Tutamlinda Kikwete pia kwa kutumia nguvu za umma

Mwiba angalia yaliyotokea Tunisia yanaweze kutokea Tz. pia. Watanzania wa mwaka jana si wa mwaka huu. Tumechoshwa na huu upuuzi wa serikali ya jk haina mwelekeo inaendeshwa kiholelaholela. Rais wako nchi imemshinda aachie tu awape watu wengine. Nchi ipo gizani hakuna maji naye kakaa kimya tu kama hayupo. Wamekausha hazina na uchaguzi sasa anashindwa ajue aanzie wapi. Aibuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!

Paukwa?
 
Watanzania tuko zaidi ya mil 40 ,waliojiandikisha jumla mil 19 ,waliopiga kura mil 8, waliomchagua kikwete mil 5(kwa mujibu wa tume).
Labda ni kweli unachosema kwa kutoangalia takwimu,ukiangalia takwimu hizo za nec nadhani usingeleta hoja yako hiyo kwani hujui hao mil 11 kwanini hawakupiga kura, na hao mil 20
Ambao hawakujiandikisha wako upande gani.
 
Alipoingia madarakani mwaka 2005, alikuwa na haiba na mvuto mkubwa sana na alipendwa na wananchi wengi wa Tanzania lakini sasa baada ya kutawala kwa miaka mitano hapendwi tena wala haonekani kuwa ana mvuto wowote!

Sasa anaongoza kwa mabavu na vitisho dhidi ya wananchi ambao wameisha gundua kuwa uwezo wake wa kuongoza na kusimamia shughuli za serikali ni mdogo sana!! Amethibitisha kuwa ni kiongozi dhaifu mwenye tamaa ya madaraka kwa jinsi alivyochakachua kura za wagombea wa upinzani na jinsi alivyotumia wake zake, watoto zake, mashekhe zake na kila mbinu ya giza katika kampeni.

Baada ya kushindwa katika medani za kisiasa kutokana na utendaji wake mbovu sasa amejificha nyuma ya dini yake na jeshi la polisi linaloongozwa na mtu wa kabila lake ambaye ni shemeji yake! Matendo yake yamenikumbusha maneno ya Mwl. Nyerere enzi za uhai wake kuwa kiongozi dhaifu atatafuta pa kujiegemeza ! alisema kiongozi wa namna hiyo atajificha ama nyuma ya kabila lake au nyuma ya dini yake!!!!
 
huna point wewe!wala hueleweki!sema ccm imetufikisha hapa tulipo ukianzia na uongozi wa hovyo nyerere mpaka kikwete!
 
...sidhani wanaosema hayo walikuwa tayari kwenda Arusha kumtetea rais wao tarehe 12. Hao watu labda wawe green guards lkn hawawezi kamwe kuwa na ari na dhamira kama ya People's power.. hii nakuhakikishia.

Hii ni kejeli 21 kwa zaidi ya 60 (plus 14)? indeed , people power!
 
Ndani ya miaka hii mitano ataondoka tu, we ngoja aendelee kuua watu wasio na hatia, ameanzia Arusha na sasa Wilayani Mbarali!

Miaka mitano ndio muhula wake wa mwisho na 2015 tutakuwepo pamoja kwenye helkopta kujaribu tena! hilo la yeye kuondolewa na nyie halipo!
 
Umeishiwa kabisa. CCM mpo wengi? Rais aliyeko madarakani ni wa Watanzania analindwa na Watanzania na kama hawafai Watanzania basi hafai hata WanaCCM. kwani maisha magumu kama kupanda kwa bei ya vitu inawafusa watu kwa kutumia vyama vyao? mwanaCCM ananunua umeme ofisi ya CCM? Rais kama hafai hafai tu. Kwa taarifa yako hao wanaCCM unaodhani kuwa watamtetea JK ndiyo wa kwanza kumtosa.
Basi Watanzania hao wako ni wa ajabu! Kumrejesha madarakani waliochosha? Pengine naweza kukubaliana nawe kuwa alikuwa afadhali kuliko kiongozi wa dini!
 
Mwiba unaionaje hali ya maisha inayomkabili mtanzania miaka 50 baada ya uhuru?kwa upande wako mambo shwari?fikiria pia wale waliopo vijijini
Hata Obama anaulizwa masuala hayohayo lakini Republican wanatumia katiba sio kuvunja katiba!
 
Nakushukuru Mkuu kwamba umeungana na mimi na kuona point ya uongozi wa hovyo wa Kikwete!!!! Naomba nikukumbushe kuwa yeye ndiye mlengwa wa thread hii, ila wewe pia waweza kuanzisha nyingine inayohusu uongozi wa Nyerere mpaka Kikwete na itapata wachangiaji!!!
 
arusha kama huelewi hakupingwa raisi ,mlikuwa mnapigania kiti cha umea huko ,mlikutana na walinzi wa amani maana mambo ya kuuteketeza mji wa arusha hamkufanikiwa ,ila hii mada inazungumzia raisi,nyimbo ambayo mnaimba siku hizi kuwa mtumie nguvu ya umma kumlazimisha raisi aondoke madarakani,aloo msije mkajaribu,ccm ni wengi sana na wamezagaa nchi nzima na nao wapo tayari kwa hilo ,anytime mkitangazza nao wanazuka kutoka kusiko julikana tayari kumlinda raisi wa nchi hii alietokana na chama chao.

kama tunisia tu!,
 
tuondolee upupu humu labda alindwe kwa nguvu ya mafisadi ila sio nguvu ya umma kwa lipi alilolifanyia taifa hadi wamlinde? Tena ukitaka kujua wengi wamejichokea (52% ya wale ambao hawakupiga kura)ambao walimstahi kwa kuamua kuacha kupiga kura kuliko kupigia upinzani bora ungekaa tu kimya kuliko kujiongelesha na kujaribu kupima upendo wa wananchi dhidi ya serikali. Huu ni upepo mwingine ndio maana kinana alisema watashinda kwa zaidi ya 80% matokeo yake wakashinda kwa taaaaabu sana kwa 61% baada ya kuchakachua.
Picha huwakilisha akili! Hivyo 61 ukilinganisha na 21 unasema ni taabu sana? sasa huyo anaependwa na wengi ni yupi?
 
Aloo usinifananishe na baba yako ,sio umemuona yeye kabadilisha matumisi ya jinsia ukafikiri watu wote wapo kama yeye!!
Na nafikiri ameanza kumfuata huyo baba yake ndio maana anajitowa hapa tumtambue!
 
Yaani hapa kijijini nilipo sioni m2 wa kumtetea jk,asubui hii tayari kuna katoto umri 1yr kamekufa, kwa kukosa damu,wameombwa 20,000 hosp hawana matokeo yake wamepoteza,sera ya matibabu ya umri huo inasemaje?kwa mtaji huo nguvu ya umma utaitoa wapi?kwa taarifa huku vjjn wanaccm ndo hoi bin taabani,angalau wanamageuzi utakuta ni watu walio na kipato hivo wanaweza kupambana na maisha hata inflation ifike 100%
Mpe kura Rostam au Manji kwani hao kwa mapesa wamewashinda hata hao wanamageuzi wako! Si unafikiri mapesa ndio kujali watu? Nasikia wazee wa Ismail bado wanadaiwa 5000 za jeneza!
 
CCM wakianza kutumia nguvu ya umma wanaweza wakajikuta wamebakia watu kumi tu; mazoea ya nguvu ya dola ni mazoea mabaya sana, hayaachiki kirahisi. Si umeona Ben Ali kule Tunisia, aliweza kuitumia dola for so loong lakini wananchi wana nguvu zaidi. Ila kwa mtindo wa kumwaga risasi hovyo hovyo kama Arusha nina uhakika hadi CCM walielewe hili somo la nguvu ya wananchi itamwagika damu nyingi sana na nahofia kuwa nyingine itakuwa ni ya watoto wa shule zetu ambao watawaiga wenzao wa Soweto!

CCM haiwezi kutumia nguvu ya umma. Not in a million years. Nguvu ya dola? hakuna shaka.

Watanzania tutakuwa wajinga mtu anaposema nenda kapiganeni na wenye silaha huku yeye akibaki kiririni na tuweke rehani roho zetu mikononi mwa viongozi wa namna hii! Tuliona kule Zanzibar hadi viongozi walipoacha kauli za kulala barabarani na kutumia busara ndio visiwa vikawa na amani.
 
Sikilizeni watu wasiokuwa na uwezo hata mdogo tu wa kufikiri. wadau hapa JF tunazungumzia uchumi wa nchi na jinsi watawala wanavyoshindwa kuwajengea wananchi mazingira ya kupata maisha bora. Jaribu kuwa rational na objective hapa sio swala la kulinda viongozi wa chama au serikali kwa nguvu ya umma. Kweli maisha ya kutegemea mjomba ndio yanakufanya kuwa oblivious wa mambo.. Pole
That ammounts to removal of the President? Hivyo Tanzania tangu iwe huru sasa ni miaka mitano tu?
 
Vijijini mbona mbali?hapa mjini maisha yamekua tyt sana,gas ya kilo 6 kwa sasa ni 30000/= kutoka sh 10000/= ,unga wa sembe kwa sasa kilo sh 800 toka 500,huyo anaetaka kuitetea csiem anapata huduma wapi?
Bajabiri una umri gani kadogoo?
 
Mwiba wewe ni fisadi tu, kila wakati unatetea uovu. Raisi ambaye hawezi kuwakemea wezi na Mafisadi anatakiwa kushauriwa mshauri basi au la!
endelea kutetea amgalia picha hizi hapa maisha bora kila Mtanzania

Haya ndio yaliyomfanya aamuwe kuutaka urais ili apigane nayo? Hebu leta picha za raha za zamani!
 
We Mwiba usimdanganye Jk. Msaada aliobaki nao ni wanajeshi na mabomu. Risasi za moto, mabomu na mizinga. Lakini upande wa watu wanaoweza kukubali kujitoa kumfia hana kabisa. Mambo yakiharibika wapenzi wake ikiwa ni pamoja na wewe mtakimbia nchi (Mna uwezo wa kutoroka kwa helikopta na mashangingi yenu ya bullet proof). Watoto wenu mlishawatanguliza nje ya nchi ndiko wanakosomea. Akaunti zenu za benki ziko Uswizi. Mnazo passport mbili. Ndio maana mmekuwa mkipigania dual citzenship ili mambo yakiharibika mkimbilie hiyo nchi ya pili. Mwahego Jk nakushauri usimsikilize Mwiba ni mnafiki, patana na wananchi sasa. Patana na mshitaki wako kabla hujachelewa. Mambo yakiharibika hutaona mtu miongoni mwa hawa wanaokuimbia mashairi ili waendelee kunufaika. Wote watakukimbia!!!!!!!!
 
Kuna tatizo sugu la kiitikadi za imani za dini tanzania ambalo ndilo linaiua hii nchi. kilichobaki hivi sasa ni kunyosheana vidole tu na kila upande unavutia kwake. JK na kundi lake wanaamini kuwa wakiristo wamefaidika sana na serkali kristo iliyotangulia na hivi sasa ni jukumu lao kuweka serkali islam yenye manufaa kwa waislam.
Siyo udhaifu binafsi wa JK bali ni msimamo wa kiitikadi ndo uliotufikisha hapa tulipo. Uteuzi wa viongozi na uendeshaji wa nchi hivi sasa haujali uwezo wa mtu bali ni itikadi yake. Ukiangalia kwa makini utaona kuwa top decision making positions zote serkalini zinashikiriwa na itikadi moja ( marais 2, makamu rais 2, waziri fedha, waziri ulinzi, waziri mambo ya ndani, mkuu wa polisi, jaji mkuu, mkuu wa mashushushu, wenyekiti na katibu chama tawala). Watu wa itikadi tofauti utawakuta kwenye nafasi za kati (mawaziri wa wizara zisizonyeti, mwanasheria mkuu nk), ambao wamegeuzwa watumishi wa mabwana waliopo juu. Hawa ndo wanatoa kauli tatanishi kuhusu ufisadi na kupambambana na ngumu ya umma kuwakingia kifua mabwana zao. Ni kama mtu na mbwa wako, unamridhisha kwa kumdondoshea mifupa. Hii itikadi ongozi ya hivi sasa imejipanga katika nafasi zote muhimu, nadhani wanalo jambo, siyo bure!
Sasa JK siyo mwenye maamuzi ya mwisho kwenye utawala wake, anasikiliza itikadi yake inataka nini, na mashauri mengine ni shinikizo kutoka nje ya nchi. Hali hii ndiyo inamfanya aonekane dhaifu na kushindwa kuwa kiongozi wa watanzania wote
 
Watanzania walio wengi wameapa kuwa ikiwa patatokea kundi linalojidai kutumia nguvu za umma kumuondosha Raisi Kikwete nao pia watatumia nguvu za Umma kuhakikisha kuwa anabaki madarakani hadi mwisho wa awamu yake.

Baadhi ya waTanzania hao walidai madai yanayotolewa na vyama vichache kuwa itumike nguvu ya umma kumuondoa Mheshimiwa Raisi Kikwete madarakani ni ya makundi ambayo yamepoteza muelekeo na sasa wanataka kulisambaratisha Taifa hili lenye utulivu na amani na kuliingiza kwenye vurumai lisilojulikana mwisho wake.

WaTanzania hao ambao wengi wao wanasema sisi ni wengi kuliko walioko kwenye hayo makundi wataonyesha ni namna gani nguvu za umma zinatumika kuhakikisha Raisi waliemchagua anaendelea kubaki kwenye madaraka kwani uhakika kuwa wingi wao ndio uliomueka madarakani upo palepale na ushindi uliopatikana sio wa kubabaisha au kupapasa ni ushindi uliotangazwa na tume na ambao ndio unaotakiwa uheshimiwe.

Sasa kutokea kwa vishambenga ambavyo vinajitutumua kwenye majukwaa kuwa peoples power itafanya kazi kumuondoa Kikwete madarakani ,wananchi hao walisisitiza madai yao kuwa wanawasuburi hao ambao watakuwa mstari wa mbele kuongoza nguvu za umma na wajiandae kukutana vilevile na nguvu za Umma upande wa Uraisi ,na wamesema watajuta kuzaliwa maana wao ni wengi sana na watakuwa hawana mswalie mtume ni kumlinda Kikwete tu mpaka kieleweke ,lakini hawatamuacha Raisi waliemchagua kuchezewa na watu wachache.
Asalamu aleykum sheikh Mwiba
 
Back
Top Bottom