Tutamlinda Kikwete pia kwa kutumia nguvu za umma

.........

Baadhi ya waTanzania hao walidai madai yanayotolewa na vyama vichache kuwa itumike nguvu ya umma kumuondoa Mheshimiwa Raisi Kikwete madarakani ni ya makundi ambayo yamepoteza muelekeo na sasa wanataka kulisambaratisha Taifa hili lenye utulivu na amani na kuliingiza kwenye vurumai lisilojulikana mwisho wake.

WaTanzania hao ambao wengi wao wanasema sisi ni wengi kuliko walioko kwenye hayo makundi wataonyesha ni namna gani nguvu za umma zinatumika kuhakikisha Raisi waliemchagua anaendelea kubaki kwenye madaraka kwani uhakika kuwa wingi wao ndio uliomueka madarakani upo palepale na ushindi uliopatikana sio wa kubabaisha au kupapasa ni ushindi uliotangazwa na tume na ambao ndio unaotakiwa uheshimiwe.

Sasa kutokea kwa vishambenga ambavyo vinajitutumua kwenye majukwaa kuwa peoples power itafanya kazi kumuondoa Kikwete madarakani ,wananchi hao walisisitiza madai yao kuwa wanawasuburi hao ambao watakuwa mstari wa mbele kuongoza nguvu za umma na wajiandae kukutana vilevile na nguvu za Umma upande wa Uraisi ,na wamesema watajuta kuzaliwa maana wao ni wengi sana na watakuwa hawana mswalie mtume ni kumlinda Kikwete tu mpaka kieleweke ,lakini hawatamuacha Raisi waliemchagua kuchezewa na watu wachache.

Pole sana unaweza endelea kuongea upuuzi wako kwa sababu kitendo cha kubadili matumizi ya jinsia si kidogo!! Wengi huwa kama ulivyo sasa.
 
Hivi ugumu wote wa maisha huu,serikali kuparaganyika,ufisadi uliokithiri,mishahara midogo,ukosefu wa walimu na vifaa vya kufundishia,uhaba wa dawa na vifaa tiba,shida ya maji,bei ndogo ya mazao kwa wakulima,serikali kuendekeza anasa na matumizi mabaya ya kodi za wananchi;hawa wanaojiita CCM hayawagusi?au ndo upumbavu....!
Tatizo hamfuati uzazi wa majira baba wa Taifa alikuwa akigusia hili kwenye mikutano yake lakini hamukumusikiliza sasa ,unajua kasi ya population ya Tanzania ? Tanzania hakuna shida hiyo unayoisema mbona vijijini maisha ni mazuri tu.
 
tuondolee upupu humu labda alindwe kwa nguvu ya mafisadi ila sio nguvu ya umma kwa lipi alilolifanyia taifa hadi wamlinde? Tena ukitaka kujua wengi wamejichokea (52% ya wale ambao hawakupiga kura)ambao walimstahi kwa kuamua kuacha kupiga kura kuliko kupigia upinzani bora ungekaa tu kimya kuliko kujiongelesha na kujaribu kupima upendo wa wananchi dhidi ya serikali. Huu ni upepo mwingine ndio maana kinana alisema watashinda kwa zaidi ya 80% matokeo yake wakashinda kwa taaaaabu sana kwa 61% baada ya kuchakachua.
 
Pole sana unaweza endelea kuongea upuuzi wako kwa sababu kitendo cha kubadili matumizi ya jinsia si kidogo!! Wengi huwa kama ulivyo sasa.
Aloo usinifananishe na baba yako ,sio umemuona yeye kabadilisha matumisi ya jinsia ukafikiri watu wote wapo kama yeye!!
 
Yaani hapa kijijini nilipo sioni m2 wa kumtetea jk,asubui hii tayari kuna katoto umri 1yr kamekufa, kwa kukosa damu,wameombwa 20,000 hosp hawana matokeo yake wamepoteza,sera ya matibabu ya umri huo inasemaje?kwa mtaji huo nguvu ya umma utaitoa wapi?kwa taarifa huku vjjn wanaccm ndo hoi bin taabani,angalau wanamageuzi utakuta ni watu walio na kipato hivo wanaweza kupambana na maisha hata inflation ifike 100%
 
Tena hawa wanaojidai wataingia mitaani bila kuruhusiwa na Serikali iliopo madarakani kihalali, tutawaomba Serikali watuwachie tuwashughulikie ki mitaani.

Hawa "wanakaanga mbuyu" wenye meno tupo, tutatafuna.
 
tuondolee upupu humu labda alindwe kwa nguvu ya mafisadi ila sio nguvu ya umma kwa lipi alilolifanyia taifa hadi wamlinde? Tena ukitaka kujua wengi wamejichokea (52% ya wale ambao hawakupiga kura)ambao walimstahi kwa kuamua kuacha kupiga kura kuliko kupigia upinzani bora ungekaa tu kimya kuliko kujiongelesha na kujaribu kupima upendo wa wananchi dhidi ya serikali. Huu ni upepo mwingine ndio maana kinana alisema watashinda kwa zaidi ya 80% matokeo yake wakashinda kwa taaaaabu sana kwa 61% baada ya kuchakachua.

Hapo ndipo utapojuwa ni nguvu za nani! Ule mkong'oto mliokula Arusha ni pati gazeti na kama mnataka kuona picha kamili, nyie anzeni tu!
 
hatimaye ule mwisho wa ccm umefika! Bravo kikwete, hatimaye kinafia mkononi mwako.
 
Nguvu ya uma itumike vizuri na isiwe ni kwa ajili ya maslahi ya wachache. na iyo amani na utulivu usiwe wa kuhubiri tu
Nguvu ya umma upi ambayo itaweza kukusanywa na Chadema ??? Na kuweza kummuondoa Raisi madarakani ,hivi mnaota au hawa jamaa wanatatizo la kufikiri ? Nawapeni kipimo ,na Chadema wajaribu tuone ,halafu mtaitisha nguvu hiyo wapi ? Maana kama ni nguvu ya Umma sehemu ni katika miji mikuu sehemu ambayo mawizara na maikulu yapo ,let us say Dar es salaam ,ambapo shughuli za serikali na mabalozi wapo ,hivi Chadema mnakubalika Dar ? Pangeni na kuyaweka mawazo yenu katika kipimo na sio mnakurupuka tu na nguvu za umma,hivi Chadema inakubalika Tz nzima ??? Msijidanganye kabisa ,naamini bado hatjaweza kuitisha nguvu za umma kwa upande wa Tanganyika bado sana ,mambo hutayarishwa ndio yakawa sio habari za hapa na pale mkakurupuka mtauliwa kama ngedere, Raisi nae anazo nguvu za umma na wapo tayari kumlinda.
 
Kipindi hiki tanzania inapita katika majaribu. Busara inahitajika kuliko kipindi kingine chochote. Hata kama Mh. Rais ni mdhaifu au ana madhaifu busara ichukue mkondo wake. Uhuru wa kupata na kutoa habari ???? watanzania wa leo wanasema wanachokitaka, kuongoza nchi si lelemama. Kuna tatizo, ndiyo, mambo hayaendi sawa ndiyo, tunalitatua vipi? Ni lazima tuwepo watu wa kati, "cooling system", Chadema na CCM Huenda kila mmoja wao anaamini anayoyafanya ni sahihi. Ipo haja na kila sababu ya kuwa na watu kati wenye msimamo wa kati. Ni kwa kujitokeza wasiofungamana na upande wowote na watakaoheshimiwa na pande zote ndipo shuluhu litapatikana. Mie naweza nikipata wenye msimamo wa kati na wenye (very nice and strong shockabsorberves) tuweweke sawa chadema, ccm, cuf na vyama vingine vya siasa. Tutaumia wote tusipopata muafaka sasahivi. Mie naogopa sana hali inavyoiona inakoelekea. Baadhi ya wananchi wanahasira sana sasahivi tena wa pande zote za kisiasa na zisizo za kisiasa. tunahitaji busara zaidi na watu wenye mrengo wa kati.
 
Tatizo hamfuati uzazi wa majira baba wa Taifa alikuwa akigusia hili kwenye mikutano yake lakini hamukumusikiliza sasa ,unajua kasi ya population ya Tanzania ? Tanzania hakuna shida hiyo unayoisema mbona vijijini maisha ni mazuri tu.

Ni kijiji gani unachokiongelea chenye maisha mazuri?
 
Hapo ndipo utapojuwa ni nguvu za nani! Ule mkong'oto mliokula Arusha ni pati gazeti na kama mnataka kuona picha kamili, nyie anzeni tu!

kumbuka pia mkong'oto walioupata maaskari kule tarime kwenye uchaguzi mdogo.
 
Watanzania walio wengi wameapa kuwa ikiwa patatokea kundi linalojidai kutumia nguvu za umma kumuondosha Raisi Kikwete nao pia watatumia nguvu za Umma kuhakikisha kuwa anabaki madarakani hadi mwisho wa awamu yake.

Baadhi ya waTanzania hao walidai madai yanayotolewa na vyama vichache kuwa itumike nguvu ya umma kumuondoa Mheshimiwa Raisi Kikwete madarakani ni ya makundi ambayo yamepoteza muelekeo na sasa wanataka kulisambaratisha Taifa hili lenye utulivu na amani na kuliingiza kwenye vurumai lisilojulikana mwisho wake.

WaTanzania hao ambao wengi wao wanasema sisi ni wengi kuliko walioko kwenye hayo makundi wataonyesha ni namna gani nguvu za umma zinatumika kuhakikisha Raisi waliemchagua anaendelea kubaki kwenye madaraka kwani uhakika kuwa wingi wao ndio uliomueka madarakani upo palepale na ushindi uliopatikana sio wa kubabaisha au kupapasa ni ushindi uliotangazwa na tume na ambao ndio unaotakiwa uheshimiwe.

Sasa kutokea kwa vishambenga ambavyo vinajitutumua kwenye majukwaa kuwa peoples power itafanya kazi kumuondoa Kikwete madarakani ,wananchi hao walisisitiza madai yao kuwa wanawasuburi hao ambao watakuwa mstari wa mbele kuongoza nguvu za umma na wajiandae kukutana vilevile na nguvu za Umma upande wa Uraisi ,na wamesema watajuta kuzaliwa maana wao ni wengi sana na watakuwa hawana mswalie mtume ni kumlinda Kikwete tu mpaka kieleweke ,lakini hawatamuacha Raisi waliemchagua kuchezewa na watu wachache.

Mwanangu shuka fupi kunja miguu mbu watakuuma
sasa umefika mahali umeidhalilisha hata NGUVU YA DOLA Kwamba imejifitini hadi haina ubavu wa kuilinda mamlaka iliyo madarakani mpaka watu walio pigika kwa kukosa huduma wastaafu walio pigika walimu waliokosa ajira umati wote choka mbaya kila kukicha afadhali ya jana......Mh hio ndiyo nguvu unayo itegemea? Basi huo ni wazimu mwana!
Ungetoa ushauri kwamba!; Utawala UVAE ROHO YA WANACHO KIBAINISHA CDM KWA VITENDO NA DHAMIRA YA KWELI ili KUWAONDOLEA/KUWAPUNGUZIA WANANCHI UMASKINI ULIOKITHIRI UJINGA NA UFISADI hapo mamlaka itadumu DAIMA

INSHAALAH!
 
Kwanini kusiwepo kura ya maoni, kama inawezekana. Matumizi ya nguvu kwa sasa hayajengi zaidi ya kuongeza na/kuleta uadui kwa wananchi wa kawaida.

Kuwepo na tume huru kusimamia maoni ya wenye nchi kupitia kura. Hapo tunaweza kupata mawazo ya wenye nchi walio wengi. Na maamuzi hayo yaheshimiwe na wote. Inaumiza kupoteza maisha ya wenye nchi bila ya kujali madhara yanayobaki nyuma.

Ninaonavyo mimi kunaweza kuwa na visasi ambavyo vitaacha makovu/vidonda visivyotibika. Sioni haja ya kuendelea kuua watu au kuuwana mitaani kwa kisingizio cha nguvu za uma kumwondoa au kumlinda alieyeko madarakani.

Tuepuke kutumiwa na makundi ya watu. Ukweli unajulikana kwa wengi. Tuchuje yote na tuamue kwa utashi wetu wenyewe.
 
CCM wakianza kutumia nguvu ya umma wanaweza wakajikuta wamebakia watu kumi tu; mazoea ya nguvu ya dola ni mazoea mabaya sana, hayaachiki kirahisi. Si umeona Ben Ali kule Tunisia, aliweza kuitumia dola for so loong lakini wananchi wana nguvu zaidi. Ila kwa mtindo wa kumwaga risasi hovyo hovyo kama Arusha nina uhakika hadi CCM walielewe hili somo la nguvu ya wananchi itamwagika damu nyingi sana na nahofia kuwa nyingine itakuwa ni ya watoto wa shule zetu ambao watawaiga wenzao wa Soweto!

CCM haiwezi kutumia nguvu ya umma. Not in a million years. Nguvu ya dola? hakuna shaka.
 
Katika mapambano yeyote lazima kuwe na resistance,sidhani kama hao wanaotaka kumuondoa madarakani wanafikiri itakuwa rahisi,JK ana watu wanampenda bado na si wachache ila pia si wengi kama ambao wanafikiri aende sasa......
 
Ndiyo maana unaleta argument za kimuembe^2.

"Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak."
 
Back
Top Bottom