Tutarajie haya baada ya kikao cha cc ya CCM

Chang'o

Senior Member
Dec 21, 2012
105
21
Leo kamati kuu ya CCM inakutana kuijadili rasimu ya katiba. Baada ya kikao hicho tutarajie yafuatayo kuwa ndio maoni yao ya CCM
1)kupinga muundo wa serikali tatu na kupendekeza tuendelee na serikali mbili
2)kupinga matokeo ya urais kupingwa mahakamani
3)kupinga kufutwa kwa viti maalum
4)Tuendelee kuorodhesha na kujadiliana mapendekezo yote ambayo kuna uwezekana wa CCM kuyakataa, naomba kuwakilisha jamvini!
 
hakuna mtu hapo ccm kwa sasa atakayekubaliana na Rasimu ila tutarajie migawanyiko na makundi mengi kuongezeka hasa ukizingatia udhaifu wa uongozi wa mwenyekiti na timu yake kumudu kashikashi za makundi.
 
Leo kamati kuu ya CCM inakutana kuijadili rasimu ya katiba. Baada ya kikao hicho tutarajie yafuatayo kuwa ndio maoni yao ya CCM
1)kupinga muundo wa serikali tatu na kupendekeza tuendelee na serikali mbili
2)kupinga matokeo ya urais kupingwa mahakamani
3)kupinga kufutwa kwa viti maalum
4)Tuendelee kuorodhesha na kujadiliana mapendekezo yote ambayo kuna uwezekana wa CCM kuyakataa, naomba kuwakilisha jamvini!

Na kama CC ya CCM ikipinga hayo mambo uliyoyaorozesha na ammbayo hujayaorozesha huo utakuwa ni mtaji mkubwa wa kisiasa kwa CHADEMA kwenye majukwaa ya siasa,tusubiri maamuzi yao tuone!
 
Mkuu hayo uliyoorodhesha ndo yatakayopendekezwa na CC ya CCM kwani tayari mambo yameshavuja na yanajulikana .Ila kuna mengine ambayo hukuyataja kama; Spika ni lazima awe mbunge,baraza la mawaziri lisiwe na limit kikatiba ingawa wamependekeza wasiwe wabunge.Pia kamati ya ulinzi na usalama iliyopendekezwa na tume pamoja na majukumu yake wao wameipinga na wanataka mfumo uliokuwepo uendelee...mku hizo sii tetesi ni live.
 
Na kama CC ya CCM ikipinga hayo mambo uliyoyaorozesha na ammbayo hujayaorozesha huo utakuwa ni mtaji mkubwa wa kisiasa kwa CHADEMA kwenye majukwaa ya siasa,tusubiri maamuzi yao tuone!

slaa alitaka mjitoe,hataki
 
Kwani msimamo wa chadema night upi? Wanataka serikali ngapi? Viti maalum vowepo au la? Maana naona viongozi wamekaa kimya...
 
Msiwe wavivu wa kufikiri, kama ccm watapendekeza na CDM nao watapendekeza na CUF watapendekeza mwisho itakuwa nini??? kumbuka tume toka mwanzo ilitoa angalizo kuwa mchakato ni marufuku kutekwa na vyama vya siasa, kinachotawala ni maoni ya watanzania kutegemea na wingi wao kwa kila pendekezo mfano wengi wanataka serikali tatu.CCM watapinduaje??? tafakari utabaini
 
CCM wamepigwa bao wakubali yaishe vinginevyo kina KINANA wanataka kuleta ya SOMALIA hapa kwetu.
 
Waziri kutokuwa mbunge jambo zuri ila waache open hata kama Mbunge anaweza apewe.
 
Hili la serikali tatu lazima wa lipinge kwani halikuanza leo hata Baba wa taifa hili alionya juu ya serikali tatu na watasimamia hapo kwenye kauli ya mzee Julius Nyerere na ikumbukwe pia John malecela aliisha oja joto ya jiwe juu ya swala hili la serikali tatu.
 
Mimi kwa hili sitaki ushabiki wa vyama.Nataka nijue kwamba hivi ni kwa nini kama tunataka muungano tusiwe na serikali moja? Hebu fikiri;

1.Tuwe na wabunge wa tannganyika kila jimbo wawili (mwanamke na mwanaume)

2.Tuwe na wabunge wawili kwa kila jimbo la Znbar (mwanamke na mwanaume)

3.Tuwe na wabunge wawili wamuungano kutokata Tanganyika (mwanaume na mwanamke)

4. wabunge wawili wa muungano kutoka zanzbar (mwanamke na mwanaume)
5 mawaziri wa tanganyika na manaibu wao

6.Mawaziri wa zanzbar na manaibu wao

7.Mawaziri wa muungano na manaibu wao

8.Ikulu ya tanganyika

9.Ikulu ya zanzbar

10.Ikulu ya muungano

11.Uchaguzi wa Tanganyika, wa Zanzbar na wa Muungano.

Hivi gharama zote hizi ni kwa maslahi ya nani?Kwa nini tusiwe na serikali moja kama tunataka muungano! Tafakari.
 
Leo kamati kuu ya CCM inakutana kuijadili rasimu ya katiba. Baada ya kikao hicho tutarajie yafuatayo kuwa ndio maoni yao ya CCM
1)kupinga muundo wa serikali tatu na kupendekeza tuendelee na serikali mbili
2)kupinga matokeo ya urais kupingwa mahakamani
3)kupinga kufutwa kwa viti maalum
4)Tuendelee kuorodhesha na kujadiliana mapendekezo yote ambayo kuna uwezekana wa CCM kuyakataa, naomba kuwakilisha jamvini!

KUNA MENGINE ZAIDI YA HAYO HAPO JUU:
Lakwanza kabisa watakataa muundo wa serikali tatu!
Watasema Spika ni lazima awe mbunge
baraza la mawaziri lisiwe na kikomo
bora kubaki na katiba ya sasa
hawaungi mkono spika kutokuwa na chama
Watasema mawaziri lazima watokane na wabunge

NATABIRI lakini msiniite mchawi.......hii katiba mpya itakuwa na mgogoro sana kabla ya uchaguzi wa 2015......pia natabiri kama jamaa watakuja na hoja hizo hapo juu wananchi wataikataa katiba mpya!!! ni utabiri tu!
 
katika kufanya yote hii nimegundua kuwa binadamu ni kiumbe wa ajabu ana utawezaje kuwasemea watu eti unaema unatabiri,unatabiri kitu ambacho kipo kwenye vichwa vya wenzake kazi bado inaendelea.
 
KUNA MENGINE ZAIDI YA HAYO HAPO JUU:
Lakwanza kabisa watakataa muundo wa serikali tatu!
Watasema Spika ni lazima awe mbunge
baraza la mawaziri lisiwe na kikomo
bora kubaki na katiba ya sasa
hawaungi mkono spika kutokuwa na chama
Watasema mawaziri lazima watokane na wabunge

NATABIRI lakini msiniite mchawi.......hii katiba mpya itakuwa na mgogoro sana kabla ya uchaguzi wa 2015......pia natabiri kama jamaa watakuja na hoja hizo hapo juu wananchi wataikataa katiba mpya!!! ni utabiri tu!

mkuu kwani upo kwenye vichwa vyao hizi akili zingine vipi mbona unawasemea.
 
Kwani msimamo wa chadema night upi? Wanataka serikali ngapi? Viti maalum vowepo au la? Maana naona viongozi wamekaa kimya...

Soma gazeti la Mwananchi la leo utaona kama wamekaa kimya au wameshafunguka. Unaweza kulisoma hata online.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom