Tutalalamika mpaka lini?

Achaneni na hizo habari tafuteni hela na my enjoy maisha..katiba haikunyimi pombe haikunyimi kucheza haikunyimi mapenzi sasa ya nini uhangaike nayo kwani wewe ni mwanasiasa?
Asante kwa maoni mkuu karibu tena
 
Nadhani swali la msingi sio "kwa nini Watanzania hawajaleta mabadiliko makubwa?" Bali "ni mazingira gani hufanya mabadiliko yatokee?"

Mifano uliyoitoa ya nchi kama

Philippines (1986),Sudan (2019), na Tunisia (2011).

Kwa kuongezea nchi za South Korea mwaka 1987 yalitokea maandamano ya amani yalichangia kurejesha uchaguzi wa moja kwa moja wa rais

Nchini Indonesia ulitokea mgogoro wa uchumi, maandamano ya wanafunzi na shinikizo la Wananchi vikachangia kuondoka kwa Suharto.

Zambia (1991): shinikizo la wananchi na vyama vya upinzani likaishia kwenye uchaguzi uliobadilisha uongozi.

Kwa Tanzania, mazingira hali ni tofauti. Kuna mjadala mkubwa kuhusu Katiba, mfumo wa uchaguzi, uhuru wa kisiasa na mwenendo wa baadhi ya kesi zenye maslahi ya umma, ikiwemo ya Tundu Lissu.

Watu wengi wanaona bado kuna nafasi ya maboresho, na wapo wanaohisi kasi ya mabadiliko haitoshi (hasa mitandaoni)

Pamoja na yote yanayoendelea na yaliyotokea October 29 2025 bado tatizo linaweza kuwa kuendea kutokana hofu ya athari za kisiasa kwa baadhi ya watu, kutokuwepo kwa mwafaka mpana juu ya ajenda moja ( Hili Chadema wamelizungumzia mara nyingi sana)

Tatizo jingine ni imani tofauti kuhusu njia bora ya kufikia mabadiliko. (CCM wamekuwa waongo kukubali mabadiliko na imefikia hatua Chadema wameamua kulipeleka hilo jambo kwa Wananchi, Wananchi nao hawajui wasimamie upande upi.

Mabadiliko ya kudumu mara nyingi hutokea pale ambapo wananchi wanaendelea kushiriki kwa njia za amani na za kisheria zikiwemokupiga kura, kufuatilia uwajibikaji, kushiriki mijadala ya sera, kuelimishana na kuunga mkono taasisi zinazofanya kazi ndani ya sheria.

Nguvu ya sauti ya wananchi huongezeka zaidi inapokuwa ya pamoja, yenye nidhamu na inayolenga suluhisho, sio vurugu.

Bado Watanzania hatujui tupo katika njia ipi. Na Mabadiliko kila nchi hutokea kwa njia tofauti. La msingi Watawala wajifunze kupitia historia za mabadiliko kutoka nchi mbalimbali.
 
Ni kutokujua tu nature ya binadamu na kupuuza somo la historia.

Asili ya binadamu ukimkandamiza lazima ataretaliate, historia inaonesha dunia imepata kuongozwa na wababe na mwishowe walianguka. Haitakuwa tofauti kwa CCM.

Kwa kilichotokea october 29, watu wamerudi kwenye drawing board, tujipe muda.
 
Una ulinzi ndugu maana hapa ndo tatizo lilipo???πŸ₯²
 
Una ulinzi ndugu maana hapa ndo tatizo lilipo???πŸ₯²
 
Bandiko lako limegusa hisia za wengi Mkuu, me nafikiri muda ndio muamuzi wa mwisho.. Kuna wengi sana wanafaidika na mfumo, wengine wananunulika kirahisi, wengine waoga wa kupitiliza, wakereketwa ni wengi pia ila ni kama mzani una balance au Kuna namna wanau balansisha kwa njia zao.

Siku wakereketwa wakiwa wengi kupindukia kuliko makundi mengine basi hakuna namna mabadiliko yatakuja.
 
Uzuo Uzi mzuri sana ,upo na maswali fikirishi mkuu
 
Tunashindwa kuungana?

Ndio.

Tunaogopa?

Ndio.

Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?

Ndio.
 
Nakubaliana na wewe mkuu
Wananchi wengi wanajua ni wapi wasimame ila watawala nao wapo makini wanawanyong'onyeza wananchi kwa kuwanyamanzisha
Wale wa kubwa wanaopaza sauti ili sisi wengi tuogope kwa kusema kama mti mbichi umefanywa hivi sisi je

Na wana tu win hapa
Haya yote yatawezekana tu kama katiba itaboreshwa tukapata tume huru na watu kuchagua bila wasi wasi nowadays mtu anasema hahangaiki kwenda kuchagua kiongozi maana mshindi anajulikana
Bado Watanzania hatujui tupo katika njia ipi. Na Mabadiliko kila nchi hutokea kwa njia tofauti. La msingi Watawala wajifunze kupitia historia za mabadiliko kutoka nchi mbalimbali.
Sisi sote tujifunze watawala na hata sisi wana nchi pia
Tuna safari ndefu ya kufikia matarajio yetu
 
Exactly tujipe muda
Na mijadala iendelee
 
Sawa mkuu ngoja tuone
Kama ulivyosema muda utaamua lakini tusiache kujadili pamoja wakati tukisubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…