Tutamlinda Kikwete pia kwa kutumia nguvu za umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutamlinda Kikwete pia kwa kutumia nguvu za umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 15, 2011.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Watanzania walio wengi wameapa kuwa ikiwa patatokea kundi linalojidai kutumia nguvu za umma kumuondosha Raisi Kikwete nao pia watatumia nguvu za Umma kuhakikisha kuwa anabaki madarakani hadi mwisho wa awamu yake.

  Baadhi ya waTanzania hao walidai madai yanayotolewa na vyama vichache kuwa itumike nguvu ya umma kumuondoa Mheshimiwa Raisi Kikwete madarakani ni ya makundi ambayo yamepoteza muelekeo na sasa wanataka kulisambaratisha Taifa hili lenye utulivu na amani na kuliingiza kwenye vurumai lisilojulikana mwisho wake.

  WaTanzania hao ambao wengi wao wanasema sisi ni wengi kuliko walioko kwenye hayo makundi wataonyesha ni namna gani nguvu za umma zinatumika kuhakikisha Raisi waliemchagua anaendelea kubaki kwenye madaraka kwani uhakika kuwa wingi wao ndio uliomueka madarakani upo palepale na ushindi uliopatikana sio wa kubabaisha au kupapasa ni ushindi uliotangazwa na tume na ambao ndio unaotakiwa uheshimiwe.

  Sasa kutokea kwa vishambenga ambavyo vinajitutumua kwenye majukwaa kuwa peoples power itafanya kazi kumuondoa Kikwete madarakani ,wananchi hao walisisitiza madai yao kuwa wanawasuburi hao ambao watakuwa mstari wa mbele kuongoza nguvu za umma na wajiandae kukutana vilevile na nguvu za Umma upande wa Uraisi ,na wamesema watajuta kuzaliwa maana wao ni wengi sana na watakuwa hawana mswalie mtume ni kumlinda Kikwete tu mpaka kieleweke ,lakini hawatamuacha Raisi waliemchagua kuchezewa na watu wachache.
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  ...sidhani wanaosema hayo walikuwa tayari kwenda Arusha kumtetea rais wao tarehe 12. Hao watu labda wawe green guards lkn hawawezi kamwe kuwa na ari na dhamira kama ya People's power.. hii nakuhakikishia.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Mambo vipi crapist.

  Leo haujaibiwa password?
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Arusha kama huelewi hakupingwa Raisi ,mlikuwa mnapigania kiti cha umea huko ,mlikutana na walinzi wa amani maana mambo ya kuuteketeza mji wa Arusha hamkufanikiwa ,ila hii mada inazungumzia Raisi,nyimbo ambayo mnaimba siku hizi kuwa mtumie nguvu ya Umma kumlazimisha Raisi aondoke madarakani,aloo msije mkajaribu,CCM ni wengi sana na wamezagaa nchi nzima na nao wapo tayari kwa hilo ,anytime mkitangazza nao wanazuka kutoka kusiko julikana tayari kumlinda Raisi wa Nchi hii alietokana na chama chao.
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Acha porojo zako. Watanzania gani hao waliosema hivyo, ni wa Msoga wakiongozwa na jk mwenyewe, rostam aziz, salva rweyemamu, ngereja, karamagi, chenge na n.k? Usituamshe tafadhali. Tuna hasira sana na vijitu kama wewe.
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mkuu mwiba..... kumekucha..... haya toa hii nimeisikia ..... nyingine je..?
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umehama lini CUF mkuu?
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndani ya miaka hii mitano ataondoka tu, we ngoja aendelee kuua watu wasio na hatia, ameanzia Arusha na sasa Wilayani Mbarali!
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hajahama. Unachokiona ni matokeo ya ndoa ya mkeka kati ya sisiem na kafu.
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umeishiwa kabisa. CCM mpo wengi? Rais aliyeko madarakani ni wa Watanzania analindwa na Watanzania na kama hawafai Watanzania basi hafai hata WanaCCM. kwani maisha magumu kama kupanda kwa bei ya vitu inawafusa watu kwa kutumia vyama vyao? mwanaCCM ananunua umeme ofisi ya CCM? Rais kama hafai hafai tu. Kwa taarifa yako hao wanaCCM unaodhani kuwa watamtetea JK ndiyo wa kwanza kumtosa.
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Mwiba unaionaje hali ya maisha inayomkabili mtanzania miaka 50 baada ya uhuru?kwa upande wako mambo shwari?fikiria pia wale waliopo vijijini
   
 12. afroPianist

  afroPianist Member

  #12
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hii jinsi ya kufikiri na lugha iliyotumika imeoana mno na ile taarifa ya ikulu iliyotolewa hivi karibuni kumpinga Dr.Slaa. Au ni wewe nini mkuu Salva Rweyemamu??! Hahaha...kazi nzuri!
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu Msiba, tatizo unazungumzia CCM kama vile una taarifa za ndani ila hujui wengine tuna access ya kweli kuhusu chama chako. Hao wafuasi wa CCM unaotutisha nao exist in your mind. Wakereketwa hawapo wamebaki watu wa maslahi. Hebu go back to the drawing board, mkuu, jaribu tena! Ila arguments hizi za sasa hazimtishi wala kumshawishi mtu.
   
 14. papason

  papason JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kilaza wa mwisho wee!!
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wewe vipi, awafikirie wa vijijini mbali kote huko. Kwa nini asijiangalie mwenye jinsi anavyoteseka na ugumu wa maisha wa kujitakia wenyewe!! Au mwenzetu anafaidi makombo ya wakubwa!!
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yakhe mimi ni Mtanzania nilie huru ,hivyo uhuru nilionao nautumia katika kutetea siasa zozote zile ,na pia nachangia Chama chochote kile ,pale nionapo siasa inafanywa na sio jazba,hivyo ninayo haki ya kusemea mawazo yangu na kuyalaza katika chama chochote cha siasa ,ikiwa ni zuri sitowacha kulisifu na ikiwa ni baya pia sitawacha kuliminyia.Ilivyokuwa mimi ni mpiga kura naamini kabisa kura yangu inathamani kwa chama chochote ,mimi ni mwananchi nilie huru ,hivyo uhuru wangu wauwezi kutekwa na chama chochote cha siasa, ikiwa hujajielewa na hujui faida ya wewe kuwa na nguvu ya kura ndio utabakia kuburuzwa kimawazo na kipropaganda na siki zote utabakia kwenye tumbaku na kasumba ya Chama kimoja tu,inaonyesha huelewei hata kwanini kunakuwa na kampeni wakati wa uchaguzi ,kwa jinsi wengi wenu mnavyoonekana mnahisi kuwa na kadi ya chama na kuwa mwananchama wa chama fulani basi ndio umeshauza kura yako na utu wako kwenye chama hicho.

  Maana kama Chama ni wanachama basi kusingekuwa na uhaja wa kufanya kampeni na hili ni lazima muliweke kwenye akili zenu,mwananchi anao uhuru na kwa uhuru huo anayo haki ya kuchagua pale ambapo anaona kutamletea maendeleo,sasa isiwe nongwa kuwa wengi wameichagua CCM ,ni bora kujipanga upya.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Umekusudia kusafiri ? Halafu unaposema ameua utakuwa hujui unalolisema,vyombo vilivyokabidhiwa ulinzi vya nchi ndio vyenye dhamana na hilo,maana kama mngefanikiwa kuivuruga na kuiwasha moto Arusha ,mkuu wa polisi angepoteza kazi au hilo hulijui.
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kutotii sheria na mamlaka zilizopo ndio chanzo cha vurugu zote hizo. Na hakuna nguvu ya umma wala nini, kinacho wasumbua ni kuwa vibaraka wa wanasiasa kwa kufuata kila kitu wanacho waambia. Chambueni pumba na mchele la sivyo mtakuwa mbuzi wa kafara kila siku huku wao wakifurahi na kugongeana cheers !
   
 19. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hivi ugumu wote wa maisha huu,serikali kuparaganyika,ufisadi uliokithiri,mishahara midogo,ukosefu wa walimu na vifaa vya kufundishia,uhaba wa dawa na vifaa tiba,shida ya maji,bei ndogo ya mazao kwa wakulima,serikali kuendekeza anasa na matumizi mabaya ya kodi za wananchi;hawa wanaojiita CCM hayawagusi?au ndo upumbavu....!
   
 20. MWAKIGOBE

  MWAKIGOBE Member

  #20
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya uma itumike vizuri na isiwe ni kwa ajili ya maslahi ya wachache. na iyo amani na utulivu usiwe wa kuhubiri tu
   
Loading...