Leo kamati kuu ya CCM inakutana kuijadili rasimu ya katiba. Baada ya kikao hicho tutarajie yafuatayo kuwa ndio maoni yao ya CCM
1)kupinga muundo wa serikali tatu na kupendekeza tuendelee na serikali mbili
2)kupinga matokeo ya urais kupingwa mahakamani
3)kupinga kufutwa kwa viti maalum
4)Tuendelee kuorodhesha na kujadiliana mapendekezo yote ambayo kuna uwezekana wa CCM kuyakataa, naomba kuwakilisha jamvini!
hii katiba imeandaliwa na ccm yenyewe wewe kijana kuipinga ngumu
Na kama CC ya CCM ikipinga hayo mambo uliyoyaorozesha na ammbayo hujayaorozesha huo utakuwa ni mtaji mkubwa wa kisiasa kwa CHADEMA kwenye majukwaa ya siasa,tusubiri maamuzi yao tuone!
Leo kamati kuu ya CCM inakutana kuijadili rasimu ya katiba. Baada ya kikao hicho tutarajie yafuatayo kuwa ndio maoni yao ya CCM
1)kupinga muundo wa serikali tatu na kupendekeza tuendelee na serikali mbili
2)kupinga matokeo ya urais kupingwa mahakamani
3)kupinga kufutwa kwa viti maalum
4)Tuendelee kuorodhesha na kujadiliana mapendekezo yote ambayo kuna uwezekana wa CCM kuyakataa, naomba kuwakilisha jamvini!
Waziri kutokuwa mbunge jambo zuri ila waache open hata kama Mbunge anaweza apewe.
KUNA MENGINE ZAIDI YA HAYO HAPO JUU:
Lakwanza kabisa watakataa muundo wa serikali tatu!
Watasema Spika ni lazima awe mbunge
baraza la mawaziri lisiwe na kikomo
bora kubaki na katiba ya sasa
hawaungi mkono spika kutokuwa na chama
Watasema mawaziri lazima watokane na wabunge
NATABIRI lakini msiniite mchawi.......hii katiba mpya itakuwa na mgogoro sana kabla ya uchaguzi wa 2015......pia natabiri kama jamaa watakuja na hoja hizo hapo juu wananchi wataikataa katiba mpya!!! ni utabiri tu!
Kwani msimamo wa chadema night upi? Wanataka serikali ngapi? Viti maalum vowepo au la? Maana naona viongozi wamekaa kimya...