane na bunge live, tutazame Sultani"

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Hivi kwa nini mjadala wa Bunge kurushwa live (mbashara) unarudi? Sielewi. Juzi nilisoma mahali kaka yangu, Nape Nnauye akijichanganya kuhusu lile tamko lake la mbwembwe kuzuia Bunge kwenda live. Amepiga siasa akidai sasa inabidi liwe live. Nape yule yule mmoja.

Sijali sana alichosema wakati ule wala anachosema sasa. Waliodai Bunge liwe live wakati ule hawakujua kama mambo yangekuwa yalivyo sasa. Sidhani kama kwa sasa wanalihitaji liwe live. Binafsi sitaki liwe live.

Tuna bunge ambalo wachezaji mahiri wa Simba wamehamishwa kwenda Yanga. Kwa nini liwe live, ili iweje? Tulihitaji bunge live tukiamini watu kama yule ‘mura’ wa Ukonga atakuwa katika jezi zile zile na ukali ule ule.

Kwanini bunge liwe live wakati mzee wa vijisenti habishani tena hoja za kisomi na Tundu Lissu huku Mama Anna Makinda akikesha nao mpaka saa saba usiku akiamua pambano walau kwa kujitahidi kuleta uwiano?

Kwa nini bunge live wakati Ninja hataweza kuvaa tena kofia yake ya kininja na kuihenyesha Serikali. Siku hizi yuko upande wao.


Kwa nini liwe live wakati Mzee Six hayupo tena? Sawa, dakika za mwisho hakueleweka lakini dakika zake za mwanzo za uspika aliwaacha kina Zitto wakue kisiasa kwa kuruhusu akili zao zifanye kazi. Kwa nini bunge liwe live, ili tuone nini?

Zama za kina Deo Filikunjombe na Zitto kukesha wakilinda mafaili yao ya Escrow zimepita. Zitto anaishia kulalamika tu katika Twitter kwamba Trilioni kadhaa zimepotea.

Zamani hii habari ingeenda bungeni halafu watu tukasogea katika vijiwe vyetu vya mvinyo na nyama choma kwa ajili ya kutazama pambano kali kutoka Dodoma.

Zama hizo sasa zimepita, mnataka bunge liwe live ili iweje? Tusikilize hoja za dada anayetaka wanaume wapimwe kama wametahiriwa kabla ya kuingia geti la bunge?

Acha bunge liende kimya kimya mpaka mwisho wa safari. Acha walio bize na Ligi Kuu ya England waendelee na utamu wake.

Acha kinamama na watoto waendelee kutazama tamthiliya ya Sultani. Hata kama bunge hili lingekuwa live bado watu wasingehangaika na rimoti.

Tuuzike huu mjadala. Tuachane nao. Nawakumbusha tu wale wenzangu katika yale mambo yetu kwamba wikiendi ijayo kwenye Ligi Kuu ya England ni Manchester United na Liverpool. Katika fainali ya kombe la Ligi ni Man City na Chelsea. Maisha bado matamu.
 
Nikukumbuka siku ile Mh Nape anajenga hoja bunge lisirushwe live, siamini kama leo angegeuka. Alienda mbali sana, mpaka akatolea mfano wa Mabunge ya Ulaya. Hakika niliumia sana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom